Kuna watu wanajua uchawi wa siasa nchi hii!!!!

Kuna watu wanajua uchawi wa siasa nchi hii!!!!

Bitilanga

Member
Joined
Oct 9, 2013
Posts
17
Reaction score
0
HATA MIMI NAWEZA KUVIUA VYAMA VYA UPINZANI!

Makala: Richard Manyota
KAMA uhai wa binadamu unavyojulikana upo katika viungo vipi ndivyo ilivyo kwa vyama vya upinzani nchini kwamba mwenye nia ya kuviua anafahamu pasipo shaka wapi pa kupiga na chama husika kusambaratisha.
Mfumo wa vyama hivyo ni wa mchungaji na kondoo, kazi ya adui ni kumpiga mchungaji na kondoo wa kundi kutawanyika; falsafa za Nabii Yesu ziko namna hiyo; nami nina jambo la kusema na vyama hivi.

Nianze na madai ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupitia viongozi wake siku za hivi karibuni kulalama kuwa, kuna njama za chama kikubwa cha siasa zinafanywa ili kukisambaratisha; kwangu mimi siyo nguvu ya chama kikubwa inayohitajika kukivuruga chama hicho; hata mimi naweza kukisambaratisha kwa ujuzi niliouleza hapo juu!
Bila hofu natamka kuwa, misingi ya vyama vingi vya siasa nchini imejengwa juu ya uwezo wa watu fulani ambao uwepo wao licha ya ubinadamu wenye upungufu, umewafanya waonekane na kujiona kuwa wao ndiyo vyama, wasipokuwepo uhai wa upinzani haupo.

Ukitaka kuviua unahangaika na kitu gani zaidi ya kumpiga mchungaji na kondoo wa kundi kusambaratika? Mbinu iko wazi cha ajabu wapinzani wanalalamika kudhoofishwa wakati misingi yao ndiyo inayowadhoofisha bila kujitambua.
Chama tawala ambacho mimi si mfuasi wake kimekuwa na misingi imara isiyojengwa kwenye akili za watu fulani ndiyo maana wanajipiga kifua kuwa watatawala milele hata kama uwezo wao wa kuongoza ni mdogo kama inavyosemwa!

Tafakari; ni nani asipokuwa mwenyekiti au katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), chama kitakufa, kusambaratika au kudhoofika?
Alikuwepo muasisi wa chama hicho, Hayati Mwalimu Julius Nyerere (Rais wa kwanza wa Tanzania), akang’atuka uenyekiti, chama hakikuyumba, Philip Mangula alishakuwa katibu wa chama hicho akatimuliwa, chama hakikuvurugika – sasa geuza makali, mnyoe Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na katibu wake Wilbroad Slaa, wapishe nafasi zao uone kitakachotokea!!!

Mwambie kwa upole Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahimu Lipumba na katibu wake Maalim Seif Sharrif Hamad wajitambue kuwa jua lao linazama kukaribisha giza, budi kwao kuwapa wengine kijiti cha uongozi uone kama chama hakitasambaratika!
Fikra za chama kina wenyewe na wenyewe ndiyo sisi haziwezi kufanya kazi kwenye ulimwengu huu wa kizazi cha kuhoji ukweli wa rangi; jielimishe kwenye matukio ya uasi yanayotokea kwenye baadhi ya vyama vya siasa nchini, msingi ni huo niliousema hapo juu.

Chama cha NCCR Mageuzi kilichokuwa moto Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, kilidhoofika, akatajwa mwenyekiti wake Augustine Mrema kuwa alihusika kukiua, huo ni mfano mwingine wa kile ninachosema; hajatokea Nabii Yesu na Mtume Muhamad wa pili kwenye dunia hii; viongozi kadhaa wakituhumiwa kuhongwa kukimaliza chama kosa ni kuwatukuza zaidi kuliko vyama husika!
Mpelekee Nape Nnauye mamilioni umwambie akihujumu chama uone kitakachompata, wala hakutakuwa na maandamano mahali popote ya kumuunga mkono kama upuuzi tunaouona kwenye vyama vya upinzani!
Ushauri wangu, vyama vya upinzani kama vinataka kuwa mbadala wa CCM iliyochokwa na wananchi kwa madai ya mitaani, lazima misingi yao ijengwe kitaifa. Kuwe na muongozo usiokuwa na tamaa, wenye manufaa kwa nchi na siyo viongozi fulani.

Lazima mkate wa chama ugawanwe na wote, uwe na faida kwa jamii na siyo watu wachache waliojifanya miungu ambao mwisho wa siku wakiulizwa matumizi mabaya ya nafasi zao ni haohao wanageuka kuwa wapokea rushwa kwa lengo la kudhoofisha vyama ili wao washibe. Nachochea tu!

MSIMAMO WANGU: Hii makala ni yenye akili sana, wenye kuelewa watakuwa wameelewa zaidi ya maandiko yanayosomeka hapo juu.
 
Back
Top Bottom