Kuna watu sasa wanaingia mitandaoni baada ya kuchungulia kuna nini kimejiri leo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,673
149,860
Habari wadau,

Kuna watu walikuwa mstari wa mbele sana kumsifia Mkulu tangu wakati wa kampeni mpaka alipoingia madarakani.

Watu hawa walikuwa na matumaini makubwa juu ya bwana huyu ila kadri siku zinavyoenda anawangusha sana na kwakweli anawaweka katika wakati mgumu sana kumtetea.

Wanachofanya hawa wenzetu kwa sasa ni kuishi kama digidigi.Yaani wanavizia kama kuna tukio jamaa kalifanya basi siku hiyo wanatoka mafichoni na kumwagia sifa kedekede ila bahati mbaya mtu mwenyewe katika matukio 5 anayoyafanya,moja tu ndio linaweza kuwa zuri mengine yote ni taaabu tupu.

Baadhi yao watajikakakamua kwa kuanziasha mada kujaribu kumsfia na kuwaponda(kuwaonyesha wako wrong) wale wanaompinga lengo hasa likiwa ni kutaka kujaribu kuonyesha kuwa hawakukosea kumuunga mkono wakati wa kampeni na pia hawakukosea kumchagua.

Kwa mfano matukio ya huko Arusha leo hii yanawatia aibu sana na unaweza usiwaone kabisa hapa jukwaani bali wanasubiri wala tukio hili lipite au lipoe kisha ndio waibuke tena na mada za kujaribu kumsafisha.

Shukuruni tu sio wadanganyika wote wana access na hii mitando ya kijamii vinginevyo huyu mtu wenu angeumbuka vibaya sana 2020.

Poleni maana atawatesa sana kwa jinsi anavyoharibu kila kukicha.
 
ameharibu nini mkuu, jaribu kutumia lugha ya moja kwa moja sio fasihi majungu.
upload_2017-5-18_21-59-43.jpeg
 
Kwa sasa hawa jamaa ambao huja hapa JF kumtetea mtu wao wamekuwa kama kusanyiko fulani la WAJINGA ambao hawana mwelekeo.

More worse jamaa kila siku kama sio yeye mwenyewe anaharibu basi vijana wake type ya Gambo lazima walisanue kama leo.

Jamaa ana PEPO la UHARIBIFU..!!

Watakuwa na wakati mgumu sana hawa 2020.
 
Lengo lao ni kuwalaza ndani tu ili kuwakomoa na hamna kesi ya maana hapo hata wao wanajua.

Katika Uongozi ambao baada ya miaka mitano nchi utarudi nyuma miaka 50 ni huu utawala wa Mfalme Juha wa Nchi ya Giningi.Anajiona IQ yake kubwa kumbe anabomoa umoja wetu badala ya kujenga.
 
Katika Uongozi ambao baada ya miaka mitano nchi utarudi nyuma miaka 50 ni huu utawala wa Mfalme **** wa Nchi ya Giningi.Anajiona IQ yake kubwa kumbe anabomoa umoja wetu badala ya kujenga.
Yamemshinda sasa anatafuta sababu ikiwezekana abaki peke yake au abaki na walio dhaifu ambao hawatampa tabu wakati ukifika.
 
Back
Top Bottom