Swali la nyongeza, Je mgeni kutoka ulaya au Marekani, akitaka kuja Tanzania atapewa Vissa?
Mgeni lazima atimishe masharti yaliowekwa na serikali kwa mgeni kuruhusiwa kuingia Tanzania.
Mgeni anaweza kuomba viza ubalozi wa Tanzania, Marekani, au akaomba visa uwanja wa ndege, Tanzania, au kwa njia ya posta, Marekani.
Kwa raia wa EU, anaweza kuomba visa katika ubalozi wa Tanzania nchini kwake, au kama hamna, anaweza kuomba kwa njia ya posta, Ubalozi wa Tanzania ulio karibu na nchi yake.
Kwa baadhi ya raia , unaweza kuomba uwanja wa ndege pia unapowasili (visa on arrival).
Masharti ya serikali ni kuwa na pesa za kutosha, uwe na anuani na simu ya sehemu unayokaa, tiketi ya ndege ya kurudi kwenu na pasi iwe ina zaidi ya miezi 6 kabla kuisha.
Unaweza kuomba multiple entry au single entry viza, viza ya kwenda katika mkutano (business visa) au ya kutalii/ kuona ndugu.
Kwa wageni, ukitaka kukaa zaidi ya siku 90, lazima uombe permit ya kuishi Uhamiaji.
Raia wa Marekani ni $100 kwa viza za kitalii za siku 90.
Raia wa Uiingereza ni poundi 40 ($65) kwa viza za kitalii za siku 90.
Ukiridhisha masharti yao, unaweza kupewa permit kutoka Uhamiaji, ya "spouse" kama umeowa/umeolewa na raia wa Tanzania, permit za kufanya shughuli za kidini, permit za kufanya biashara na kadhalika.