Kuna tofauti yoyote kilichoiua news of world na walichofanya mwanahalisi?

babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
5,221
3,167
Britain's biggest selling Newspaper and has more than 160 years on the business.Kutokana na scandal ya phone hacking News corporation ambayo inamilikiwa na Murdoch wamehamua kulifunga

Kuna tofauti yoyote walichofanya Mwanahalisi dhidi ya kupata habari kati ya Zitto, Rostam Aziz na wengineo? Na sheria zetu zinasemaje kwenye hili?

News of the World closed down: David Cameron orders judge-led inquiry into phone hacking allegations

David Cameron this morning announced a judge-led inquiry into the News of the World phone hacking scandal as he admitted turning "a blind eye" to the crisis in the British press but refused to apologise.

In his first public statements since yesterday's announcement that the Sunday tabloid is to close, the Prime Minister said he would appoint judge to investigate the phone hacking allegations and promised "no stone will be left unturned".

Mr Cameron announced a second inquiry, to begin immediately, into the "culture, practices, and ethics" of the press, and said that the Press Complaints Commission would be replaced with a "new system entirely." He added that phone hacking may have taken place at other newspapers besides the News of the World.

The Prime Minister compared the scandal to MPs' expenses and said he and other party leaders "did not do enough" - but refused to apologise for his handling of the situation.

He said he took "full responsibility" for bringing Andy Coulson, the former News of the World editor, into Downing Street. Mr Coulson is widely expected to be arrested later today.

Mr Cameron added that he "would have accepted" the resignation of News International chief executive Rebekah Brooks, which was reportedly offered last night.

SOURCE: THE TELEGRAPH

Zitto ahusishwa na Rostam





Na Ezekiel Kamwaga - Imechapwa 15 December 2010



ZITTO Kabwe, naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amekuwa na mawasiliano ya karibu na na mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, imefahamika.

Kufichuka kwa taarifa za mawasiliano kati ya Zitto na Rostam kumekuja wiki moja baada ya gazeti hili kuchapisha mawasiliano kati ya Zitto na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa nchini (TISS), Jack Zoka.

Aidha, kufichuka kwa mawasiliano kati ya Zitto na Rostam kumekuja siku mbili baada ya mama mzazi wa Zitto, Shida Salum kunukuliwa akisema, "Mwanangu ni mkorofi."

Mama Zitto alikieleza kikao cha Kamati Kuu (CC) ya chama chake kilichofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, "Namfahamu mwanangu. Ni mkorofi. Si msikivu."

Kwa mujibu wa rekodi ya mwingiliano wa simu za mdomo na maandishi (sms) kutoka kwa Zitto kwenda kwa baadhi ya vigogo wa ngazi ya juu serikalini, TISS na Rostam, watu hao wawili wamekuwa wakijadiliana mambo kadhaa.

Miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakijadiliwa na viongozi hao, yanahusu CHADEMA, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na taifa kwa ujumla.
Rostam ambaye CHADEMA imekuwa ikimtuhumu kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi, ni mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM.

Gazeti hili limeshindwa kujua mapenzi ya Rostam kwa CHADEMA hadi kujipa jukumu la kujadiliana na Zitto juu ya "uhai bora" wa chama hicho.
Kwa mfano, Zitto na Rostam walifanya mawasiliano ya simu mara tano hapo tarehe 11 Agosti 2010. Simu iliyotumika katika mawasilino hayo, ni Na. +255756809535 ambayo hutumiwa na Zitto na +255754555555 ambayo hutumiwa na Rostam.

Mawasiliano hayo yalifanyika saa 07:08:35, saa 22:09:02, saa 22: 28: 39, saa 22:49:54, saa 22:44:37 na saa 22:45:09.
Wakati mawasiliano hayo yanafanyika simu ya Zitto ilikuwa inasomeka kuwa yuko Uzunguni, Dodoma, huku simu ya Rostam ikisomeka kuwa ilikuwa Area D, Dodoma.

Mawasiliano mengine yalikuwa katika maeneo tofauti. Mathalani mawasiliano ya Zitto na Rostam yalyofanyika 30 Novemba 2010 yalionyesha kuwa Zitto yuko Ohio, Ilala, Dar es Salaam. Yalifanyika saa 14:58:42, saa :16:41:58, saa 15:38:00, saa 16:09:56 na 17:48: 35.

