Kuna siri nzito kwenye Deni la Taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna siri nzito kwenye Deni la Taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Apr 15, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Taarifa ya CAG inaonyesha deni la taifa limekua hadi kufikia Sh14.4 trilioni sasa tunajiuliza hivi inaingia akilini kweli? Tunashindwa kujitegemea katika bajeti hapo hapo tunatoa misamaha ya ajabu, hivi hii nchi kweli itakwenda? Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma wiki hii, CAG alisema deni la taifa limeongezeka kutoka sh10.5 trilioni mwaka wa fedha wa 2009/2010 hadi kufikia sh14.4 trilioni mwaka 2010/2011 sawa na ongezeko la asilimia 38.

  “Kuna ongezeko kubwa la deni la taifa lakini hoja hapa si kuongezeka kwa deni la taifa bali ni kwamba deni hili limeletwa kwa mikopo yenye manufaa kwa taifa na yenye kukuza uchumi wa nchi? Hii ndio hoja ya msingi ya kuangalia,” alisema. Mara baada ya kutolewa kwa ripoti hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuu(PAC), John Cheyo alionyesha kushangazwa na kuendelea kukua kwa deni la Taifa wakati miradi mingi nchini haina fedha. “Deni la taifa linatupa matatizo sisi wote hapa kwa sababu mimi sielewi maana tunakopa lakini miradi yetu haina pesa hapa kuna kitendawili,”alisema Cheyo na kusema Bunge itabidi lijadili na kutegua kitendawili hicho.

  Maoni yangu

  Suala la kukua kwa deni la Taifa si geni masikioni mwa watanzania. Deni hili limekuwa likikua hata bila ya mabadiliko yoyote yanayoonekana hadi imefikia hatua masikio yetu yamekuwa sugu kusikiliza wimbo wa kukua kwa deni la Taifa. Kuna uwezekano mkubwa sana usugu huu wa masikio yetu kusikia kichefuchefu hiki, unawapa fursa mafisadi kuingiza madeni hewa kwenye deni la serikali na hivyo kufanya deni kuongezeka, inawezekana tunaingiza figures hewa kwenye hilo deni au fedha tunazokopo zinafika nchini na zinaliwa na wezi wachache na hivyo hazifikii walengwa. Tunaambiwa kwa mwaka wa fedha 2009/10-2011/12 asilimia 38% ya deni hilo imeongezeka.

  Ukiangalia miaka ambayo huduma zimezorota sana hapa nchini kwa viwango vyote ni mwaka 2009-2012 sasa kama kuna pesa mingi hivyo tulikopa zipo wapi Mungu wangu????zimetumika kwenye miradi gani ya kumkomboa mwananchi???Zilikopwa kwa kazi gani???zimetumika kwa shughuli gani???Mbona kila siku ni afadhali ya jana???Hapa tunahitaji microscopic eyes kubaini mauoza mana kama mpaka CAG na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuu wanashangaa, itakuwaje sisi tusiofika huko jikoni????Mimi nadhani CAG/Cheyo wasiishie tu kwenye kushangaa. Wadig down kujua kuna nini, Bora iundwe tume maalum kuchimbua undani wa madeni yetu na ikiwezekana reputable Auditing firms wapewe kazi ya kulichokonoa hilo deni mana nadhani hili deni ni commulative toka enzi ile ambayo BOT ilikuwa chini ya Majizi kama Balali na washirika wake wa Serikalini. Kama waliweza EPA, si ajabu kuwa walianzia kwenye madeni mengine na kuishia EPA. MwanaJF changia nini kifanyike katika hili??
   
 2. i

  ibange JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  JK atatuachia sisi na watoto wetu mzigo mkubwa ana wa madeni. Hizo hela zenyewe ndio wana safiria
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Utouh janga la kitaifa.
   
 4. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  tumefanya sherehe za miaka 50 ya uhuru.

  Tumefanya chaguzi ndogo.

  Tumesamehe kodi.

  Tumesafiri sana nje kwenda kukopa

  Tatizo la umeme.

  Tatizo la mafuta.

