Kuna wadada wengine wanashangaza kweli

Kuna wadada wengine wanashangaza kweli

Apitakujilamba

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2013
Posts
205
Reaction score
83
Habari zenu wana jamvi

Mapenzi ni jambo gumu sana hapa duniani na ndio maana mwimbaji mmoja aliimba mapenzi kizungu zungu, leo naomba nije na kisa ambacho kimeshawahi kunitokea kama kijana.

Kuna kipindi nilikuwa na uhusiano na dada fulani, ilitokea tu tulikutana sehemu tukaanzisha urafiki wa kawaida tu, lakini baada ya muda tukajikuta tumekuwa marafiki zaidi. Mara nyingi kwenye mahusiano kunakuwa na siri kubwa baina ya wapendanao, kila mmoja anajua ndani yake kwa nini yupo kwenye uhusiano huo.

Mimi nilimpenda yule dada, lakini mara nyingi napendelea kumtafiti mtu kiundani kabla ya kufall moja kwa moja, tuliendelea na urafiki wetu huku nikiendelea kumdadisi kama huyu dada atanifaa kwenye maisha. Nilikuwa najaribu kumuuliza vitu vingi lakini alikuwa ananijibu partially kwa hiyo sikufanikiwa kupata majibu. Lakini mara nyingi tunasema time will tell, baada ya muda nilikuja kugundua kuwa alikuwa na jamaa yake ila wamekorofishana. Na niligundua hilo baada ya jamaa kuamua kurudisha uhusiano kwa huyo dada. Dada alikuwa anakataa kurudisha uhusiano lakini huyo jamaa alimtumia dada yake huyu rafiki yangu kuwaunganisha tena (dada mtu ndiye alimuunganishia jamaa kabla na ndio hivyo baada ya kugombana alitumika tena kuwaunganisha).

Baada ya muda mambo yakabadilika, maana mawasiliano na yule dada yakapungua, kitu kizuri yule dada alikuwa huru kuniambia kitu gani kimetokea. Kiukweli yule mdada alianza uhusiano na mimi kwa nia ya kutaka kupunguza maumivu yake lakini baada ya kuwa na urafiki nami akajikuta ameingia kwenye mtihani achague yupi, arudi kwa jamaa au aendelee na mimi. Nakumbuka siku moja nilikuwa nae mjini mara tukakutana na mdogo wake yule jamaa, aaaah yule mdogo mtu akaripoti kwa jamaa..... siku walioonana na huyu dada alichezea kipigo cha haja.

Baada ya kumuona dada hana maamuzi ni kama aelewi nini afanye nilibidi mimi nifanye maamuzi ingawa yalikuwa magumu maana nilikuwa nimeshampenda yule dada. Aisee niliamua kutompigia simu na wala kutopokea simu yake kwa kipindi kirefu tu. Alijaribu kunitafuta bila ya mafanikio, nilifanya kila njia nisimuone wala asinione. Ofcourse nilitengeneza mazingira ya dada kuendelea na jamaa yake kwa amani. Baada ya mwaka mmoja, yule dada aliniandikia email kwamba anaolewa na anaomba niende kwenye haruc yake. Nilimtakia kila la heri na kumhaidi kwamba nitahudhuria lakini siku hiyo nilipata udhuru sikuhudhuria.

Baada ya ndoa, mawasiliano yakawa ya kawaida maana nikajua tayari ameolewa kwa hiyo haina shida kwangu wala kwake. Kwa hiyo siku akijisikia kupiga simu atapiga mi nitapokea. Nakumbuka siku moja nikampigia simu nikamtania nikamwambia nimeoa ila samahani nilikuwa cjakutaarifu uhudhurie mmmmh yule dada alibadilika sauti ikabadilika na hapo hapo akakata simu na hakupokea tena.

Baada ya kitambo kidogo sikumbuki nilimpigia au alinipigia lakini nikamwambia kuna siku nilikutania ila mi bado sijaoa nikashangaa dada kafurahi utafikiri nini nikashangaa nikasema yaaani umeolewa halafu hutaki mi nioe. Nilijaribu kumdadisi vizuri maana yule dada hanifichagi kitu, akaniambia siku ile nilivyomwambia vile siku nzima alikuwa analia, nilimuuliza kwa nini jibu lilikuwa anajuta kwa maamuzi aliyofanya.

