Kuna upendo au hakuna upendo katika maisha yetu?

Kuna upendo au hakuna upendo katika maisha yetu?

Mjusi Sharobalo

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2025
Posts
8,278
Reaction score
14,559
Kuna muda nakaa chini na kufikiria kwa umakini sana kichwani mwangu, upendo wa kweli ni hadithi za kufikilika zisizo na ukweli ndani yake au ni kweli upendo wa thati upo katika maisha yetu, binafsi mimi huwa napenda lakini sijawahi kukutana na mtu aliyenipenda kwa dhati katika utu uzima huu labda utotoni, kiasi kwamba huwa nafikiria huenda ni mimi pekee duniani mwenye moyo wa upendo,

Hili huwa linanipa tafakuri nzito sana kichwani mwangu, je watu huwa wanapenda kweli au ni maigizo tu kama tuliyozea kutazama kwenye filamu za Kikorea na Kihindi, na kama wanapenda kweli kwanini watu wengi huwa wanawaumiza watu wanaowahitaji na kuwathamini katika maisha yao?,

Kama wewe unaamini kama ninavyo amini mimi hakuna upendo wa dhati, au unaamini upendo upo na huwa unapenda na kupendwa utupe muongozo hapa tuufahamu labda hatuujui upendo ni nini!...
 
Upendo ni dhana ya kufikirika ,ambayo binadamu kamwe hatokaa kuifanya wala kuifikia , level tofauti za maisha zinaonyesha hakuna kitu kinaitwa upendo
 
Back
Top Bottom