Kunguni na Mende ndani ya basi la abiria!

Kunguni na Mende ndani ya basi la abiria!

TUJITEGEMEE

Platinum Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
27,472
Reaction score
28,338
Hivi majuzi nilibahatika kuzunguka baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara/Tanganyika kwa kutumia usafiri wa mabasi ya abiria.

Cha kusikitisha basi moja la kampuni fulani nililopanda lilikuwa na kungunguni wengi ajabu. Kunguni wale hawakuwa na aibu walikuwa wanatoka kwenye ma'cover'/foronya ya/za viti vya basi hilo na kung'ata mchana kweupe.

Wakati tunaanza safari hiyo basi lilikuwa halijajaa, Baada ya kuwastukia kunguni wale kwenye siti yangu nikaamia kwenye kiti/siti nyingine, kule ndo nikakumbana na kunguni watoto lakini 'barubaru' kwa kung'ata, Nikarudi kwenye siti yangu ya awali.

Sikuvumilia kung'atwa na kunguni wale bila kulalamika, nilimuita konda kumueleza kero ya kunguni kwenye basi lake. Kwa siri , konda, nikamuonyesha kikosi cha kwanza cha kunguni kilichokuwa kwenye egemo la mgongo wangu waliojibanza karibu na tobo la foronya la siti yangu. Akashtuka 'kiana', alichosema nikuwa basi lile alikabidhiwa jana yake.

Na jana hiyo kazi aliyoanza nayo ni kupambana na mende kwenye basi hilo waliokuwa wengi kiasi cha kutishia abiria kususia basi. Akanihakikishia kuwa na hao mende hakuwamaliza vizuri.

Mwisho wa mazungumzo yetu alimrudikia konda aliyekuwa anasimamia basi hilo hapo awali kwa usumbufu huo. Nilichokifanya, tulipofika sehemu ya kuchimba dawa, mimi nilishuka kwenye basi hilo na kwenda kuchimba namba za gari/basi hilo maana walikuwa hawajaandika namba za basi hilo kwenye tiketi/risiti ya nauli ya basi.

Nilisafiri kwenye basi hilo nikiwa roho juu, ingawa haikuwa mara yangu ya kwanza kuumwa/ng'atwa na kunguni! Niliwahi kungatwa nilipokuwa shule ya Bweni enzi hizo.

SWALI KWA WADAU:

1. Ni nani anahusika kuwawajibisha, wamiliki, makonda, hata madereva wa mabasi yenye kuhatarisha afya za wasafiri?

2. Mimi kama abira sikunyingine nikikumbania na kadhia ya namna hiyo nikashtaki wapi ili wawajibishwe wahusika kwa uzembe huo?

USHAURI:
Abira wote wa vyombo vya usafiri kuweni makini mnapopanda vyombo hivyo kwa kuhakikisha havina vihataraishi vya afya zenu kama, kunguni, mende, nakadhalika.

Update:
=======
Kama nilivyoahidi: ZUBE TRANS (Moshi-Mwanza), siti namba F1, T954 AHH: nauli 35,000/=

 
Teh teh teh teh teh umetisha mkuu pole! Nadhani hawa Sumatra wasiishie tu kuangalia mafuta Bali wahamasishe watu wa afya kwenda kukagua haya magari pia
 
Itakuwa basi la Mohamed Trans.
Mkuu nimejifunga makusudi kutotaja jina la kampuni kwa lengo jema tu, mamlaka zinazohusika zifanyie kazi suala hili kwa mabasi yote ama vyombo vyote vya usafiri wa abiria. Nadhani nawe ungefanya hivyo.
 
Bora ungeshuka kwa kuwa kunguni wakiingia nyumbani ni hatari kwani hawana adabu. Jirani yangu mtanashati lakini kila mara huanika godoro.kwa sababu ya kunguni. Amejaribu sana kuwaita wapuliziaji wa dawa lakini wapi.
 
Hujawahi kuwaona na Panya vile vile? Haya ma Bus yana siri nzito.
 
