Kundi la Lowassa lajitokeza kwa NGUVU kamati ya Mwinyi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kundi la Lowassa lajitokeza kwa NGUVU kamati ya Mwinyi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bongolander, Nov 5, 2009.

 1. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Wakuu moja kati ya mambo ambayo bado hatujafikia kukubaliana humu dani ni kama EL amefutwa kabisa kwenye siasa za Tanzania au kuna uwezekano kuwa ni mbogo aliyejeruhiwa tu, ambaye akirudi kutakuwa na kizungumkuti. Hii habari ni copy and paste thing, kama ni duplicate naomba mod iweke inapohusika, lakini naona ina thamani kidogo ya kusomwa. Kuna mawili matatu yanapatikana kwenye magazeti ingawa asili yake ni hapa lakini yanaweza kutusaidia kuelimisha.


  *Yumo Naibu Waziri, wapinga ufisadi wataka watuhumiwa wang'olewe CCM


  Daniel Mjema, Dodoma


  WABUNGE wa CCM wameendelea kuparurana mbele ya kamati ya Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, huku baadhi wakimtetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na wengine wakisema watuhumiwa wote wa ufisadi wavuliwe nyadhifa za ndani ya chama.

  Mvutano huo umetokea wakati kuna malumbano makali yanayoendelea baina ya wabunge na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) juu ya kuwahoji (wabunge) kuhusu kupokea posho mbili kwa kazi moja.

  Hii pia ni muendelezo wa malumbano yaliyopo kuhusu utekelezaji wa maazimo ya Bunge juu ya hatua za kuwachukulia maafisa waliotuhumiwa kuhusika na kashfa ya zabuni tata ya kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura iliyotolewa kwa Kampuni ya Richmond.

  Mjadala huo mkali ulioanza saa 2:00 usiku hadi saa 7:30, huku baadhi ya wabunge wakichachamaa na kutaka baadhi ya vigogo ndani ya chama hicho wanaotuhumiwa kwa ufisadi wang鈥檕ke.

  Hata hivyo, inadaiwa kuwa kundi linalomtetea Lowassa lilijibu mapigo kwamba, hakuwa na makosa na mambo aliyotuhumiwa nayo yalitungwa kwa sababu ya wivu na uchu wa madaraka na kama njia ya kumwondoa katika nafasi yake.

  Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk Makongoro Mahanga na Mbunge wa viti maalumu, Bernadeta Mushahushu waliiponda ripoti ya Richmond kuwa iliandaliwa kummaliza Lowassa kwa wivu na uchu wa madaraka wa baadhi ya wana-CCM.

  Dk Mahanga ambaye ni Mbunge wa Ukonga, alisema ripoti hiyo ni feki huku akipendekeza Rais Kikwete aunde tume huru kupata ukweli akidai kuwa Lowassa alionewa.


  Wabunge waliitaka CCM iache kukumbatia viongozi wasio waadilifu na kutaka wote walio na tuhuma wajiengue au waenguliwe ili kurejesha imani ya Watanzania kwa CCM na Serikali.

  Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, zimeeleza kuwa mbunge wa kwanza kuwasha moto alikuwa Christopher Ole Sendeka wa Jimbo la Simanjiro.

  Inadaiwa kuwa mbunge huyo machachari alitaka Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa wawajibishwe kutokana na kuhusishwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi.

  Lowassa na mawaziri wengine wawili walilazimika kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na kuhusishwa na kashfa katika mchakato wa Richmond.

  Chanzo cha habari kimeeleza kuwa mbunge huyo alitaka pia kuenguliwa kwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba kwa kushindwa kusimamia chama kimaadili.

  鈥淥le Sendeka alienda mbali na kusema pamoja na nia nzuri ya serikali ya JK kupambana na ufisadi, Makamba haonekani kuguswa na tatizo hilo," kilidai chanzo hicho.

  Katika kikao hicho cha faragha, Mbunge wa Sumbawanga, Paul Kimiti aliwashutumu wabunge ambao ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), kwa kushiriki kumdhalilisha Spika wa Bunge, Samuel Sitta katika kikao chake kilichofanyika hivi karibuni.

  Alisema Sitta ni kiongozi mahiri anayeliongoza Bunge kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo na kumshutumu Mbunge wa Bahi, William Kusila kwa kitendo chake cha kumwita Spika kuwa ni laini.

  Kimiti alisema kama Nec ingemnyang鈥檃nya Spika kadi ya CCM na kumwondoa kwenye uspika, basi kauli ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere kuwa kusambaratika CCM kungeleta upinzani wa kweli na kwamba hapo ndipo chama imara cha upinzani kingezaliwa kutoka CCM.

  Kwa upande wake, Mushashu aliwabeza Wabunge wanaoitwa wapambanaji wa ufisadi na kudai kwamba vita ya ufisadi ni sera ya CCM na sio sera ya wabunge hao wachache.

  Alidai wabunge hao hawajatumwa na CCM na kutaka wawajibishwe na kumshutumu mmoja wa wafanyabiashara nchini (jina tunalo) na vyombo vyake vya habari kwa kushirikiana na kundi hilo.

  Mbunge wa Kalenga, Stephen Galinoma alilipongeza kundi hilo la wabunge wapambanaji wa ufisadi na kusema lengo lao ni takatifu na kumpongeza Sitta kwa kuliongoza Bunge kwa viwango.

  Kwa upande wake, Mbunge wa Longido, Michael Lekule Laizer alisema CCM kimepoteza maadili na kuna ubaguzi ulioanza kujengeka ndani ya chama.

  鈥淜una ubaguzi ndani ya chama katika kushughulikia wanachama wake鈥iongozi wanakaa kimya katika masuala ya msingi ya wananchi na kuwafanya wapoteze imani na serikali,鈥?chanzo chetu kilimkariri mbunge huyo.