  Ufisadi.
   
 5. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Dah inawezekana huyu bwana anakopa ili kuwezesha safari zake. Mana kama kila safari anatumia 300m ukizidisha kwa safari 100 tu kwa mwaka utaona kuwa ana 30 Bil za safari tu achilia mbali wageni anaowaalika Tanzania na kuwakarimu. Dah tumekisha.
   
 6. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kama tulichukua mkopo kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa nchi, haina tofauti na kuchukua mkopo ili ufanyie sherehe ya harusi. Wote huu ni uwendawazimu. Kwani tusingeadhimisha km tulivyoadhimisha, siku zingeganda hadi tuadhimishe ndo ziendelee???
   
 7. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  eti ukusanyaji kodi umevuka lengo?
  Kati ya walipa kodi kumi maarufu utakuta makampuni ya simu hayapo!
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Tunasubiri nini kuingia msituni?
  Jk anakotupeleka siko!
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180

  Ni kweli!
  Hizi safari za Jk za kila mwezi kwenda kumeza vidonge nje zinaiongozea taifa mzigo mkubwa kwenye deni la taifa.
   
 10. n

  nyantella JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Patriote kwenya Guardian ya leo Jumapili, 15th April, page 2, kuna mwandishi mmoja anaitwa Richard Mgamba, kaandika article moja nzuri sana "Lies behind fabricated statistics and hidden agenda" ila ukiisoma kabla hujala unaweza shinda njaa! anyway ina majibu yoote ya maswali yako. find and read it.
   
 11. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Tanzania nchi yenye kuongozwa na mbweha na fisi wenye hila na tamaa wakati huohuo ni wajinga na mbumbumbu wa kutupwa
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,607
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280
  .....Serikali fisadi kila inapoishiwa na kushindwa kulipia matumizi yake ya kila siku basi maamuzi huwa ni kuchapisha pesa zaidi na matokeo yake ni ongezeko kubwa la deni la Serikali kwa Shilingi 3.9 Trillioni. Hawana mpango wowote ule wa kupunguza matumizi makubwa ya Serikali ambayo hayana tija yoyote kwa Watanzania kama vile gharama za kuyahudumia magari ya kifahari katika Wizara mbali mbali, safari za nje za Kikwete na maofisa wengine wa Serikali, misamaha mikubwa ya kodi inayotolewa kwa maofisa mbali mbali wa Serikali wakiwemo Mawaziri na Wabunge na pia kuongeza mapato ya kodi kwa kuhakikisha "wachukuaji" wa rasilimali za Taifa kama vile dhahabu, Tanzanite, Almasi, misitu, gas n.k. wanalipa kodi inayostahili ili kuongeza pato la Taifa. Dr Slaa hakukosea pale aliposema kwenye kampeni za 2010 kwamba, "Kumchagua tena Kikwete ni janga la Taifa."

  ~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Mawaziri, wabunge waongoza kusamehewa kodi
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Sunday, 15 April 2012 10:58
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0diggsdigg

  Na Daniel Mjema,Dodoma

  SIKU chache baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwasilisha ripoti yake bungeni ikionyesha ongezeko la misamaha ya kodi, imebainika kuwa mawaziri na wabunge ni miongoni mwa vigogo wanajinufaisha na Sheria ya Msamaha wa Kodi kinyume cha taratibu.

  Orodho ya majina ya watu waliosamahewa kodi na Serikali katika mwaka wa fedha 2009/2010 iliyopo katika tovuti ya Wizara ya Fedha, inaonyesha majina ya baadhi ya mawaziri, wabunge na wakuu wa taasisi za Serikali wakiwa wamenufaika na misamaha hiyo.

  CAG Ludovick Utouh katika ripoti yake, anasema misamaha ya kodi iliyotolewa kwa taasisi mbalimbali, hadi kufikia Juni 30,2011 ni Sh1.02 Trilioni na kueleza kuwa eneo hilo la misamaha ya kodi linapaswa kutazamwa ili kuepuka kuwa na makusanyo pungufu ya kodi.

