Zipo stori kongwe kuhusu nyoka aina ya koboko kuwa kuna muda anawika kama jogoo. Hii ni kweli?
- Tunachokijua
- Kwa mujibu wa tovuti ya Saint Loius Zoo wanamtaja nyoka aina ya Black Mamba kama nyoka wakubwa, wenye kasi, wakali na wenye sumu kali, hivyo kuwafanya kuwa miongoni mwa wanyama wanaokamata nafasi ya juu kwenye mlolongo wa chakula katika mazingira wanayoishi. Wanaweza kufikia urefu wa takriban futi 14 (mita 4.2) na wana uwezo wa kutambaa kwa kasi ya maili 12 kwa saa katika umbali mfupi. Pia, wana uwezo wa kung’ata mara kwa mara, jambo linalowaruhusu kuingiza kiasi kikubwa cha sumu wanaposhambulia.
Madai
Kumekuwapo na madai kuwa kuna baadhi ya nyoka wanawika kama jogoo. Na baadhi ya wadau wamebainisha kuwa nyoka wa aina hiyo wanajulikana kama Black Mamba.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefanya ufutailiaji wa madai hayo na kubaini kuwa madai ya nyoka kuwika kama kuku si ya kweli.
JamiiCheck imewasiliana na mtaalamu kutoka chuo cha ukufunzi Mkufunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Tito Lanoy ameeleza kuwa dhana hiyo haina uhalisia kwani kutokana na muundo wa ulimi wa nyoka kugawanyika mara mbili huku wakiwa na meno madogo mbelel hivyo si rahisi kwa wao kuwika kama kuku.
"Sio kweli kuhusu dhana hiyo, ulimi wa nyoka ni kama kamba iliyogawanyika mara mbili kwa mbele na meno yake yanakuwa yameshikana na nyama, hakuna namna nyoka anaweza kutengeneza sauti kama jogoo".
Aidha mtaalamu amebainisha kuna baadhi ya aina ya nyoka wanaweza kutengeneza baadhi ya sauti ikiwemo kupuliza, au kuvuta kuvuta hewa ndani
"Kuna baadhi ya nyoka wanaweza kutengeneza sauti kama tatu hivi, mfano aina ya Kifutu ndio anaweza kupuliza na anafanya hivyo kama kutoa tahadhari.
Pia kuna nyoka wanafanya sauti kama ya kuvuta ndani, hiyo inaweza kufanywa na jamii ya koboko.
Aina nyingine ni sauti kama ya kuvuta kwa ndani hivi, hiyo inaweza kufanywa na nyoka jamii ya koboko, kobra n.k"