  Mbunge huyo alipendekeza kuwa viongozi wote wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali wapokonywe nyadhifa zao ndani ya CCM, kwani kuendelea kuwepo kwao kunakipaka matope chama.

  Chanzo chetu cha habari kimepasha kuwa mbunge huyo alitahadharisha kuwa kama hatua za haraka hazitachukuliwa, CCM itagawanyika makundi mawili.

  Alifafanua kuwa, mgawanyiko huo utatokea kwa kuwa kila kundi linaonekana kutoyumba katika misimamo yake, jambo ambalo ni la hatari sana katika mustakabali wa chama.

  Kamati hiyo ya Mwinyi iliundwa na NEC ya CCM katika mkutano wake mjini Dodoma hivi karibuni, ili kuchunguza kiini cha mpasuko miongoni mwa wabunge wa CCM hali ambayo inatishia mshikamano wa chama hicho na serikali yake.
  Wajumbe wengine wa kamati hiyo ambayo imekwishahoji makundi mbalimbali ya wabunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa na Abdulrahman Kinana.

  Source Mwananchi 4 Nov 2009
   
 2. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  October 2007 niliandika hivi katika Gazeti la Thisday. Na hii ilikuwa kabla ya Ripoti ya Mwakyembe kuhusu Richmond.

  "Had the Richmond fiasco happened in the mature democracies, Mr. Lowassa would have hanged his prime minister's gloves long time ago. He would be tending his cows in Monduli and possibly writing the last chapter of his memoirs. By publicly and implicitly acknowledging that he somehow kept his eye off the ball during the emergency power procurement process, Hon. Lowassa does not merit good grades on the leadership scoreboard. The prime minister has also dismally and abysmally failed to shake off the notion that he was not above board when dealing with the emergency power project. But Tanzania is still a "kindergarten" democracy so Mr. Lowassa is going to stick around for a while.

  Mr. Lowassa does not have many options to maneuver on the Richmond deal. As a head of government he should come to terms with the fact that the emergency power project was bungled under his watch. He should take political responsibility, put to task his subordinates who might have"misled" him, swallow his pride and offer public apology so that we can put this scandal behind us. Akubali yaishe in Kiswahili.

  If the above prescription proves a bitter pill to swallow, Mr. Lowassa can opt for all night long prayers in the hope that come 2015 the likes of ThisDay Newspaper will not be around to invoke the Richmond ghosts. These ghosts will jog the public's memory to ensure the Richmond tale is still pending, unfinished business. 2015 will not be the time for the "it wasn't me" antics."
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Nov 5, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  kina Lowasa, wataweweseka sana mwisho wake ni kupata KIHARUSI tu, binafsi najua hawatarudi kutudanganya kwa sababu WATANGANYIKA wememjua adui yao wa Maendeleo ni genge la wana mtandao. na genge hilo linaongozwa na RA na Lowassa, watashindwa na kulegea. is up to them.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hivi hakuna mambo mengine ya kuongea jamani.Kila kukicha Lowassa ,mara Sitta mara Richmond...Mods please nakuomba kwa heshima na taadhima unifute humu JF nisiweze kuonekana tena..maana hapa kimekuwa ni kijiwe cha umbea sasa..Please naomba unifute
   
 5. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Kigogo unaniangusha mzee, usifutwe hamia kwenye jukwaa letu lile la jokes na mapenzi pia nakuomba usome signature yangu.
   
 6. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado sijaona nguvu ya kundi la akina Lowasa hapo. Kwa mtizamo wangu, naona kundi hilo limekosa nguvu kwa kiasi kikubwa sana kwani halina hoja tena baada ya mambo karibu yote kuwekwa hadharani.
   
 7. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kigogo unataka mambo gani yajadiliwe badala ya hawa?
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hawa unawaonea, Hawa hawakuwa na nguvu kubwa CCM kati ya 1961 na 2005. Je Nchi iliendelea kipindi hicho?.

  ADUI WA MAENDELEO NI CCM-Maana ipo tokea 1977 na kabla ya hapo wale wale waliojiita CCM walikuwa TANU.

  Adui wa maendeleo ni CCM-Fulstop
   
 9. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Tutapigishana kelele nani hafawi na nani afadhali...mwishowe tujuwe tu kuwa mtu hawezi kunukia uturi au manukato katika soko la samaki. CCM ndiyo iliyoshindwa kwa watanzania hata kama angeletwa nabii kuiongoza haingeliweza, kama ilivyo saa, kubadilika na kubadilisha chochote kwa wanachi wengi masikini wa tanzania
   
 10. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #10
  Nov 5, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kabla ya kuihukumu CCM ni vizuri tukakubaliana ni nani mbaya ndani ya chama hicho? Mambo haya hatukuyasikia kabla ya Lowasa kujiuzulu, inakuwaje leo hii yamepamba moto kiasi hiki?
   
 11. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #11
  Nov 5, 2009
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwani wewe Kigogo ulipojiregister JF ulimwambia Mods au wewe mwenyewe uliingia na kuiona JF babu kubwa, ukiona mambo yamekutinga na huo Ufisadi wako kwanini usijiengue mwenyewe kwa kutuaaga wana jamii------please men dont disturb Mods
   
 12. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #12
  Nov 5, 2009
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  HALAFU HUYU mahanga, si juzi juzi tu amekimbila mahakani, hivi kweli reasoning capacity yake iko ok, i dont think so, the guy must be insane------naona kila siku anahangika kuwatetea akina Lowasa, au RA Eddo mabwana zake, make Watanzania wote wanaona jinsi picha ilivo, na wanaona akina RA na LO wametukosea kwa kutufilisi, sasa yeye inakuaje au yeye sio Mtanzania?
   
Loading...