RAY DONOVAN
Senior Member
- Jul 2, 2015
- 153
- 147

Kuna tuhuma kuwa baadhi ya viongozi wa awamu iliyopita na wengine wa awamu hii wako kwenye payroll ya serikali ya Egypt ili kuzima au ku sabotage kwa namna mbali mbali miradi ya kilimo cha Umwagiliaji na matumizi mengine ya maji toka ziwa victoria
Baadhi yao wako ndani ya idara mbali mbali za serikali na maslahi yao ni kwa ajili ya serikali ya Misri na sio Tanzania
Imefika mahala baadhi ya miradi imepigwa chini na watu wa idara ya mazingira kwa visingizio mbali mbali kuwa ili watanzania wasitumie maji ya aiwa victoria
Naomba wenye kujua undani wa haya madai watujuze kwa nini tumewekewa restriction kutumia maji wakati Ethiopia na Sudan wanaendelea na miradi mikubwa mikubwa ya Umwagiliaji na Mabwawa makubwa ya umeme na kadhalika huku sisi tunaambiwa kuwa maji kwenda Shinyanga na mikoa mingine haiwezekani kwa kiwango cha kutosheleza wananchi.
Huko juu Ethiopia wao wameamua kujenga na KUMALIZA kujengaBwawa la umeme kubwa kuliko yote Africa kwenye mto Nile ambao chanzo cha maji yake ni huku kwenye ziwa Victoria
SHERIA
Kuna watu watakuja hapa kukujazeni ujinga wao kuwa kuna mkataba wa 1929 ambao lazima sisi tuuheshim
Ukweli ni kuwa:
1. MKATABA ulikuwa kati ya serikali ya kikoloni ya UINGEREZA na MISRI
2. Kuna mkataba wa Vienna wa The Vienna Convention on Succession of States in Respect of Treaties, ibara ya 16, inasema kuwa mataifa huru au yaliyopata uhuru kama TANGANYIA/TANZANIA hayahitaji kurithi treaty obligations of its colonial power.
Someni mkataba wa Vienna ambao sisi ni signatory na link hii hapa:
http://legal.un.org/ilc/texts/instruments/english/conventions/3_2_1978.pdf