  Hatua ya Serikali kuruhusu kutolewa kwa misamaha ya kodi inayofikia asilimia 18 ya makusanyo yote ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imewashtua wananchi, wasomi na wanasiasa ambao sasa wanahoji umakini wa Serikali.

  Katibu Mkuu

  Hata hivyo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhan Kijjah aliliambia Mwananchi Jumapili jana kuwa misamaha ya kodi ipo kisheria na kwamba kila mmoja ana haki ya kuipata.

  "Misamaha ipo kisheria, watu wote wanapata kulingana na sheria iliyopo, hakuna upendeleo," alisema Katibu Mkuu huyo.

  Alisema katika mwaka wa fedha ujao, watapitia upya Sheria ya Misamaha ya Kodi kuona kama ina upungufu ili ifanyiwe marekebisho kwa lengo la kuongeza mapato ya kodi.

  Kijjah alisema kamati ya kuangalia mapato, itapitia upya sheria hiyo kubaini udhaifu wake na itapendekleza nini cha kufanya.

  Kuhusu tuhuma zilizotolewa na CAG katika ripoti yake bungeni, alisema hawajapata ripoti yake na kwamba wanaisubiri ili waipitie na kumpatia majibu.

  Alisema wanatarajia kupata ripoti hiyo wiki ijayo na kuifanyia kazi kwa mwezi mmoja kabla ya kumkabidhi.


  Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG,) inaonyesha kuwa kiwango hicho cha misamaha ya kodi kilichotolewa mwaka 2010/2011 ni cha juu ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

  Alifafanua kuwa taarifa za TRA zilionyesha kuwa misamaha ilitolewa kwa taasisi mbalimbali yenye thamani ya sh1,016,320,300,00 ambazo ni sawa na asilimia 18 ya makusanyo yote nchini.

  Kwa mujibu wa Utouh, kama kiasi hicho kisingesamehewa, TRA ingekusanya Sh6.5 trilioni sawa na Sh717.4 bilioni zaidi ya kiasi kilichokadiriwa kukusanywa ambacho ni Sh6,566,525,544,378.

  "Siku zote tumekuwa tukipiga kelele kuhusu misamaha ya kodi ingawa tunasema misamaha ya kodi haiepukiki lakini lazima isimamiwe na iwe ni lazima kutolewa…kwa kweli eneo la misamaha ya kodi ni la kutazamwa,"alisema.

  Utouh alisema misamaha hiyo ya kodi ya asilimia 18 ni ya juu sana ukilinganisha na viwango vya misamaha ya kodi vinavyotolewa nchi jirani za Kenya, Uganda na Rwanda na kutaka suala hilo litazamwe kwa macho mawili.

  Orodha ya watu walionufaika na misamaha ya kodi kuanzia mwaka 2006 hadi 2008 iliyopo katika tovuti ya Wizara ya Fedha inajumuisha baadhi ya mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa idara za Serikali na baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu.

  Hoja hiyo ya misamaha ya kodi imeibua mijadala mbalimbali nchini huku Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya (Chadema) akihoji sababu ya kutolewa kwa kiwango hicho kikubwa cha msamaha na kutaka waliosamehewa watajwe.

  "Watajitetea kuwa wametoa misamaha ili kuvutia wawekezaji lakini tujiulize hivi kwani hizo nchi za Kenya, Uganda na Rwanda zenyewe hazivutii wawekezaji?... Hizo fedha zingepelekwa kwenye miradi ya barabara tungekuwa wapi? Alihoji.

  Mbunge huyo alimtaka Waziri wa Fedha, Mustapha Mkulo kuwataja watu au taasisi zilizonufaika na misamaha hiyo ili Watanzania watumie orodha hiyo kupima kama watu na taasisi hizo, zilistahili kupata misamaha hiyo ya kodi.

  Mbunge mmoja wa CCM ambaye hakutaka kutajwa jina lake, alidai kinachoonekana ni kuwa Waziri Mkulo hana uzalendo na nchi kwa sababu haiwezekani atoe misamaha ya kodi na hapo hapo deni la taifa liendelee kukua.