Mawasiliano mengine ya Zitto na Rostam yalifanyika siku mbili kabla ya wabunge wa CHADEMA hawajakutana Bagamoyo.

Mawasiliano hayo yalifanyika tarehe 7 Desemba 2010 saa 07: 57:27, saa 14:32:08, saa 09:44:36 na saa 14:07:07.

Haijaweza kufahamika pia kiini cha mawasiliano kati ya Zitto, Zoka, Rostam na vigogo wengine wa serikali, CCM na usalama wa taifa.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu kutoka ndani ya kikao cha CHADEMA, awali mama Zitto alieleza masikitiko yake kuhusiana na taarifa mbalimbali zinazomhusu mwanawe.

"Najua mwanangu ni mkorofi. Lakini kuna njia ya kufanya kuliko kukitia chama msukosuko…Kila mara Zitto, Zitto, Zitto. Haya mambo hayana faida kwa chama," alieleza.

Hata hivyo, vyanzo huru vya taarifa vimeeleza MwanaHALISI kuwa mpango uliopo ni kumtumia Zitto "kusambaratisha CHADEMA."
"Kaka, nakuhakikishia kuwa upo ushahidi wa kutosha kwamba Zitto anatumika kuvuruga CHADEMA. Kuna baadhi ya vigogo ndani ya CCM na serikali, wanaomtia ujinga kwa kumueleza, ‘kwa hali ilivyo ndani ya CCM, wapo baadhi ya watu wanatamani kuondoka. Lakini hawawezi kwenda CHADEMA kwa sababu kinaongozwa na Mbowe (Freeman Mbowe),'" ameeleza mtoa taarifa.

Anasema, "Hivyo wanampampu Zitto kugombea uenyekiti. Wanataka Mbowe ang'oke na CHADEMA kisambaratike. Ni kwa sababu, wote wanaomtumia Zitto, wanajua kuwa huyu bwana mdogo hana uwezo wa kuongoza CHADEMA na haaminiki."

Akiongea kwa kujiamini, mtoa taarifa anasema, "Ni mbinu zilezile zilizotumiwa NCCR- Mageuzi, ambapo baadhi ya vigogo wa idara ya usalama wa taifa walitumia fedha ili kumng'oa Marando (Mabere Marando), katika uongozi wa chama."

Anasema taarifa kwamba wapo watu wanataka kuondoka ndani ya CCM na kujiunga na CHADEMA ni mkakati unaosukwa kwa ustadi mkubwa na baadhi ya vigogo wa serikali kwa kushirikiana na usalama wa taifa.

Inadaiwa ni katika mkakati huo, ndimo linapatikana jina la Rostam ambaye uongozi wa juu wa chama hicho umekuwa ukimtuhumu kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi nchini.
"Unajua ndugu yangu hapa Tanganyika, Rostam angependa sana awe na uwezo wa ku-control vyama vyote vinavyokua, hasa CHADEMA kwa sasa; ingawa uwezo wake wa kupenyeza unakuwa mgumu.

"Mkakati wake ni kumweka mtu wao katika uongozi wa juu wa CHADEMA ili waweze kumuendesha. Mpango huo ukifanikiwa, kina RA (Rostam) wataacha ugomvi na CHADEMA. Kwa sasa mtu wao ni Zitto. Na kuna mambo mengi ya siri ambayo RA amekubaliana na Zitto," anaeleza mtoa taarifa mmoja ambaye yuko karibu na Rostam na Zitto.

Mjadala juu ya mwenendo wa mashaka wa maisha ya kisiasa ya Zitto, uliibuka baada ya katibu wa wabunge wa CHADEMA, John Mnyika kuwasilisha taarifa ya shughuli za kamati hiyo mbele ya Kamati Kuu.

Kikubwa kilichojadiliwa ni hatua ya Zitto kuongoza kikundi cha baadhi ya wabunge kusaliti maamuzi halali ya kamati ya wabunge wa chama hicho.
Zitto anatuhumiwa na wabunge wenzake kutotii agizo la kutoka nje wakati Rais Jakaya Kikwete anahutubia Bunge, 18 Novemba 2010.

Katika taarifa yake kwa CC, Mnyika alisema katika kushughulikia suala hilo, hakukuwa na lolote la kuviziana kama ambavyo baadhi ya wajumbe wamedai.

