Sungusunguu
JF-Expert Member
- Aug 4, 2018
- 1,280
- 998
Suspect wa kwanza akifa mwenza ni mwenzake. Unless labda haukuwepo na una ushahidi wa hilo. Ukitazama Crime and investigation utagundua upelelezi uwa unaanzia ndani kwenda nje. Yani suspect uwa wanaanza kwua watu wa karibu, mfano anaoishi nao mtu labda mume, au mke, ndugu, kama ana watoto wazima, then ndiyo wanaenda nje iwe amejinyonga au kauawa.Habarini!
Kuna rafiki yetu mmoja mke wake kajinyonga wakiwa pamoja ndani na mpaka sasa mwanaume kakamatwa na yuko polisi
Je ni sahihi kijana huyo kushikiliwa na je sheria inasemaje mtu akifa ndani ya nyumba na mkiwa pamoja kwani kwa maelezo ya uyo jamaa anadai yeye aliwahi kulala na mwanamke alibaki sebuleni ambako akakuta kajinyonga na anadai aliwahi kumtoa kamba shingoni nakumfungua kisha baadae ndo akaanza kutoa taarifa kwa majirani
Kujiua kama ilivyo kosa kisheria pia kwa Mungu ni dhambi. Hivyo ni wazi kwa upande wa kiroho huwezi kumwita shujaa mtu aliyejiua bila kutilia maanani sababu iliyomfanya ajitoe uhai; na wala huwezi kusema yupo mbinguni labda kama alijirudi na kutubia dhambi ya kujiua kabla hajakata roho.Ikiwa aliyejinyonga katokea kule kwa shujaa Mkavi Nyika, jua kwamba kaongezea idadi ya mashujaa mbinguni. Hata hivyo, duniani pagumu sana, ukiona mtu kajiua/kauwawa, basi tuhuzunike kidogo tu, na kazi iendelee. Maana tuliobaki, hatujui tutakufaje!
Unajua kiwewe cha kumkuta mwezi wako amejinyonga wewe? Fikiria unaingia chumbani unarudi unamkuta ananging'inia! Yaani usiache kujaribu kumuokoa useme unasubiri polisi? Kwanza nikuambie: kitendo cha kumuacha eti unasubiri polisi wakati muda mfupi mlikuwa wote kitaleta mashaka zaidi kuwa wewe ndiye uliyemuua.Alipaswa amuache hapohapo ananing'inia hadi polisi waje wamtoe
Hili la kusema asingejaribu kumtoa kwenye kitanzi nakataa. Yaani uko na mke wako sebuleni, na ni mzima, ukaingia chumbani, haijalishi umekaa muda gani, kurudi ukakuta ananing'inia kwenye kitanzi uache kujaribu kumuukoa eti unasubiri polisi? Haki ya nani itakuchukuwa muda sana ku-convince polisi kuwa siyo wewe umemuua. Kawaida kwenye mazingira kama hayo jambo la kwanza hutaamini kama ameshakwisha kufa na utakimbilia kumtoa.Kuna masuala mengi ya kujibu
1 Alikuwa wapi mpaka mwenziwe ajinyonge?
2 Hakusikia kishindo chochote?
3 Kwanini amfunguwe kamba badala ya kuita polisi nao ndio wakafungua kamba?
4 Mwilini mwake ana mikwaruzo yoyote ile?
5 Kuna ujumbe wowote wa marehemu wa kujinyonga.
Simu ya marehemu inahitajika kuangaliwa kwa umakini kama kuna ujumbe wa usaliti kwa mwenza wake mpaka kupelekea mauti kumfika.
Jeshi la polisi lifanye kazi yake kwa haki pande zote isitumuke hisia bali ushahidi kamili wa kujiridhisha.
Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
Je alikutwa ana majonzi au analia kwa hisia kali!!? Kama alikutwa mkavu atasumbuka sanaJe, ni sahihi kijana huyo kushikiliwa na je sheria inasemaje mtu akifa ndani ya nyumba na mkiwa pamoja kwani kwa maelezo ya uyo jamaa anadai yeye aliwahi kulala na mwanamke alibaki sebuleni ambako akakuta kajinyonga na anadai aliwahi kumtoa kamba shingoni na kumfungua kisha baadae ndo akaanza kutoa taarifa kwa majirani.