  "Taarifa ya CAG inaonyesha deni la taifa limekua hadi kufikia Sh14.4 trilioni sasa tunajiuliza hivi inaingia akilini kweli? Tunashindwa kujitegemea katika bajeti hapo hapo tunatoa misamaha ya ajabu, hivi hii nchi kweli itakwenda?"Alihoji.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma wiki hii, Utouh alisema deni la taifa limeongezeka kutoka sh10.5 trilioni mwaka wa fedha wa 2009/2010 hadi kufikia sh14.4 trilioni mwaka 2010/2011 sawa na ongezeko la asilimia 38.

  "Kuna ongezeko kubwa la deni la taifa lakini hoja hapa si kuongezeka kwa deni la taifa bali ni kwamba deni hili limeletwa kwa mikopo yenye manufaa kwa taifa na yenye kukuza uchumi wa nchi? Hii ndio hoja ya msingi ya kuangalia," alisema.

  Mara baada ya kutolewa kwa ripoti hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuu(PAC), John Cheyo alionyesha kushangazwa na kuendelea kukua kwa deni la Taifa wakati miradi mingi nchini haina fedha.

  "Deni la taifa linatupa matatizo sisi wote hapa kwa sababu mimi sielewi maana tunakopa lakini miradi yetu haina pesa hapa kuna kitendawili,"alisema Cheyo na kusema Bunge itabidi lijadili na kutegua kitendawili hicho.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 13. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #13
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  this is not a light matter.... but as Tanzanians as we are; it will just pass by like many other serious matters, na kutuacha tukishobokea akina Lulu, Kanumba na Diamond
   
 14. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #14
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  yoyote aliyempigia kura jk kwa kupewa kofia au khanga ajue aliuziwa hivyo kwa mkopo kupitia deni la taifa,nyambaf@"?,%
   
 15. N

  Nabwada Senior Member

  #15
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Samahani wanajamvi,mie naomba sie watu wa Mtwara tusiusishwe na hilo deni,kwani hatukushirikishwa wakati wa kukopa wala kutumia hiyo Pesa.
   
 16. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hiyo misamaha unayoongelea inatolewa kwa wabunge. Kama sikosei Tanzania ni nchi yenye serikali kubwa isiyo na ulazima. Licha ya kulipana mishahara mikubwa wanapeana mikopo na misamaha mikubwa.
   
 17. j

  jjjj Senior Member

  #17
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakuu mnakumbuka shuka kumekucha.............ila ufujaji wa kodi ztu ni mkubwa mno,haviniingii akilini
  hata kidogo kwamba kuna Bilion moja wamelipwa wafanyakazi hewa,hivi ni wepi hawa ?hatuwajui kweli? tumewalipaje?
  kwani pesa zao zimeingia katika acount gani?

  Kwani tumeshajiuliza tangu bwana mkubwa aingie madarakani amesafiri nje ya nchi ni marangapi?hadi leo na kila safari iligharimu kiasi gani?

  Kuna sababu gani za kimsingi kutoa misamaha ya kodi,je ni kampuni gani na za nani zilifutiwa madeni na sababu zilizopelekea,
   
 18. a

  adolay JF-Expert Member

  #18
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280
  Historia hudiandika.

  Naamini kabisa kwa dhati ya moyo wangu kila Rais alietesa na kufisadi watu wake mwisho wake mbaya sana.

  Mfano:-

  Idd Amini - Uganda
  Mabutu - Zaire (DRC)
  Ghadaf - Libya
  Hussen Mubarak -Misri
  Habijerima -Rwanda

  Orodha ni defu. Na hapa kwetu wasijisahau kwamba Mkapa na kikwete Kazi wanayo tena kubwa.
  Yanaweza kuwa maneno matupu walioyazoea lakini watatahayari kwamba hata Ghadaf hakuamini nini kilitokea pamoja na nguvu jeuri ya fedha, Jeshi nk.
   
 19. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #19
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,950
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  Washajua 2015 nchi si yao. Wanavuna
   
 20. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #20
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,950
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  au maandalizi ya kuhonga 2015?
   
Loading...