Kuna wanaodai hii wallpaper, picha ya kawaida tu ukiiweka kwenye simu yako kama wallpaper basi simu ya android itacrash

mikedean

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
2,526
2,000
Kuna wanaodai hii wallpaper,picha ya kawaida tu ukiiweka kwenye simu yako kama wallpaper basi simu ya android itacrash,je sababu ni nini na kuna picha za namna hii nyingi tu zinazoweza kusababisha simu kuwa nzito au kustalk tukiziweka kama wallpaper?

Kwa wataalamu sasa wa mambo ya teknolojia basi mkuje hapa,Wengine wanadai ni kwa sababu ya rangi,baadhi ya app za simu ziliibadili rangi kidogo ili ifit kwenye app zao.Tujadili.
IMG_20200605_085605.jpeg
 
ymollel

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
2,628
2,000
Kwanza hata haina resolution kubwa kivile kuifanya picha hiyo iwe kubwa. Halafu unaposeti wallpaper ya still picture huwa simu ina-Crop kulingana na mahitaji yake.

Wallpapers zinazofanya simu kuwa nzito ni zile zenye ANIMATIONS, Ambapo kama simu yako ina RAM au Processor ndogo , basi simu itakuwa nzito na baadae inaweza ku-freeze.

Pengine hiyo ilikuwa ni animated wallpaper lakini mtu akaiscreen shot ikawa static picture.

Otherwise..
Mimi nimeiweka hiyo wallpaper uliyoileta, sijaona tofauti na picha zingine za kawaida.
Screenshot_20200605-130804.jpg

From JF App
 
sjosh4

JF-Expert Member
Apr 10, 2020
848
1,000
Nimeona kuna jamaa anafanya review za simu na yeye kasema hii kitu
 
Stephen Chelu

Verified Member
Oct 31, 2017
4,633
2,000
Hii kitu hata mimi niliiona na jana na wakawa wametoa maelezo ni kwa nini inakuwa hivyo sema sikufuatilia kabisa.
 
mikumiyetu

JF-Expert Member
Aug 16, 2016
1,193
2,000

gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
1,553
2,000
Hiyo picha imefanyiwa utafiti na simu ngapi ili tujue uhakika wa hiyo taarifa.
 
mikedean

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
2,526
2,000
Nadhani ni baadhi ya simu za samsung ila sio zote,labda tunaweza kujiuliza why samsung na sio iphone,oppo,huawei etc?
 
Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
2,867
2,000
Kwanza hata haina resolution kubwa kivile kuifanya picha hiyo iwe kubwa. Halafu unaposeti wallpaper ya still picture huwa simu ina-Crop kulingana na mahitaji yake.

Wallpapers zinazofanya simu kuwa nzito ni zile zenye ANIMATIONS, Ambapo kama simu yako ina RAM au Processor ndogo , basi simu itakuwa nzito na baadae inaweza ku-freeze.

Pengine hiyo ilikuwa ni animated wallpaper lakini mtu akaiscreen shot ikawa static picture.

Otherwise..
Mimi nimeiweka hiyo wallpaper uliyoileta, sijaona tofauti na picha zingine za kawaida.
View attachment 1469307

From JF App
Ni kweli lakini ni ile OG yenyewe siyo ambayo umeidownload toka web nyingine au umeiscreenshot. sababu ni moja tu kuna pixel moja kwenye hiyo picha inafanya android os ishindwe ku handle color hivyo kucrash au kuifanya simu iingie kwenye recovery mode
 
mikedean

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
2,526
2,000
Pixels ndo nini mkuu hebu nifafanulie kwa ufupi

Kuna kitu kinaitwa color spectrum, kuna level ya rangi ambayo macho ya binadamu yanaona, vifaa vya simu kama android na printers vinatumia mfumo wa rangi unajulikana kama standardd RGB, kwa kawaida binadamu anaona zaidi rangi ya green kuliko red na blue so hata kwenye hizo device zina function kwa kufocus zaidi green kuliko red au blue. Kumbuka hizi ni primary color na ndizo zinatengeneza rangi nyingine zote kwa kuzichanganya.
Kuna formula ambayo android inatumia ili kudisplaya rangi kwa kuzichanganya hizi rangi tatu ili kutengeneza pixel moja baada ya nyingine. Pixel ni kile kidoti kimoja kinachotengeneza picha na picha imetengenezwa na pixels nyingi sana. Lakini mwisho wa siku hizi rangi inazichanganya kutoka na kokolea kwake so inazichanganya kwa percentage na mwisho wa siku ikijumlisha hizo percentage itapata mia na hiyo mia ni sawa na 255.
Sasa kwenye picha OG ilipigwa na camera ya canon siyo kwamba ina virus wala imekuwa tempered kuna pixel moja ilikuwa inaifanya simu inachanganyikiwa ikizichanganya badala ya kupata 255 inakuja 256, so simu inafreeze na android ilivyotengenezwa kamakuna error inabidi ifunga hiyo process, sasa kila ikifunga bado picha inakuwepo kwasababu umeiset kama wallpaper so error inajirudia mwisho wa siku simu inazima au inajipeleka recovery mode.
Mimi siyo mzuri katika kutoa maelezo lakini haya ni maelezo niiliyoyapata kwa expert mmoja mtaalam wa mambo ya simu ana channel kubwa youtube ya kureview simu hadi makampuni ya simu yanamlipa kwa kazi hiyo.
 
mikedean

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
2,526
2,000
Ahsante umeeleweka kaka.Nimekuelewa sana.shukrani,ubarikiwe

Ninja assasin

JF-Expert Member
Jul 2, 2018
1,217

Safi sana nimekupata
 
Joeli

JF-Expert Member
Apr 25, 2011
4,969
2,000
Ni kweli lakini ni ile OG yenyewe siyo ambayo umeidownload toka web nyingine au umeiscreenshot. sababu ni moja tu kuna pixel moja kwenye hiyo picha inafanya android os ishindwe ku handle color hivyo kucrash au kuifanya simu iingie kwenye recovery mode
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom