Kuna vyeo/nafasi huwa sizielewi serikalini

Mfano mzuri ni bodi ya wadhamini. Au msajili wa hazina. Kwa wenye uelewa mzuri wa urasimu serikalini mtufahamishe. Ongezeeni na vyeo vingine
Bodi ya Wadhamini au Board of Trustees hazipo serikalini tu...hata kwenye private sectors...hao ndo wababe wanaosimamia muelekeo mzima wa organisation..we elewa kuwa hao ni kama miungu-watu flani hivi
 
mwandishi wa hotuba wa rais simuelewi wakati rais anatoa hotuba kichwani
Kutoa kichwani inategemea aina ya tukio au sehemu lakini katika matukio nyeti kama vikao vya kimataifa au semina lazima asome hotuba akiacha akibolonga hilo ni lake lakini kama anaongea na wananchi wa Chato aandikiwe hotuba ya nini wakati mwingine anatiririka kisukuma. Juzi pale chuo si alikuwa na hotuba aliyoandikiwa akasema hawezi kuitumia ile kwakuwa inamnyima uhuru wa kuongea sasa mukhali ulivyopanda sio akalikoroga kuhusu wale watoto wa udom aliwaita vi.ra.za? Labda ungesema MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA. Hivi huyu ana kazi gani kwa sasa? Maanda kusajili ukishaandika kwenye daftari ambayo ni kazi ya dakika zisizozidi 5 unakaa ofisini kufanya nini? Kutokana na kukosa kazi ndio maana juzi juzi akaona ahamie kuwa msemaji wa rais kwa kufafanua hotuba ya rais
 
kweli kabisa mkuu JPM haitaji mwandishi wa hotuba ...
Ndio maana katika hotuba anarudia rudia suala hata mara tatu, mara anasema anamaliza mara anaendelea kueleza jambo kwa urefu na kujirudia rudia.
 
Vyeo vyote hivi vina maana kwa wanaojua majukumu yao ni nini, lkn kwa wasiojua majukumu yao inakuwa vigumu kwa mtu wa nje kujua umuhimu wake, na shida tuliyonayo nibkuwa vyeo vingi serikalini wstu hawajui majukumu yao, wao ni kupiga deal tuu.
 
Meya Wa jiji, Meya wa manispaa ya ilala, Temeke, Kinondoni, Mkurugenzi Wa jiji, Mkurugenzi Wa manispaa ya Ilala, Temeke, Kinondoni
 
Mkurugenzi wa halmashauri, mwenyekiti wa halmashauri, mkuu wa wilaya.

Non sense.
 
Back
Top Bottom