Kunasehemu nahisi tumewekewa pandikizi toka nchi jirani

concordile 101

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
1,242
2,000
Ukifuatilia matukio yanayoendelea sasa hivi Tanzania ni wazi kuna sehemu ndani ya ofisi zetu nyeti tumewekewa pandikizi ili uchumi wetu uyumbe kwa manufaa ya maendeleo ya nchi nyingine.

Ukifuatilia kuanzia matukio ya uuzaji wa mahindi, madini na hapo juzi tu korosho, ni wazi kuna nia ya dhati kuifilisi nchi yetu na isiweze inuka tena.

Ukienda zambia, Mozambique ,Congo na nchi kadhaa zinazotuzunguka idadi ya wafanyabiashara wanaohamia huko toka tanzania ni ya kutisha, sana.

Kwa mfano mji wa pemba nchini Msumbiji kwa mwaka jana nimeshuhudia zaid wafanyabiashara 20 ambao nilikuwa nawajua kariakoo wakifungua frame na wengine kupitiliza mpaka nampula na miji mingine.

Funika ni zambia, kuna watu kama watatu waliokuwa wanaingiza mizigo ya kutisha wamehamia zambia na wanakula bata na biashara sasahivi inalipa zaid hata walipokuwa Kariakoo.

Kwa sababu kule hakuna yale masuala ya kununua nguo 20 niuze 21 nipate faida ya 1. Kule nikinunua 20 nauza 25 faida ya kufa mtu na hakuna masuala ya tra kufuatiliana.

Tukija kwenye suala linaloendelea la bureau de change, bila siri hapa kuna ujambazi unaendelea kwa sababu.

Kama kweli ni kudhibiti kwanini

Wabebe pesa na kusiwe na kuandikishana

Kwanin camera zibebwe na wahahusika wataka kuficha ni?

Kwanini polisi wahusike kwenye haya masuala, kama ni hivyo hata kipind watu tra wanapokuja dai kodi watumwe na wanajeshi kuja kukusanya.

Kwanini iwe vuruuvaraa wakati ni mwaka juzi tu wamepitisha sheria mpya ya uendeshaji wa haya maduka?
 

Lyamber

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
10,412
2,000
Jamaa haridhiki aliona akipandisha mtaji watu wataanguka lakini watu bado wamekomaa sijui uwe na bilioni 3 lakini watu bado wanae sasa hivi anataka kufosi dola ishuke hii dola mwezi wa 4-5 itakaribia 2600-2700
 

kigogo warioba

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
5,700
2,000
Mchawi wetu mkubwa ni mzee baba, hataki kuambiwa, anachoongea ni tofauti kabisa na anachokifanya, atoe kauli ya hata ya kuachiwa na kufutiwa makosa akina mbowe matiko zitto, lissu na wangine, awashike mkono, asipofanya hivyo uchumi wetu utazidi kudorora, aweke kwanza amani!:oops:
 

concordile 101

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
1,242
2,000
Jamaa haridhiki aliona akipandisha mtaji watu wataanguka lakini watu bado wamekomaa sijui uwe na bilioni 3 lakini watu bado wanae sasa hivi anataka kufosi dola ishuke hii dola mwezi wa 4-5 itakaribia 2600-2700
hapa hakuna cha kutaka kushusha ila hapa kuna wizi unafanyika kwa kutumia mamlaka kaka. Rejea clouds na mercedes benz
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom