Kuna Timu mafanikio yake ya Kipekee CAFCL yatakuwa ni Kufurahia Mechi yao Kuonyesha 'Live' nchini Sudan

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,542
108,877
Kama mechi yenu tena ya hapa hapa nyumbani Dar es Salaam nchini Tanzania Uwanja wa Mkapa ilionyeshwa mubashara (live) na mkademadema na kupata alama (point) moja mnadhani kwa kuonyeshwa kwao ndiyo mtawafunga?

Wenzenu Wasudan (Waarabu) nje ya mpira pia wana jicho kali la kibiashara hivyo waliona wawajambisheni (wawatishe) kwanza kuwa mechi yenu haitoonyeshwa ili mjae katika shabaha mlalamike kisha Azam Tv nao wakiomba dili la kuionyesha watoe pesa ndefu kama ambayo wameitoa na sasa mechi yenu kuonyeshwa.

Kwa kifupi hawa Wasudan mnaoenda kucheza nao wamefanikiwa sehemu mbili, ya kwanza ni wao kuwa na uhakika wa kuwafunga kwao lakini pia wameshaingiza pesa ya kutosha kutoka kwa Azam Tv.

Na ni nani aliyewadanganya kuwa Waarabu hata mechi yao ikiwa mubashara (live) huwa hawafanyi fujo na figisu figisu zao?

Fujo mtafanyiwa sana tu kudadadeki zenu, tena za kila aina! Kufungwa mtafungwa tu na hakuna mtu wa CAF atakayewatisha.

Na mkumbuke wakati nyie mkimsifia na kumbabaikia tajiri wenu mjanja mjanja (tapeli tapeli), wao tajiri yao ana fedha ambazo mpaka zingine hajui azipeleke wapi!
 
Kama hizi fujo na figisu zingekua na maana tungeona hawa Al hilal wakiwa na makombe kadhaa ya klabu bingwa.

Lakini na figisu zote huwa wanaishia kuburuza mkia kwenye makundi.
 
Na kuna timu mafanikio yake ni kucheza robo tu na makombe wanachukua wengine
Hela zinazopatikana katika hatua za makundi na robo fainali kwenye hii ligi yenu ya mbuzi (ya Aragija) huipati hata kwa dawa.
 
Nasikia mechi ya utopolo haitaonyeshwa live...hahaa! kama naona walichoandaliwa!!
 
Hela zinazopatikana katika hatua za makundi na robo fainali kwenye hii ligi yenu ya mbuzi (ya Aragija) huipati hata kwa dawa.
Katika football tunajivunia makombe na wala sio pesa bwashee.

National Al Ahly washawahi kusema kua wanatumia hela nyingi kuliko wanayoipata kwenye mashindano ya CAF.

Thamani ya timu inakua valued na 'titles'.
 
Kama hizi fujo na figisu zingekua na maana tungeona hawa Al hilal wakiwa na makombe kadhaa ya klabu bingwa.

Lakini na figisu zote huwa wanaishia kuburuza mkia kwenye makundi.
Sasa kumbe yanga mnafeli wapi kuifunga nyingi timu mbovu kama hiyoo??
 
Hakuna cha figisu wala nini tunasonga mbele makundi...kiwango chetu ni juu zaidi yao acheni ushabiki maandazi.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Hata Waathirika wa UKIMWI huwa Wanasisitiziwa mno Kuishi kwa Matumaini wakati Kiuhalisia wanajulikana kuwa muda wowote wanaondoka 'mazima' na kuyaanza Maisha yao mapya Udongoni.
 
Back
Top Bottom