Kuna siri gani kwenye Kanisa Katoliki kuhusu Miracle Hunter?

Huu uzi hauwafai wafia dini mkuu
ndio maana nimetoa angalizo ujue iko hivi kuwa mlutheri au mkatolic au nani haina maana kuwa kanisa ni takatifu
hapana kuna mambo yatakuwepo mengi tu ambayo hata waumini hamuwezi kuyajua ndio maana kanisa mfumo wake wa serikali yake haupo katika biblia ni watu hukaa chini na kuweka mikakati yao binafsi
so kanisa takatifu ni nafsi yako na Mungu wako wala sio lile dhehebu tunaenda kulisalia wala sio hilo jengo Kama wewe ni Mkatoliki wewe ndioo unapaswa Kuwa Mtasi kiimani na matendo ila lile jengo na katiba zinabakia kwa matakwa ya wanadamu tu
angalia maandishi mekundu katika uzi huu ni angalizo msije kupata madhara
Mimi sio mfia dini na sina tatizo na mada yako. Nimejaribu kutoa mawazo yangu kulingana na upeo wangu, mengine utayapata kwa wadau wengine.
 
Umenifungua hapa. Nikiwa O-level nilikuwa na ukaribu na binti mmoja. Ni wa wilaya jirani na ulipopazungumzia. Wanayemfahamu wakanitahadharisha kuwa niwe makini naye kwani yeye na babaake ni watu hatari. Ni wachawi kupindukia.

Nilipododosa walijua vipi kuwa wao ni wachawi nikaambiwa padri aliwaumbua. Eti katika shughuli zao za kuroga akawapiga picha. Picha zingine aliwapiga wakiwa wapo kwenye usafiri wao wa ungo. Picha zikasambazwa kijiji kizima.
Nilipouliza padre alifanikisha vipi hili kama yeye si miongoni mwao, nikaambiwa tu yuko vizuri. Akapewa sifa kuwa ana uwezo wa kuyajua hayo.
Labda nae mi Miracle Hunter...
 
Sio kitu kipo rasmi kwamba kila mmoja anakijua na kinawekwa hadhari only few selective ndio wanajua haya nadhani ndio maana nimejaribu sana kutafuta habari hiii mitandaoni nimeikosa
Ni exorcism mkuu,ni aina ya operation ya kiroho inayofanywa na mapadri maalum kwa ajili ya kuondoa roho chafu au pepo kutoka kwa mtu.na zoezi hili kina hatua zake kulingana na kiwango cha possession.provoking demons ikiwa ni awali
 
Umenifungua hapa. Nikiwa O-level nilikuwa na ukaribu na binti mmoja. Ni wa wilaya jirani na ulipopazungumzia. Wanayemfahamu wakanitahadharisha kuwa niwe makini naye kwani yeye na babaake ni watu hatari. Ni wachawi kupindukia.

Nilipododosa walijua vipi kuwa wao ni wachawi nikaambiwa padri aliwaumbua. Eti katika shughuli zao za kuroga akawapiga picha. Picha zingine aliwapiga wakiwa wapo kwenye usafiri wao wa ungo. Picha zikasambazwa kijiji kizima.
Nilipouliza padre alifanikisha vipi hili kama yeye si miongoni mwao, nikaambiwa tu yuko vizuri. Akapewa sifa kuwa ana uwezo wa kuyajua hayo.
Labda nae mi Miracle Hunter...
Heri yako bwana ujue kuna vitu vipo katika maswala yetu ya dini lakini hakuna mtu ambaye anaweza kuvijua asipokuwa ni mshirika wa mambo husika
sijui embu tuone wanaojua kama watakuwa tayari kutoa elimu hiii
 
Huyu kajichanganya huyu..! Kwa mbali wakarismatic wanafanya maombi ya namna hii.
Inamaana wakaristimatic hawatumii jina la Yesu katika maombi?
sijajichangana mkuu sema labda mada imekuwa jiwe kwako hauwezi kuielewa
 
Katika amri ya ya nane ya Mwenyezi Mungu imekataza kusema uongo na kumshuhudia mwenzako uongo, angalia ukichokiandika madhara yake kwako kiroho, fikiria mara mbili umepotosha watu wangapi humu jamvini. Mashaka yangu utakuwa wewe ni atheist

kabla sijaileta hoja ya leo naomba kwanza wale ambao hawana interest na mambo ya dini ama hawapendi kujifunza mambo ya ziada huu uzi hauwafai wala hawatakiwi kuwepo hapa, wale wasioamini kuhusu Mungu huu uzi hauwafai
wale wanaona dini zao zimekamilika wala hawataki ziguswe basi pia huu uzi hauwafai.
Huu uzi hauwafai wote wenye personal interest na dini.Sasa naenda katika point yangu
 
usilete personal interest hapa mkuuu
 
Habari ya jumapili wana JF
kabla sijaileta hoja ya leo naomba kwanza wale ambao hawana interest na mambo ya dini ama hawapendi kujifunza mambo ya ziada huu uzi hauwafai wala hawatakiwi kuwepo hapa, wale wasioamini kuhusu Mungu huu uzi hauwafai
wale wanaona dini zao zimekamilika wala hawataki ziguswe basi pia huu uzi hauwafai.
Huu uzi hauwafai wote wenye personal interest na dini.Sasa naenda katika point yangu

Kunawatu wanaitwa "MIracle Hunter" hiki cheo anaweza kuwa nacho mtu yeyote mwenye elimu hiyo lakini nimeona sana kwa wale mapadre wanakuwa nayo hii kitu na sio kila padre ila ni few selective
Hawa majamaa kazi zao kubwa wanazokuwa wanadai wanazifanya inakuwa nikufuatilia mambo ambayo yametokea sio ya kikawaida kawaida katika maeneo yao.
NImewahi kushuhudia shuguli moja kule peramiho kwakweli ni mambo fulani kama uganga kabisaa lakini unakuta wanatumia vitu ambavyo ni vitakatifu(kwa madai yao)mfano msalaba, maji ya baraka na baadhi ya sala(spell)

