Kuna redio yoyote ya Tanzania ambayo inacheza burudani tu bila habari wala blaa blaa nyingine

uwe hodari

JF-Expert Member
Dec 16, 2022
3,982
8,336
Redio ambayo haina haya mambo ya habari za Tanzania labda iwe nje tu kwa kifupi wala haina vipindi vya kuongea ongea

Nimejaribu kutafuta Fm redio naona zote asilimia kubwa wanatangaza ujinga tu

Redio za Tanzania zote zitaanza ratiba

Kwa kusoma magazeti na blah blah kibao..

Watakuja wengine kuendesha umbeya na kupiga taarabu

Wataingia mchana wapige nyimbo za bongoluleva

Watakuja michezo

Hakuna kipya ni wanarudia ujinga ujinga tu

Kuna redio moja kipindi cha nyuma jina limenitoka
Kuanzia saa kumi jioni hadi saa mbili ilicheza nyimbo ya kongo oldskul

Usiku kuanzia saa mbili inacheza worship song hadi saa saba usiki

Kuanzia saa saba hadi saa moja kamili inacheza nyimbo za taratibu km rnb, country and soul,

Ghafla ilipotea hewani

Je, kuna ingine mwenye kujua ina maudhui ya mziki tu? Tena mziki mzuri
 
mi naskilizaga Choice Fm 102.5 naonaga wana miziki tu
Hata hii pia itaanza tu kuwa na watangazaji,, kwani wasafi fm inavoanza mbona ilikua mziki mwanzo mwisho but now 😦😦

Mm pia sipendi kuskiliza radio kwa sababu ya watangazaji hawana content yyte ya ku deliver japo naona Radio one, Clouds fm ma efm kwa mbaaaliiiiiiii vipindi vyake (sio vyote) huwaga vina content sana. .

Mfano radio one kwny kipindi cha asubuhi cha kumepambazuka unaweza kuta wamemwalika afisa wa Traffic, au afisa wa TRA akawa anatoa elimu ambayo sometime hukuwa nayo.

Pia kipindi cha malumbano ya hoja alhamisi usiku unakuta sometime wanajadili mambo ya maana mfano, namna ya kumaliza mgao wa umeme.

Pia clouds fm kuna kile kipindi cha PB,,,,napenda kukisikiliza sababu ya content za masoud kipanya KP.
 
Hii aliyoitaja mdau Choice FM ni wakongwe wana more than 13 yrz kwenye industry mwanzo wakati inaanza ilikuwa inapiga ngoma tu hilo la kuweka watangazaji walishajaribu wakaachana nalo naona sasa wameondoa utaratibu huo.

Tulioishi zamani kwenye burudani miaka ya nyuma 1998/2000s-2012 kulikuwa na FM radio ikiitwa Kiss FM pacha na RFA hii haitakaa itokee tena yaani kipindi hicho mtu kulala ulikuwa unalala kwa sababu ni utaratibu wa binadamu ila ungetamani usipitwe na chochote kutoka kwenye hiyo radio station.
 
Hii aliyoitaja mdau Choice FM ni wakongwe wana more than 13 yrz kwenye industry mwanzo wakati inaanza ilikuwa inapiga ngoma tu hilo la kuweka watangazaji walishajaribu wakaachana nalo naona sasa wameondoa utaratibu huo.

Tulioishi zamani kwenye burudani miaka ya nyuma 1998/2000s kulikuwa na FM radio ikiitwa Kiss FM pacha na RFA hii haitakaa itokee tena.
Nakumbuka kiss fm mara ya kwanza naipata nikiwa moro miaka ya 2000 hapo, nimeweka ka waya nje kama antenna na search station nikakutana na hiko kituo asee ni ngoma bandika bandua mwanzo mwisho
 
Kwa kweli Radio zote siku hizi ni UJINGA, hakuna vipindi ila ni story binafsi tu mara jana tumeinjoi Sana, umependeza, Leo Bata tukale wapi yaani ujinga and still the government keep quiet so sad utasikia TUTUNZE MAADILI shame on you
Hamna kitu kinaniboa redioni kama hicho, yaani kipindi kinageuka kua genge la story tu.
Sijui jana nimekula nini na wapi, story za kijingajinga tu
 
sikukatalii hata

Choice FM
ilifika kipindi nilisikiliza hii (miaka ya 2013 ) enzi za akina Tandy , mpaka playback zake nikawa nimezikariri, asubuhi mpaka jioni, ikitoka ngoma hii najua inafata hii
wakatoka wakaja kina Seba, wakatoka, wakafanya ikawa stesheni ya Kiswahili ( mwishoni mwa 2019 hivi ) nikaacha sikiliza mazima

kwa sasa ni TBC Int'l, ndiyo stesheni yangu
 
Kama uko dar es salaam weka 90.9 fm.
Hata sasa hivi weka.
Kama ukisikia taarifa ya habari au wanataja masaa, njoo uwaambie mods wanipige ban.
Ngoja nikupe somo kidogo.

Redio unazosikiliza karibia 70% zote zinatambulika kama redio za burudani na hata wakiweka hapa vyeti vya usajili ni iko hivyo.

Redia za habari ni chache sana hapa nchini na zinafahamika.

Hiyo redio sijui 90.9 bado mpya kwa lugha ya kitaalam ni tunasema wapo kwenye probation time, ambayo inaweza kufika hadi 3months fully muziki.

Haya maredio ya siku hizi yanasajiliwa kwa burudani alafu wanajiingiza kwenye kutangaza habari na matukio wakati katika asilimia 100% habari ni kiduchu mno!.

NB; Msioelewa msizikashifu hizi fm hicho wanachofanya ndicho hasa burudani yenyewe as (porojo) muda mwingi, wanahakisi usajiri wao.

Ni sawa unaposajili gazeti why kuna kakipande wanaweka kaji_cartoon!!.
 
Kwa kweli Radio zote siku hizi ni UJINGA, hakuna vipindi ila ni story binafsi tu mara jana tumeinjoi Sana, umependeza, Leo Bata tukale wapi yaani ujinga and still the government keep quiet so sad utasikia TUTUNZE MAADILI shame on you
Kweli hasa vipindi vya mchana, hakuna hata mada maalum, ni kupiga stori kama wapo kijiweni vile
 
Hii aliyoitaja mdau Choice FM ni wakongwe wana more than 13 yrz kwenye industry mwanzo wakati inaanza ilikuwa inapiga ngoma tu hilo la kuweka watangazaji walishajaribu wakaachana nalo naona sasa wameondoa utaratibu huo.

Tulioishi zamani kwenye burudani miaka ya nyuma 1998/2000s-2012 kulikuwa na FM radio ikiitwa Kiss FM pacha na RFA hii haitakaa itokee tena
Ok sawa sawa.
 
Back
Top Bottom