Mentor
JF-Expert Member
- Oct 14, 2008
- 20,328
- 23,879
Nilipokuwa nasoma Kenya kuna kipindi walitoa takwimu kuhusu waume kupigwa na wake zao.
Kama sijasahau, it was an alarming 43% in the lake zone!
Sasa jana kuna jambo lililotokea;
Nikiwa naenda kumchukua dada yangu saluni maeneo ya kijichi-mbagala,
niko nje kwenye ka-restaurant napata soda yangu nikingoja wamalize. Kwa pembeni
amekaa mbaba mmoja na binti wanapiga stori zao.
Mara ghafla akaja mkewe yule baba akaanza kumfokea,
"Unafanya nini na huyu mwanamke hapa?"
mara, "Haya nikukute nyumbani sasa hivi!"
Mume akalalama kiasi, "sasa unataka kuaibishana hadi huku"
Mke wake akamjibu mara ya pili na ya mwisho, "Sitaki maneno, ondoka sasa hivi nikukute nyumbani!"
Yule bwana kwa unyonge kabisa akanyanyuka tena bila hata kuaga akaenda zake...
Nikabaki najiuliza, hivi hata huku Tanzania kuna wabongo wanaonewa na wake zao namna hii? Kupigwa je?
are there any statistics of such things?
Maana kule Kenya, ilibidi na wababa wanaopigwa na wake zao wajitokeze nao kutaka kusaidiwa....huku vipi? ama hali haijawa tete bado? ama ni kuvumiliana ktk harakati za kudumisha amani?