1.walimu wachache wanafunzi wengi kuna kipindi nilijitolea kufundisha math form 3 shule flan nilikuwa na stream 5 karibia wanafunzi 400 nambie hapo utatoa test ngapi usahihshe kwa wakati wazipate,mazoezi utatoa??kwanza muda unapata wapi na hata ukipata muda unachoka sana.nilikuwa napiga vipindi 12 kwa siku week nzima hapo nimejitolea mwalimu wa kuajiliwa hafanyi hivi.
2.wanafunz wa shule za kata wengi slow learner wachovu wanakotoka hapikwi vizuri kumbuka darasa la saba ni majibu ni kuchagua.....moja ya vituko nilivyokutana navyo mtoto anafika form 3 hajui table, kiingereza kinamsumbua wengine hata kugawanya mzozo hawajui
3.walimu wanajiita cheki namba hawana mzuka na kufundisha maana shule za umma mtoto akifeli akifaulu hapati chochote na maslahi yao madogo so ufundishaji ni ule bora liendeee
4shule za kata nyingi ni boys na girls na watoto wetu hawa wanaanza kuwaka ngono wakifika secondary so mapenzi pia ni sababu kubwa ya watoto kufeli watoto hawa waoneni hivi wanapiga na miti watoto wa kike wanatoa sana mimba yahn kuna mambo yanafanyika unasema hiki kazazi ni noooma.vitoto vinakutongoza mwalimu live live hahahaha.
5.hawa watoto wa shule za kata wengi pia wanatokea familia maskini hivyo hawazingatii shule kivile na wengine ni rahisi kurubuniwa.
6.walimu wana roho mbaya sana just mwalimu wa hesabu wa kujitolea shule nzima ina walimu watatu kisa nafundisha vizuri naingia bila kitabu darasani napiga pesa za tuition za hapa na pale navaa na kunukia nadhifu kuliko wao wakanifanyia mizengwe maskini mpka nikawaachia shule yao, wakienda walimu kuomba nafasi ya kujitolea mwalimu wa taaluma anawaambia shule ina walimu wa kutosha,sasa unajiuliza shule ya kata tangu lini ikawa na walimu tena wa sayansi wa kutosha???
Binafsi nayajua mazingira ya kata in out kozi nimesoma hizi shule wayback zinaanzishwa na nimefundisha miaka miwili niseme hizo sio shule za kupeleka mtoto... watoto wengi wanaharibika kwa kukutana na watoto wenzao wenye tabia mbovu na ikitokea umepeleka basi jitahidi sana mzazi umfatilie hatua kwa hatua mwanao