Bora ungeshuka kwa kuwa kunguni wakiingia nyumbani ni hatari kwani hawana adabu. Jirani yangu mtanashati lakini kila mara huanika godoro.kwa sababu ya kunguni. Amejaribu sana kuwaita wapuliziaji wa dawa lakini wapi.
Mkuu safari ilishafika mbali...na sikuwa na ujanja wa kubadilisha basi...!
 
Mkuu hao kunguni umeshawabeba sasa subiri vita yake . . Nakumbuka nilipanga chumba lakini nilikaa wiki 1 tu chumba kizima kunguni tu... Tena usiombe uvae nguo nyeupe ukitulia tu hao wameibuka.... Usiku haulali wanafujo sana hao wadudu
 
Mkuu nimejifunga makusudi kutotaja jina la kampuni kwa lengo jema tu, mamlaka zinazohusika zifanyie kazi suala hili kwa mabasi yote ama vyombo vyote vya usafiri wa abiria. Nadhani nawe ungefanya hivyo.

Mkuu woga wa kutokutaja jina la bus ni ujinga uliopitiliza!! Naomba utaje jina la kampuni, kutokutaja jina ni kulea huo upuuzi na hutaki kuwa suluhisho. Nafikiri suluhisho lianzie kwetu wenyewe, badala ya kuwakabdhi serikali kila jukumu! Inavyoonekana kuna watu watakabidhi serikali majukum ya kulea familia zao!!!

Nitashukuru kama utakuwa na busara kwa kutaja jina la kampuni, ili wajirekebishe, otherwise na wewe ni sehemu ya tatizo katika hilo bus!
 
Mkuu hao kunguni umeshawabeba sasa subiri vita yake . . ..

Kunguni tena!

Mambo ya kuleteana wadudu nyumbani

Yaani ni tabu tupu...! Kusafiri na basi hilo nikiwa roho juu ni kwa sababu nilikuwa nafikiria namna walivyonisumbua wakati niko shule ya Bweni. Nilipata shida sana.

Unajua shule kuna vituko kweli. Nilipofanya uchunguzi wakati nipo shule kuwa hao kunguni waliingiaje pale, jibu nililopata lilinishangaza sana. Ni kuwa kuna mwanafunzi mmoja alikuwa na usingizi sana. Alipojigundua kuwa lazima asome kwa muda mrefu kwa siku iliaweze kufaulu mitiahani yake, basi akalazimika kukodi/kutafuta jeshi la kunguni na kuwafugia kwenye kitanda chake ili wawe wanamuamsha...akasome. Kunguni wale walimfanyia kazi kwa weledi wa hali ya juu, maana mwanafunzi huyo alilazimika kukimbia kitanda chake mwenyewe akawa analala darasani.

Sasa nilipowakuta kunguni kwenye basi, sikuelewa, lengo lilikuwa ni nini...! (kama alikuwepo aliyewaleta mule kwenye gari kwa makusudi).
 
....

Nitashukuru kama utakuwa na busara kwa kutaja jina la kampuni, ili wajirekebishe, otherwise na wewe ni sehemu ya tatizo katika hilo bus!

Nadhani uko sahihi...nitataja jina la kampuni, namba ya gari, na namba ya siti lakini sitataja ilikuwa tarehe ngapi nilisafiri na basi hilo ingawa ni mwaka huu. Nitafanya hivyo kesho baada yakusikia maoni ya wadau wengine juu ya hili.
 
Mkuu Jitegemee mimi kwa uelewa wangu naona kama ni ujumbe mzuri unaohusu siasa yetu ya Tz.
 
Hukupiga hata kapicha ka ushahid mkuu?
Mkuu sikukumbuka kupiga picha...! Najua picha ingesema zaidi kuliko maneno...Unajua nilisafiri bila kufunga mkanda, kwani nilipojaribu kuuvuta ulipokuwa umekwamia kati ya siti yangu na ya jirani nikumbana nao...ikabidi ni salimu amri na kuuacha mkanda.
 
Back
Top Bottom