Kuna tofauti kati ya VISA na Pasport?

Kuna tofauti kati ya VISA na Pasport?

lup

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
2,514
Reaction score
2,743
Jamani mi naomba kuuliza, hivi kuna tofauti gani kati ya VISA NA PASSPORT? Kwani kuna mtu ameniambia kupata VISA ni ngumu sana kwani nilifikiri PASSPORT NDIO VISA. Pia unaweza kuishi au kutembelea nchi kama za ulaya na Marekani bila VISA.?
 
acha ushamba. vsa unaipata ktk ubaloz wa nchi unayoenda. passport unaipata ktk wzara ya nchi yko na huwez kutembelea nchi bla kua n vsa wala passport vyte muhm
 
Mkuu my name is my name, mkuu lup ameuliza afahamishwe kwa sababu hajui. Na kutokujua kitu si jambo la ajabu.
Ungemjibu tu bila ya kumuita "mshamba" nafikiri ingependeza.
JF ni sehemu ya kubadirishana mawazo na pia kupeana maarifa.
 
Kama raia wa Tanzania ni haki yako kupata passport .
Passport inakuwezesha wewe kusafiri na kukutambulisha umetokea wapi.
Ila Visa unawekewa ndani ya passport, ukitaka kwenda nje ya nchi,unaenda ubalozi wa nchi husika na kuwekewa visa.
Huwezi kwenda Marekani au Ulaya pasipo na Visa na passport .
 
Kuna nchi wanakugongea mhuri na kuonyesha siku utakazokaa hapa ni kwa nchi ambazo kama mtanzania unaruhusiwa kuingia pasipo kuprocess visa ubalozi kwanza au kwa lugha nyingine mtanzania aruhusiwa kuingia bila VISA. Kwa mfano Mtanzania ukiwa na pasipoti yako unaruhusiwa kwenda South Africa lakini ukifika uhamiaji airport watagonga kwenye pasipoti yako kuonyesha kuwa utakaa siku 90. Lakini ukitaka kwenda nchi nyinginezo kama hata zilizopo Africa baadhi ni lazima uende Ubalozi wa nchi hiyo hapa Dar Es Salaam au Nairobi utajaza fomu zinazotakiwa, utaonyesha viambatanisho na kulipia. Wakishakukubalia watakupa VISA ambayo ni document itayobandikwa ndani ya pasipoti yako.
 
acha ushamba. vsa unaipata ktk ubaloz wa nchi unayoenda. passport unaipata ktk wzara ya nchi yko na huwez kutembelea nchi bla kua n vsa wala passport vyte muhm

Umemjibu vizuri sana ila umeanza kwa kumkosea,ni busara wakati mwingine ukampa jibu pasina kuongeza sentensi ya kuudhi kama hiyo ya 'acha ushamba' walimu wangetufunza kwa kututusi wengi tungeyakimbia madarasa!
 
Jamani nashukuru sana.ukweli niliku sielewi.
Ila nauliza tena.gharama ya VISA huwa ni kiasi gani kwa wastani? Na je huwa inausubufu kupata au ni maelezo yako:?
 
Jamani nashukuru sana.ukweli niliku sielewi.
Ila nauliza tena.gharama ya VISA huwa ni kiasi gani kwa wastani? Na je huwa inausubufu kupata au ni maelezo yako:?

Gharama ya visa huwa inatofautiana kwa sababu kila nchi huwa inaweka viwango vyake kutokana na category gani unayoomba. ...mfano kama unataka kuingia nchi husika kama mwanafunzi basi kiwango chake ni tofauti na kama unataka kuingia kama mtalii
 
Jamani nashukuru sana.ukweli niliku sielewi.
Ila nauliza tena.gharama ya VISA huwa ni kiasi gani kwa wastani? Na je huwa inausubufu kupata au ni maelezo yako:?

Usijali hakuna mtu ajuae kila kitu so kila mtu ana ushamba sehem fulani.

Swali lako ni general sana, Visa ziko za aina nyingi (kwenye nchi husika) ama visa inategemea nchi na nchi (variations according to countries).

So sio rahisi sana kukupa jibu sahihi kwa sababu hazina bei uniform, ila kwa ujumla visa za kwenda ndani ya Afrika hazina mashart magumu kama zile za kwenda ulaya/America/Australia. Hizo ni ngumu kupata na bei imechangamka pia
 
Jamani nashukuru sana.ukweli niliku sielewi.
Ila nauliza tena.gharama ya VISA huwa ni kiasi gani kwa wastani? Na je huwa inausubufu kupata au ni maelezo yako:?

Gharama za VISA ,inategemea na Nchi unayotaka kwenda ,,,kila Nchi inatoza kiwango chake,,swali la pili.VISA ni kibali ambacho upewa mtu anayetaka kuingia Nchi Fulani ,hivyo kabla ujapewa hiyo VISA kuna taratibu utatakiwa kuzifuata,,kutokana na taratibu za hiyo Nchi utakayotaka kwenda,sasa usumbufu wake ni wewe mwenyewe kama utaenda kuomba VISA na huna vigezo wanavyohitaji,,hila ukiwa umejikamilisha na vigezo vyao ni kitu Rahisi sana kupata..Ndugu.
 
Jamani mi naomba kuuliza, hivi kuna tofauti gani kati ya VISA NA PASSPORT? Kwani kuna mtu ameniambia kupata VISA ni ngumu sana kwani nilifikiri PASSPORT NDIO VISA. Pia unaweza kuishi au kutembelea nchi kama za ulaya na Marekani bila VISA.?

OK ni hivi Passport ni kijitabu kidogo kinachokutambulisha wewe ni nani na picha yako itakuwepo umezaliwa wap mwaka gani na kadhalika na hiko kijitabu aka passport unaenda wizara ya mambo ya ndani kuomba ya nchini mwako! Sasa Visa ni muhuri utagongwa kwenye passport yako kukuruhusu kuingia nchi nyingine na unaenda kuiomba ubalozi wa nchi uendako mfano ubalozi wa marekani nchini Tanzania! Kila la heri
 
Jamani nashukuru sana.ukweli niliku sielewi.
Ila nauliza tena.gharama ya VISA huwa ni kiasi gani kwa wastani? Na je huwa inausubufu kupata au ni maelezo yako:?

Inategemea nchi gani unaenda na unahitaji visa vya jinsi gani.
Mimi nilitoa $100 ili kupata visa vya Marekani hiyo gharama ilikuwa 6 years ago.
Usumbufu inategemea na nchi unayoenda, kinachotakiwa uwe na sababu ya kwenda huko utakapo na ujue kujieleza vizuri.
 
Una miaka mingapi?

Umesoma shule ipi?

Nnakuomba nijibu hayo nikupe ushauri.
 
acha ushamba. vsa unaipata ktk ubaloz wa nchi unayoenda. passport unaipata ktk wzara ya nchi yko na huwez kutembelea nchi bla kua n vsa wala passport vyte muhm
Unahisi kulikua na umuhimu gani wa wewe kumdharau kiasi hiki!?
 
Una miaka mingapi?

Umesoma shule ipi?

Nnakuomba nijibu hayo nikupe ushauri.

Wewe nawe unaleta mengine? shule ya mtu inahusiana vipi na ushauri wako? haya kasoma Alharamain olevel na kinondoni muslim alevels.
Nyie ndo walewale wanaouliza makabila.
Watu wengine bwana
 
Back
Top Bottom