Kilichonifanya kuwa interested kuwajua hawa watu nikuwa kwa mara ya kwanza nilibumiana nao peramiho tena wakiwa wapo wanawajibika(katika pitapita ndio tukajikuta tuko eneo la tukio) walikuwa ni mapadre watatu na walikuwa na wazee wawili na mwana mama mmoja ambaye alikuwa anashida na wanamfanyia ibada fulani alikuwa kafunikwa na shuka fulani rangi ya kaki lina michoro ila sikuelewa ile michoro vizuri maana tulikuwa umbali kidogo na nilijua ni mwanamke sababu ya sauti yake(mimi nilijua anamapepo wanamuombea)lakini utendaji ulikuwa ni tofauti
Kwanza zile sala zao walitumia kilatin na kiingereza(na miongoni mwao padri mmoja alikuwa ni mtu mweusi kabisa) chakushangaza zaidi nikuwa sikusikia neno Jesus katika sala zao za kiingereza , ila ilikuwa ni baadhi tu ya majina ya malaika na commanding language zao binafsi kama "In the name of the Lord...."hayo maneno nayakumbuka vizuri sana nk lakini hawataji jina la Yesu
baadaye tukiwa tunashangaa pale kuna mtu akaja nyuma yetu tuliposimama
kugeuka alikuwa ni padre mwingine akatuambia tuondoke maana tunaweza kudhurika, nilipoondoka ndio katika pelelezapeleleza nikajua wanaitwa "Miracle Hunter" aliyenipa hii habari ni katekista mmoja hivi toka mkoani kwetu naye anawajua kwa ufupi sana japo anasema haelewi ni wapi kuna mafunzo hayo maana si kila mtu anapata

Aliongeza niwatu ambao wanaweza hata kumuita mzimu wa mtu na wakaongea nao wanafanya mambo yaa ajabu na kutisha mno.
ila sasa shida yangu ilibakia katika lugha wanazotumia na kutokutumia JIna la YESU kama vile wakristo tunavyojua
sasa naomba mwenye kuwajua vyema hawa watu naomba atusaidie habari zao zaidi nimetafuta sana google ila sijapata kitu kwakweli kama ni elimu ziko prohibited naomba unayejua unaweaz hata ukani pm
Kwa taarifa yako ndani ya dini hizi kuna mambo meengi ya ajabu sana ikiwemo ,ugaidi,uchawi,uharamia nk. Na yote hayo yanaongozwa na viongozi wa dini kwa siri kubwa sana.kwa hiyo ndg.ww hutakiwi kujua saana mambo hayo kwani yatakutoa ktk imani yako ya kidini. Nenda kanisani au msikitini ukasali halafu kafanye yako.tofauti na hapo utajikuta unayajua mengine yatakayokutoa ktk imani unayoishikilia.
 
May be ingawa siamini pia, itakuwa ni kitu kingine.
Kuna mtu hapo juu kaongelea habari za exorcism ukijaribu kugoogle hiyo kitu utashangaa sana,
Ujue mambo mengi yapo katika dini zetu ila huwa hatuyajui, kwanini hatuyajui?
Kwasababu mara nyingi inakuwa tunahubiriwa tu na viongozi wa dini yale ambayo wao wameamua kutufundisha, lakini ukiamua wewe mwenyewe kama wewe ujifunze zaidi utafunguliwa mambo mengi sana ambayo huenda hukutegemea kama ungeweza kuyaona ama kuwa dini yako inajihusisha nayo.
Muhimu nikulinda moyo wako usije ukapotea maovuni, ukiona elimu za ziada zinawezakukupoteza ni heri ukaachana nazo, ila uhalalisia wa dini hizi ni tofauti kabisa na vile ambavyo sisis tunajua kwa nje nje tu
Mengine makubwa yanafanyika ambayo tungeyajua huenda tungehama ama kuacha kusali kabisa
 
Kwa taarifa yako ndani ya dini hizi kuna mambo meengi ya ajabu sana ikiwemo ,ugaidi,uchawi,uharamia nk. Na yote hayo yanaongozwa na viongozi wa dini kwa siri kubwa sana.kwa hiyo ndg.ww hutakiwi kujua saana mambo hayo kwani yatakutoa ktk imani yako ya kidini. Nenda kanisani au msikitini ukasali halafu kafanye yako.tofauti na hapo utajikuta unayajua mengine yatakayokutoa ktk imani unayoishikilia.
Umenenena vyema mkuu
sema napenda niyajue mengi maana mimi mwenyewe huwa nafundisha Neno la Mungu kwahiyo naona ni sehemu yangu ya kujifunza yanayonifaa nayachukua yasiyo nifaa naachana nayo
Asanthe kwa ushauri wako pia
 
Kuna jambo pia nimeambiwa hapo juu kuhusu exorcism jaribu ku-google sasa exorcism in catholic pitia mada mbalimbali yaani utastaajabu ya filauni kwakweli
Samahani mtoa mada naona kama umezunguka sana
Tuambie madhumuni ya mada yako tu maana wengine vyuma vimekaza hadi kufikiria tunashindwa
 
Samahani mtoa mada naona kama umezunguka sana
Tuambie madhumuni ya mada yako tu maana wengine vyuma vimekaza hadi kufikiria tunashindwa
Ha ha ha ha soma hadi mwisho utapata nini dhumuni mkuuu
 
Back
Top Bottom