Kuna nini Tena Tandahimba?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Habarini, nilikuwa busy na masomo lakini toka Juzi nimekuwa
nikipokea sms kadhaa zikinipa taarifa juu ya mabomu yanayoendelea
kulipuliwa Tandahimba tena safari hii inaonekana vurugu hizo zimehamia
vijijini na si pale mjini. Nimepokea taarifa za vurugu ikiwa ni pamoja na
jaribio lililofanyika kijijini Kilomba(Mtwara vijijini) la kuwafungia baadhi ya
viongozi ofisini na kisha kuchoma moto ofisi hiyo hata hivyo viongozi hao
waliokolewa na polisi.

Waungwana taarifa hizi nazipata nusunusu tena kwa meseji za simu ya
mkononi. Mwenye taarifa zaidi atujuze chanzo cha vurugu hizo ingawa taarifa
zisizo rasmi zinasema wakulima wanalalamikia malipo kidogo ya awamu ya
tatu ya zao la korosho.
 
Back
Top Bottom