Kuna nini NIDA hadi vitambulisho havitoki tena?

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,845
2,000
Nchi zetu changa zinapelekeshwa kila siku na ubeberu. Ukiwepo mpango wowote wenye maslahi kiuchumi kwa umma ila unakinzana na maslahi ya ubeberu au vikaragosi vyao unakwama.

Ni vigumu mtu kuamini sababu zinazotolewa kila siku kwanini mpango wa Serikali kuwapatia wananchi wake vitambulisho vyenye ubora mkubwa kukwama. NIDA kuna jambo.

Inaelekea kila Mkurugenzi mpya akiwekwa anakutana na jambo. Hebu niambieni mbona vitambulisho vya wapiga kura kwa ubora huo huo vinakamilika lakini vitambulisho vya Taifa vinasuasua. Kuna watu hawataki kila mtanzania atambulike kwa maslahi yao mabaya kwa taifa.

Ni muda sasa wa kutimua panya wanaotafuna mradi wa vitambulisho vya taifa usiende unavyotakiwa. Mabilioni yanapotea bila faida kamili iliyokusudiwa kwa mradi wa vitambulisho vya Taifa.
 

sala na kazi

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,884
2,000
Niliwahi kusema hii nchi inahitajika vijana wadogo waaminifu waikimbize mchaka mchaka.

Yaani mijitu inalipwa bado inaweka mitambi juu ya meza 3+ years.

Inatia aibu + huzuni sana kwa kweli, vya kura ni kwa muda mfupi tuu,ila hivi wanajivita kama minyoo

Ilihali wizara ya mambo ya ndani .Chini ya Simbachawene alisema mpk July waTz wote watakuwa wamepata ID...ila mpaka saiv Holla.

Hii nchi inaongozwa kwa mihemko + maneno maneno tu.
 

BelindaJacob

Platinum Member
Nov 24, 2008
6,305
2,000
Tangu mwaka juzi sijapata hiyo ID. Mwaka jana nikaenda pale Kawe kufuatilia.

Mama niliemkuta pale ile nampa tu kikaratasi lenye jina langu aangalie akanijibu kwa lisauti hilo kuwa hakijatoka, hata hakucheki kwenye kompyuta. Nyuma yake maboxi mengi yamejaa hizo ID. NIDA washenzi sana.

Nikatafuta full nakala kwa network zangu, nimeki-laminate na inanisaidia kwa sasa.
 

dolevaby

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
12,293
2,000
Niliwahi kusema hii nchi inahitajika vijana wadogo waaminifu waikimbize mchaka mchaka.

Yaani mijitu inalipwa bado inaweka mitambi juu ya meza 3+ years.

Inatia aibu + huzuni sana kwa kweli...vya kura ni kwa muda mfupi tuu,ila hivi wanajivita kama minyoo

Ilihali wizara ya mambo ya ndani .Chini ya Simbachawene alisema mpk July waTz wote watakuwa wamepata ID...ila mpaka saiv Holla


Hii nchi inaongozwa kwa mihemko + maneno maneno tuu
Kuwa kijana na uaminifu vinafananaje?
 

Dream Queen

JF-Expert Member
Nov 4, 2015
4,996
2,000
Nakumbuka siku naenda kuchukua changu tulikalishwa masaa matatu hakuna kitu kinaendelea

Ila kuna watu wanafika wanachukua wanaondoka, tukaanzisha mtiti ndio wakatulia na kutuhudumia lakini walikua wajizungusha makusudi kumbe wanataka rushwa.

Hii nchi Rushwa haiwezi kuisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom