Kuna siri gani kwenye chumvi?

Chumvi ya mawe inauwezo wa hali ya juu Sana ingawa watu wanaipuuzia

Me mwenyewe alimanusura inidhuru baada ya kuitumia kuzungushia kwenye eneo la kitanda changu ila sitasahau ilinifanya nisakamwe na wachawi
 
mashanajr nakuomba hapa kunaswala linahitaji ufafanuzi maana hata waganga wakienyeji,wachungaji wanaoponya wanatumia sana chumvi sijaelewa ila katika bible kunamaali Ruth alikatazwa asigeuke alipogeuka akawa jiwe la chumvi iko sababu hapa.
Aligeuzwa jiwe la chumvi ile awe faida kwa matumizi ya wengine.. Japo Bible haijafafanua ni chumvi ya aina gani
 
Mods naomba mtauweka uzi huu kwenye jukwaa sahihi kama nimekosea.

2 Wafalme 2:19-22

Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza. ndani yake.

Wakamletea. Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, BWANA asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza.

Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena.

Leo katika pitapita zangu nikakutana na video moja tiktok kuna mdada anaongea habari za chumvi, story za kuogea chumvi na kadhalika. Na kuna watu wanashuhudia kabisa zimework out kwao.

Pia nikakumbuka zile story za kama mtu mtu ana mikosi wanamshauri akaoge maji ya baharini atoe mikosi. Huenda kuna ukweli. Mimi sijajua.

Nikalazimika kutafuta kwenye biblia story za chumvi na ndio nikakutana na hiyo ya 2 Wafalme 2:19-22. Sijajua kwenye vitabu vya dini zingine kama imezungumzwa wenzetu mtatusaidia.

Kwenye bible inaonesha kumbe chumvi ilikuwa inatumika toka miaka hiyo kuponya vitu as kama ilivyo kwenye hiyo story ya wafalme.

Kuna siri gani kwenye chumvi?

Kama una nondo za kuongezea unaweza kutiririka.

Jumapili njema.
Chumvi YA Wapi mdau, uwe inatoa ufafanuzi.
 
chumvi ni madini meupe yanayotumiwa kwa kutiwa ndani ya chakula ili kukipa radha .kazi ya chumvi katika mwili kuimarisha mifupa na zipo nyingi.sasa katika ulimwengu wa roho.kuna siri kubwa ukisoma kwenye biblia umeona na kifungu umetaja waf2;20 utaona chumvi inavyo fanya kazi.hili jambo linaendana na imani.ukisoma wabre11;1.inasema hivi iman ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiayo ni bayana ya mambo yasioonekana.neno zito hapo ni yasio onekana.yaani kuna mambo yanaonekana lakini yapo mengi yasionekana na yanakisi katika ulimwengu wa mwili.narudi kwenye chumvi.ukiambatanisha na imani chumvi katika ulimwengu wa roho inaharibu,inaozesha,inavunja,inateketeza,.Lakini inaweza kuwa kinyume yake kulinga na uitaji na maombi unayo yaomba.
Sio lazima chumvi iwe nyeupe mzee
 
mashanajr nakuomba hapa kunaswala linahitaji ufafanuzi maana hata waganga wakienyeji,wachungaji wanaoponya wanatumia sana chumvi sijaelewa ila katika bible kunamaali Ruth alikatazwa asigeuke alipogeuka akawa jiwe la chumvi iko sababu hapa.
Hivi mke wa Lutu alipogeuka nguzo ya chumvi ni nani aliyegeuka nyuma kuthibitisha kuwa aligeuka nguzo ya chumvi
Ingawa kibibilia kugeuka nyuma inaweza kuwa na maana pana zaidi ya kugeuka kutazama nyuma. Inaweza kuwa ni kutenda yale yale ya zamani au ya nyuma ambayo yalikuwa haya mpendezi MUNGU
 
Ingawa kibibilia kugeuka nyuma inaweza kuwa na maana pana zaidi ya kugeuka kutazama nyuma. Inaweza kuwa ni kutenda yale yale ya zamani au ya nyuma ambayo yalikuwa haya mpendezi MUNGU
Asante hili sasa ndio jibu
 
ahh basi wewe unachanganya na magadi.tunazungumzia chumvi mzee nenda uendako chumvi ni nyeupe na ueupe huo una nguvu katika ulimwengu wa roho
Hata magadi ni mazuri kuliko hata hyo chumvi, hutibu mambo mengi, ikiwemo tumbo, pia huondoa uchawi wa zongo, so ukichaganya magadi na hyo chumvi ya mabonge Matokeo yake ni makubwa zaidi, pia ukimwagia kwenye biashara inaondoa machawo yote mabaya na aliyeroga eneo lako atajua hajui huko aliko.
 
Naskia hata Kama una mdeni wako fasta tu anakulipa Ela yako unayomdai.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom