Nadhani hapo issue ni communication. Ongea unachopenda kifanyike, kwa sababu background habits needs polishing.
Naelewa pia kuna wanaume ambao kwenye mahusiano na ndoa changa walikuwa washauri wazuri kwa wake zao. Lakini as time went on, wakagundua walikuwa wanampigia mbuzi gitaa.
Usije kutamani kuishi na mwanaume ambaye mwanzoni wa ndoa alikuwa mshauri mzuri, lakini alivyoona ushauri wake hautiliwi maanani, akaingia kwenye silent mode.
Mwisho wa siku wageni wakija nyumbani wanasema, "mume wako mpole, hata haongei" kumbe ni silent mode.