Kuna uhusiano gani katika hili? Msaada tutani

Kuna uhusiano gani katika hili? Msaada tutani

Mkuu hata kama ungembeba, kisingebadilika kitu. Na huwezi kubadilisha kifo cha mtu kwa kuchukua hatua mbadala, kwa sababu wewe sio chanzo. Hiyo intuition yako itumie kuwasaidia walio hai kama unavyofanya sasa hivi, lakini ukiona inakuletea woga na kujitenga, jua hiyo ni phobia yako ya utotoni ndiyo tatizo haswa.
Sawa mkuu, kama nimekuelewa ni kwamba nisijaribu kujishughulisha na jambo ambalo Sina uwezo nalo.
 
Sasa unataka kufanya nini? Kwamba umueleze kuwa unakaribia kufa? Je utaeleweka? Au unataka kuitwa mchawi kwamba ulisema jamaa atakufa na kweli akafa?

Au unadhani unaweza badilisha hatima yake,kwamba ukimwambia inaweza kumuokoa na kifo,,hiyo kitu hakuna ikifika siku yako imefika,je kuna mtu angetaraji Lissu angekuwa hai,lakini siku yake bado,unakumbuka ile ajali ya ndege india,wakati ndege inapaa ikaungua,akapona mtu mmoja tu,basi jua kifo ni fumbo kubwa sana,kwahiyo wewe just observe mambo tu lkn huwezi badilisha chochote
Asante sana mkuu, kwa ushauri huu najaribu kujenga justification kwamba it's not my fault and I can change nothing.
 
Duuh! Sawa mkuu najaribu sana kukuelewa.

Kuna kipindi nilikua naota karibia Kila siku nakutana na watu wawili wamevaa mavazi meupe namimi pia nimevaa mavazi meupe kama wao jumla tunakua watatu, Lakini nikiwaangalia wale watu wanaonekana ni transparency namimi pia nakua transparency kama wao.
Nilikua napiga nao story nyingi sana alafu Kuna muda ni kama wanataka kuondoka ila Mimi natamani kuendelea kubaki nao, maana mazingira ya kule ni amani alafu ni Raha sana. Bhasi mmoja wapo alikua ananigusa begani najikuta nashtuka nipo kitandani na tayari ni alfajiri.

Hii pia ni Moja ya kumbukumbu ambayo iliniacha na gepu kubwa moyoni maana wale watu hawaji tena. Na ilitokea hivyo baada ya kuanza kuyachukia maisha ya hapa duniani Yaani nilikua natamani niwe naonana na wale watu. Je! Unaweza kuwa na uzoefu wowote na hii Hali?
Kwahili hapana sina uzoefu nalo
 
Back
Top Bottom