Hapo lawama zikaanza kuniangukia, kwamba mimi ndio nimesababisha mpaka ameolewa na mtu ambaye hafurahiii ndoa. Alinilaumu kwa kutopokea simu zake kipindi hicho na alinitafuta bila ya mafanikio, kiukweli nilimwambia nilikuwa nakupa muda wa kufikiri maana ulikuwa hauna jibu sahihi. Alinieleza mengi ambayo yanamfanya haione ndoa chungu, lakini nilimtia moyo amwombe mungu maana WE HAVE OUR DREAM BUT GOD CREATES DESTINY.
 
Hata sikuelewi kabisa eti unasemaji? ulipokuwa unanilia pale kwenye mti mkubwa kila nikipita leo unakuja kuandika hapa kurasa 10 zote.
 
Tatizo la wanawake wengi wakati wa uchumba jua mko wawili anatega huku na huu atakayeanza ku propose ndo huyo huyo anabeba mzigo, majuto huja baadaye
 
kwa hiyo unataka tukushauri kitu gani?
 
Hata sikuelewi kabisa eti unasemaji? ulipokuwa unanilia pale kwenye mti mkubwa kila nikipita leo unakuja kuandika hapa kurasa 10 zote.

ha! ha! ha! ha! ha!
anajifariji na hakupati ng'ooo jinsi nilivyokuteka!
 
Yaani afadhali wanawake nao wafanye hivyo. Kwa miaka mingi wanaune wamefanya hivyo, wachumba tele afu mnashangaa anaoa mwingine kabisaa!
Tatizo la wanawake wengi wakati wa uchumba jua mko wawili anatega huku na huu atakayeanza ku propose ndo huyo huyo anabeba mzigo, majuto huja baadaye
 
....utaota manundu we endelea chart nae ....nawe oa unasubiri nini?
 
Hapo hamna ndoa hapo nashangaa walio comment juu yangu wote hawajaliona hilo!!!nina wasiwasi na wewe mkuu umeshakula na kitakachofuata ni kumbambia watoto muoaji

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
ulishndwa kung'amua ni kpindi gani alikuhtaji zaid kwasababu hsia zilitawala ubongo wako zaid ya uhalisia.
 
Tatizo la wanawake wengi wakati wa uchumba jua mko wawili anatega huku na huu atakayeanza ku propose ndo huyo huyo anabeba mzigo, majuto huja baadaye

Haina guarantee, whether amechagua A au B, ndoa yoyote Ina ups and downs. The good thing ni kwamba ameolewa.
Hata angeolewa na mleta thread nadhani kwa namna moja au nyingine angeface problem ile ile ya kujuta na kudhani alikosea, pengine aliyemuacha ni right choice.
 
Mwambie kule alikoolewa ndipo Destiny yake ilipo. Hata ungemuoa wewe angekuwa na vilalamishi Fulani Fulani. Huyo anadhani ndoa is all about roses!!
 
Ila bado unampenda eeh, unatamani ndoa ivunjike eti.
hehee
 
Hiyo habari huwakuta wanawake wengi...wengi huolewa sio kwa kuwa wanawapenda sana hao waliowao bali kwa kuwa wanhitaji tu kuwa ndoani na hao waliowaoa.
 
naomba mungu aniepushe mbal na haya majanga ya wanawake..(akil zao fupi mno)
 
in short huyo dada alifanya maamuzi ya haraka kuolewa kwa sababu alikuwa hajielewi ni nani hasa anamfaa na inawezekana wewe ndio ulikuwa chaguo lake but kutokana labda ushawishi alioupata kutoka kwa ndugu zake aolewe na huyo mtu wake na ukizingatia wewe umemchunia akawa hana jinsi ikamlazimu aolewe, bado anakupenda ila unatakiwa ukae nae mbali coz ni mke wa mtu. What is done is done have to move on with your life acha kuwasiliana nae.
 
Back
Top Bottom