Kuna tofauti gani kati ya Kuongoza na Kutawala?

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,700
1,721
Wakuu, nimekuwa natafakari kwa muda mrefu dhana hii tunayoaminishwa ya 'utawala bora' na si 'uongozi bora'. Naamini pana tofauti kabisa kati ya KUONGOZA na KUTAWALA.

Ukifuatilia mambo ya siasa wenzetu (nje ya bara letu la Afrika) wanataka kujiongoza wenyewe kwa wenyewe, ila sie Afrika hasa kusini mwa jangwa la Sahara tunataka kujitawala wenyewe kwa wenyewe.

Angalia katika mambo haya ya uchaguzi nchi zote zinazojiongoza matokeo yake ni ya kuridhisha pande zote zinazogombea lakini sie tunaojitawala ni kama vita vya watawala na watawaliwa.

Cha ajabu hata wasomi wetu wanavoitafsiri katiba eti ni mkataba kati wa watawala na watawaliwa! Hii si halali na inajenga dhana ya mwenye cheyo kujiona Mungu mtu.

Tubadilike.
 
Hata mimi naunga mkono hoja. Nchi nyingi za ulimwengu wa tatu zinaongozwa na watawala na sio viongozi.

Kiongozi kwangu mimi ni yule mtu aliyechaguliwa na watu wake kwa ajili ya kuwatumikia na kuwawakilisha kutatua masuala na kero mbalimbali ziwe za kisiasa,kiuchumi na kijamii huku akitambua kwa utashi wake watu hao anaowaongoza wanahitaji nini ili waweze kujikwamua kutoka lindi la umasikini na kuwa na maendeleo ya kweli.

Kwangu mimi kiongozi ni mtu muadilifu,mwaminifu,mcha Mungu, mwenye maono ya mbali, mbunifu, mtu wa kujishusha(humble person) na sio mpenda sifa za kijinga, anayefanya mambo yake kwa vitendo na si maneno, mtu mwenye huruma na hawi mbabe bila sababu ya msingi, daima yupo kwa ajili ya kutekeleza matakwa na masilahi ya watu wake walio mchagua na sio matakwa yake binafsi au kikundi flan cha watu wachache.

Kwa nyakati tulizopo ni aghalabu kuwa na viongozi kwa kuwa tumekuwa tukitawaliwa na watawala badala ya viongozi wa kutuongoza na ndio maana halisi ya mfumo wa kidemokrasia.

Tabia na hulka za watawala mara nyinyi huwa ni za ubinafsi mfano kujilimbikizia mali,kupeana vyeo kwa upendeleo, ubabe na vitisho ili waendelee kubakia madarakani, kutokujiamini, ni wapenda rushwa, madikteta wa kidemokrasia, nk.
 
Wadau

Kuna mjadala unaendelea live sasa hivi Voice of America kujadili hali ya kisiasa Zimbabwe. Mchabguaji mmoja amedai viongozi wengi Africa ni Watawala na sio Viongozi.
Inaonekana ipo tofauti kati ya Utawala na Uongozi.
Wajuzi tusaidiane.
Karibuni
 
Wadau
Kuna mjadala unaendelea live sasa hivi Voice of America kujadili hali ya kisiasa Zimbabwe. Mchabguaji mmoja amedai viongozi wengi Africa ni Watawala na sio Viongozi.
Inaonekana ipo tofauti kati ya Utawala na Uongozi.
Wajuzi tusaidiane.
Karibuni
kuongoza ni kuelekeza mtu ama kikundi cha watu kwenye uelekeo sahihi kama wanavyoamini,kupendezwa na kutaka wao na kutawala ni kuelekeza mtu ama kikundi cha watu kwenye uelekeo sahihi ama usio sahihi,iwe wanaamini ama hawaamini,wanapendezwa ama hawapendezwi na wanataka ama hawataki.
[HASHTAG]#nahisi[/HASHTAG] ni hivyo
 
Mheshimiwa Sana Rais wa Tanzania ameludia neno kutawala zaidi ya mala ishirini kwenye speech yake akiongea na Wana CCM wa Nchi nzima. Mimi nikiwa kijana mwenye elimu ya darasa la nne je Kuna tofauti Kati ya kutawala na kuongoza?
 
Back
Top Bottom