BLUE BALAA
JF-Expert Member
- Nov 30, 2010
- 1,222
- 786
Kuna Thomasi Nyimbo...
Rose Kamili
Mashishanga
Tundu Lissu - Huyu kutwa kupayuka kwenye vyombo vya habari badala ya kutumia vikao vya chama.
List goes on....
Mwanzishaji wa thread hii alikuwa na nia njema lakini wakina Sokomoko wanajaribu kudandia kwa lengo tofauti; ukweli Shibuda ni ccm damu damu, ameingia chadema baada ya ccm kumkatalia kugombea ubunge. Kama kungelikuwapo upenyo wa kukidhi haja yake hiyo bila ya kutoka ccm angelifanya hivyo. Katika hali hiyo siyo mtu wa kuamini moja kwa moja. Kuhusu Marando huyo kinachosababisha watu kumtilia shaka ni historia yake ya ushushushu. Na wengine wanakumbuka alivyowahi kuchaguliwa kuingia kwenye bunge la Afrika Mashariki kwa nguvu za ccm. Zaidi ya hapo mimi binafsi, huwa nashindwa kuelewa ni kwanini alifika mahali akaiachia nccr(M) kudidimia mikononi mwa Mbatia! Ukiyahunganisha yote hayo inakuwa wazi kwamba ni mtu wakufanya naye kazi huku ukiwa mwangalifu.
Si vyema kuwahukumu watu kabla ya kutenda kosa tena ni kinyume cha haki zote zinazofahamika duniani. Binafsi sioni sababu za kuwatilia shaka kwani chama kinaongozwa na kanuni na katiba itakayopambanua pumba na mchele. Kufanyia kazi usalama wa taifa si sababu tosha kwa Marando kuwa "stigmatized" na kumtazama Shibuda kama CCM damu nikum-stigmatize pia. Watu hugeuka kufuatana na mazingira yanavyojifungua. Hakuna aliyezaliwa CCM kama ilivyo kwa Chadema na vyama vingine ambapo wengi waliopo katika kambi ya upinzani leo ndiyo walewale waliokuwa makada wa CCM. Kina Maalim Seif, Lipumba na hata Rais wa mioyo yetu (Dr. Slaa) waliwahi kuwa makada wazuri wa TANU na CCM na sintashangaa siku moja kumwona hata JK akijiunga na upinzani kadiri mazingira yatakavyojifunua. Vile vile wengine wanaotajwa kwa niaya kuwafitinisha wana CHADEMA kwani hata mimi mwenyewe nilikuwa mshabiki na kada mzuri tu wa CCM nikiwa Jeshini hadi baada ya siasa za vyama vingi kuingia na kustaafu. Chadema tunapaswa kuvitumia vipaji na ujuzi wa waliokuwa makada wa CCM wanaouelewa vyema uimara na udhaifu wa CCM. Moja ya mbinu wanazotaka kutumia CCM kuimaliza Chadema ni kupandikiza hali ya kutiliana shaka na kusababisha vurugu ili kukiua au kukipunguza kabisa nguvu chama hiki pekee cha upinzani wa kweli. Nawasihi wana Chadema wa kweli tuachane na propaganda za wahuni na walaghai hao ili waambulie patupu.Wana JF mimi kuna wanachama wapya wa Chadema sina imani nao kabisa. I dont have any personal issues with them but I am uncomfortable with them. I dont real know what they have in their hearts. Ni bwana Mabere Marando na Shibuda. They are very good in politics game lakini sina uhakika kama kweli ni wapinzani. Naomba kama kuna mtu anaweza nitoa wasi wasi nao anieleze. Asanteni na kama kuna niliemkwaza anisamehe,
Wana JF mimi kuna wanachama wapya wa Chadema sina imani nao kabisa. I dont have any personal issues with them but I am uncomfortable with them. I dont real know what they have in their hearts. Ni bwana Mabere Marando na Shibuda. They are very good in politics game lakini sina uhakika kama kweli ni wapinzani. Naomba kama kuna mtu anaweza nitoa wasi wasi nao anieleze. Asanteni na kama kuna niliemkwaza anisamehe,
Mkuu Rev Masanilo naona leo umeamka VibayaSOkomoko ni shoga wa kiume!