Dunia inaendeshwa na vitu viwili pesa na mapenzi, kimoja ni cha kiroho na kingine ni cha kimwili... Pesa inang'arisha na kutakatisha mwili hivyo kamwe haifichikiUmeshawahi kujiuliza hili?
Ukiwa huna pesa umepigika hakuna hata mtu anayekusogelea, hata walio mbali hawakupigii. Hata ndugu zako wanakuwa kimya, japo kwa kuwa uko mbali nao hujawaambia kama uko kwenye wakati mgumu. Kama una mchepuko wako wala hata hana muda na wewe.
ILA SASA
Siku umepiga dili flani ukapiga mkwanja wa uhakika.... mfano kuna malipo umeyapata kama milioni kadhaa au laki kadhaa. bosi wako amekuambia broo cheque yako tumepeleka bank, hapo unakuwa na uhakika leo niko fresh. Unapanga bajet zako kadha wa kadha, kabla hujaenda kuchukua hiyo hela, au ndani ya siku moja tangu upate hela, zinakuja sms kibao, unapigiwa simu toka pande zote... wanakutajia matatizo, mengine yanatia huruma. Mchepuko wa muda mrefu mlishasahauliana siku hiyo anaanza tuu kuchat na wewe tena yuko mkoa mwingine....
Hivi wanajuaje kuwa leo una hela ndo waanze kukuomba wakati hujawaambia?
Mshana Jr, nakukaribisha
Heshima kwaji Mkuu.Dunia inaendeshwa na vitu viwili pesa na mapenzi, kimoja ni cha kiroho na kingine ni cha kimwili... Pesa inang'arisha na kutakatisha mwili hivyo kamwe haifichiki
Jr
Sio matatizo tu hata vitu vizuri vya kitonga ushafikiria?
Hii imenitokea, Jamaa alitaka niuzia simu s9 plus kwa bei ya 500k na Sikuwa na kitu,nilihangaika kuitafuta ikashindikana.Sio matatizo tu hata vitu vizuri vya kitonga ushafikiria?
Anatokea mtu kapigika mbaya anatafta hela ya kuongezea mwanae apate ada anakuja na iphone X ng'ada kabisa anataka laki 3 tu akuachie simu hapo unajua fika ile simu ni 2.3m na resale value iko juu ila huna hata mia mfukoni.
Mwengine anaweza akaja na Laptop ya maana ukiangalia thamani si chini ya laki 7 anakwambia nsaidie jamaa nataka kufukuzwa na landlord nahitaji laki mbili tu nikamilishe kodi ya nyumba. Halafu uwezo unao ila mda anaokuja huna hata sh.100 mbovu.
Hapo ndipo unapoona ukata hauna maana, ila siku ukiwa na milioni hivyo vi deal hauvioni kabisa.Hii imenitokea, Jamaa alitaka niuzia simu s9 plus kwa bei ya 500k na Sikuwa na kitu,nilihangaika kuitafuta ikashindikana.
Sent using Jamii Forums mobile app