"Hakuna kanuni iliyovunjwa, wala hakuna kinachoitwa kuviziana. Wabunge walikuwa na hasira sana juu ya hatua ya Zitto na wenzake kutotii agizo la kamati na kupita katika vyombo vya habari kupotosha ukweli," alisema Mnyika kwa sauti ya upole.

Akiongea kwa sauti ya kusisitiza, Mnyika alisema, "Mheshimiwa mwenyekiti, kwa kweli, wabunge walitaka hata kuwapiga wabunge walioasi makubaliano yao. Uongozi wa Kambi ukafanya juhudi kulipeleka mbele suala hili, angalau kupunguza munkari wa wabunge," alieleza.
Ni katika kikao hicho cha wabunge kilichofanyika Bagamoyo, ndipo wabunge walipiga kura ya kutokuwa na imani na Zitto.

Kile kilichoitwa, "kuviziana" kiliibuliwa ndani ya kikao cha CC na Dk. Kitila Mkumbo, ambaye amenukuliwa akisema ameshutushwa na hatua ya wabunge kumhukumu Zitto wakati ni mgonjwa.

Alikuwa ni Benson Kigaila, mjumbe wa CC aliyeeleza viongozi wenzake umuhimu wa kujenga chama imara badala ya kuangalia mtu.
"Mtu aliyekosea, lazima aadhibiwe. Tusiangaliea kama ataanguka, au atanufaika. Kwa muda mrefu, chama hiki kimenufaika kwa makosa ya CCM, ambapo kutokana na makundi yanayokinzana, wameendelea kukumbatia maovu. Ni lazima chama kichukue hatua za kukabiliana na magenge haya," alieleza.

Mjumbe mwingine wa CC aliyeongea kwa sharti la kutotajwa gazetini, ameliambia gazeti hili, "Yale mambo yalikuja kama taarifa, si vingenevyo. Jukumu sasa, liko kwa Zitto mwenyewe kujipima kama anaweza kuongoza watu ambao hawana imani naye."

Baada ya kupeleka taarifa hiyo CC, wabunge wameeleza, "…Tunapeleka maamuzi yetu haya kwa Zitto. Anatakiwa kuamua ama kuachia ngazi au kusubiri hatua nyingine zinazofaa kuchukuliwa kwa mtu kama yeye katika kikao chetu kingine."

Mara baada ya mjadala wa Zitto kwa CC kutoingilia maamuzi ya Kamati ya wabunge wake, ndipo uamuzi wa kuunda kamati ndogo ya "kumpa ushauri" Zitto ilipoundwa.

Kamati hiyo inaongozwa na Profesa Mwesiga Baregu.Wajumbe wake ni Nyangali Shilungushela, SylivesterMasinde na Mama Zitto.
Kazi ya kamati ya Baregu ni kufuatilia nyendo za Zitto, kumshauri jinsi ya kujibadilisha ili hatimaye arejee katika njia iliyonyooka.

CHANZO: MWANAHALISI
 
Yes, kuna tofauti kubwa sana tena sana. News of the World kupitia kwa Private investigators wao wamekuwa wana-hack simu za familia za wafiwa including wanajeshi waliokufa Iraq, na victims of mabomu ya terrostis (7/7). Na mbaya zaidi kwa victim mmoja wali-hack voice messages zake wa-delete baadhi ili kuwapa -false hopes familia ya wafiwa - all in the name ya kupata 'sensitional news'

Investigative journalism kama ya kuanika wanasiasa wanakula huku na huku kama mwanahalisi walivyo-report issue ya Zitto, au wanaiba mali ya umma, in my view hii iko upande wa public interest, lakini kuuza stories au 'vilio' vya wafiwa ambao kimsingi hawakuchagua kufiwa is wrong.

Hii ndio tofauti ya News of World na Mwanahalisi.
 
Hata mimi naona tofauti kidogo. News of world wanatafuta habari za wafiwa kuleta sensation, wakati MwanaHalisi wanaletewa habari na watu wa serikali (UWT) ili waandike habari za kukimaliza chama fulani au kuwamaliza wanasiasa fulani. Kwa hali yoyote, MwanaHalisi ni shahidi wa ukiukwaji wa taratibu za matumizi ya simu, si mshtakiwa wa kosa hili. Waliopewa dhamana ya kutunza usiri au privacy ni makapuni ya simu, lakini kwa uroho wa madaraka na tamaa ya fedha, makampuni ya simu yanauza siri kwa wanasiasa na wana usalama. Si kosa la MwanaHalisi hili.
 
Back
Top Bottom