Kuna raha ya kupewa jina zuri na wazazi?

Kwani

JF-Expert Member
Jan 12, 2016
455
562
Za ukosefu wa sukari wakuu!!

Binafsi napenda jina langu na najivunia kuwa nalo,vipi wengine kuna raha yoyote ya kujivunia jina?
Kama ipo kwanini watoto wanaendelea kupewa majina ya hovyo hovyo?

S.1998
 
mambo ya kumwita mtoto tabu,shida,masumbuko,hapendeki,sikitu kisa situation ya maisha iliyopo au kisa vijembe kwa majirani ni ujinga,mpe mtoto jina badae awe proud.kuna ndugu yangu(namwita mama mdogo) anaitwa "Hasara" lakini saiv kalifupisha anaitwa "Sara"
 
majina ya pwani bhana,imagine nna wajomba wawili mmoja anaitwa "Sina sudi" anajiita Sudi mwingine anaitwa "Fikirini" anajiita Fikiri achilia mbali mama mdogo anaitwa Semeni.niliuliza maana ya sina sudi wakasema maana yake ni "sina bahati" Fikirini ni ujumbe kwa jamaa na marafiki kwamba wafikiri;ujumbe unapelekwa kwa walengwa kupitia jina mtoto.nikijaaliwa kupata mtoto nitamwita jina zuri.
 
Ukiwa nalo zuri ndo nini kwa mfano.
 
Ukiwa nalo zuri ndo nini kwa mfano.
imagine wewe ungekuwa unaitwa "Matatizo" mkuu ungefurahia jina hlo? bora uitwe Furaha, Faraja,Zawadi nk(kwa majina ya kiswahili) au majina ya kidini kama joseph, hassan nk.kwa mtazamo wangu hayo ya mfano machache ni mazuri.
 
majina ya pwani bhana,imagine nna wajomba wawili mmoja anaitwa "Sina sudi" anajiita Sudi mwingine anaitwa "Fikirini" anajiita Fikiri achilia mbali mama mdogo anaitwa Semeni.niliuliza maana ya sina sudi wakasema maana yake ni "sina bahati" Fikirini ni ujumbe kwa jamaa na marafiki kwamba wafikiri;ujumbe unapelekwa kwa walengwa kupitia jina mtoto.nikijaaliwa kupata mtoto nitamwita jina zuri.
Mi natafuta maana ya jina "Chausiku", hicho cha usiku ni kinini?? Then ni jina maarufu sana huko pwani pwani.

Lakini hata ya kizungu nayo ni shidaa kuna jamaa yangu anaitwa "Dickson" sijajua kama lina maana nyingine lakini jamaa ukimuita kifupi dick anakuchapa kofi. Anatumia zaidi la ukooo
 
Majina mazuri unayapata mbeya au kigoma na bukoba mf.Lugano ua Asajile na akina Amanyisye ukienda Kgm mf.Nzoyimana au Ndikumana nk
 
Mi natafuta maana ya jina "Chausiku", hicho cha usiku ni kinini?? Then ni jina maarufu sana huko pwani pwani.

Lakini hata ya kizungu nayo ni shidaa kuna jamaa yangu anaitwa "Dickson" sijajua kama lina maana nyingine lakini jamaa ukimuita kifupi dick anakuchapa kofi. Anatumia zaidi la ukooo
daa hata me sijui,au mtoto akizaliwa usiku bhas wanamwita chausiku haha!
 
Jina zuri lina raha yake , kwa mfano jina langu watu wengi hawaamini hadi inabidi niwaonyeshe ids zangu. My name is so dope hadi mwanangu nimempa jina langu, mane and the funny part ni la kiswahili lakini it can be translated globally in each and every language.
 
If you don't like something change it; if you can't change it, change the way you think about it.
 
Back
Top Bottom