Kuna watu wanaishi vizuri sana, tembea uone

Dit000

JF-Expert Member
Apr 21, 2017
656
856
Wale mungu aliwowabariki wameweka 3D epoxy materials kwenye nyumba zao, unakuta lounge kubwa, rangi ndani nzuri, nyumba ndefu, bodi inang'aa taa za kwenye bodi unakuta wameweka zile nyeupe zina umbo kama sahani approxmetely 50cm diammeter zina mwaga murua, sofa kubwa za ngozi zimevalishwaa na romantic sofa covers, tv kubwa inchi 75 8K sony na hometheatre iko pale 7channels hapo ukivaa na yale mamiwani speshoo ya kuangaliazia tv, yaani watu unawaona kama live asee inapendeza sanaa

Ukiingia maliwato kule ndo unaweza usitoke dah!

Jamani tutafuteni pesa kwa bidiiii

Hizi hapa ni beachcomber hot tubes, ikiwa ndani ya unakolala utapata raha sanaa , ukiingia ndani huku maji yanazunguka maana yenyewe maji yake yanazunguka kama maporomoko so yanakuwa yanakutekenyaa mwili mzima , pembeni umeshikiria juice ya tendee ya baridi halafu kwenye ukuta kuna smart TV nzuri unaangalia taarifa ya habari, huku unafanya tahajudi ya ujio wa bwana yesu kristo bei zake ni dola 20000 sawa na tsh 48millioni, hii ni starehe ya kuoga tu

Yaani hapa unaweza kuwa kama uko mbinguni, unaoga masaa mawili badala ya dk 30,

moja - Copy.PNG


tatu.jpg
 
Back
Top Bottom