Kuna nini kuhusu shule binafsi kilichofichika?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,817
35,827
Nimeona habari hii

Barua ya ada yawatibua wamiliki shule binafsi

Kila mara serikali inapojaribu ku regulate sekta hii kumekuwa figisu kwelikweli.

Wamiliki wa shule hizi wanajua kuwa sekta zingine zote ziko regulated? Je wanajua wanetu wanapotakiwa kwenda na penseli mbili mbili kila mwezi, vifutio viwili viwili kila mwezi, madaftari duplicate mpaka ya mwalimu kimsingi tunakwazika sana basi tu?

Vipi michango hadi ya mishahara ya walinzi?

Yote bila ya kuongelea ada za shule hizi ambazo kindergarten tu mostly ni juu kuliko ada ya chuo kikuu?

Ndiyo maana kwa upande kwingine serikali ina point kuzuia mikopo kwa waliosomeshwa shule binafsi.
 
Hili la shule binafsi lilihitaji mamlaka kama ilivyo kwa ewura, Sumatra, nk.
 
Nimeona habari hii

Barua ya ada yawatibua wamiliki shule binafsi

Kila mara serikali inapojaribu ku regulate sekta hii kumekuwa figisu kwelikweli.

Wamiliki wa shule hizi wanajua kuwa sekta zingine zote ziko regulated? Je wanajua wanetu wanapotakiwa kwenda na penseli mbili mbili kila mwezi, vifutio viwili viwili kila mwezi, madaftari duplicate mpaka ya mwalimu kimsingi tunakwazika sana basi tu?

Vipi michango hadi ya mishahara ya walinzi?

Yote bila ya kuongelea ada za shule hizi ambazo kindergarten tu mostly ni juu kuliko ada ya chuo kikuu?

Ndiyo maana kwa upande kwingine serikali ina point kuzuia mikopo kwa waliosomeshwa shule binafsi.
Mnachokimbia shule za serikali ni nini?
Kwanini usiiambie serikali iboreshe shule zake ili hawa wenye shule binafsi wapunguze bei kwakukosa wanafunzi baada ya shule za serikali kufanya vizuri?
Yaani nyie mnataka mpaka shule za privaymte zianze kuzalisha vilaza kww kulazimisha waendeshe kwa mipango yenu wakati za kwenu zimewashinda?
 
Shida iliyopo Watanzania ni watu wabinafsi kuliko mfano, wanaosomesha hizi Shule wanapenda zibakie kuwa hivyo aghali ili wao tu ndo waweze kusomeshea watoto hapo lkn 95% ya wazazi wanaopenda Shule binafsi ziwe kwa ajili ya wachache wao walisomeshwa na Serikali bure lkn leo hii hawataki wasio na uwezo wafaidike!
 
Regulator wako anaangalia kodi

Regulators kama walivyo tcra, ewura, Sumatra, nk wajibu wao ni kulinda maslahi ya mlaji kwa niaba ya serikali.

Kama unayemwongelea ana makengeza basi huyo siyo regulator kama uzi unavyoonyesha umuhimu wa kuwa naye.
 
Mtoa mada ninawasiwasi na uelewa wako,shule binafsi ni hiyari ya mzazi kuamua shule gani unaweza mpeleka na wala siyo kuisubir serikali iingilie Kati pia ktk elimu hakuitaji siasa kiukweli, acha mambo yaende kitaalamu pia tambua cc wa tz tunaitaji maji,huduma bora ya afya,umeme wa uhakika na barabora zinazopitika muda wote kuliko kick za kisiasa za kuingilia Ada ya shule binafsi ili muonekane mnamjali mtanzania wa kawaida
 
Shida iliyopo Watanzania ni watu wabinafsi kuliko mfano, wanaosomesha hizi Shule wanapenda zibakie kuwa hivyo aghali ili wao tu ndo waweze kusomeshea watoto hapo lkn 95% ya wazazi wanaopenda Shule binafsi ziwe kwa ajili ya wachache wao walisomeshwa na Serikali bure lkn leo hii hawataki wasio na uwezo wafaidike!

Mkuu una hoja ya msingi. Suala hili limekuwa taboo kuongelewa. Nadhani serikali imekuwa na nia ya ku regulate hizi shule ila imekosa uungwaji mkono kutokana na ubinafsi utakaoendelea kutugharimu kwa muda mrefu sana sisi wadanganyika. Tena haswaaa wale tunaojidhania tuko vizuri kuliko wale.
 
juzi nilienda hosp nikakuta mgonjwa mwenzangu hohehae Kama mm amechajiwa 85,000/= hana bima ya afya....huyu anaitaji huduma bora na kuangaliwa kwa haraka kuliko kick za Ada elekezi, Serikali tuipe muda iangalie mambo ya msingi kuliko kuipa kazi ya kuregulate Adaaa
 
Mtoa mada ninawasiwasi na uelewa wako,shule binafsi ni hiyari ya mzazi kuamua shule gani unaweza mpeleka na wala siyo kuisubir serikali iingilie Kati pia ktk elimu hakuitaji siasa kiukweli, acha mambo yaende kitaalamu pia tambua cc wa tz tunaitaji maji,huduma bora ya afya,umeme wa uhakika na barabora zinazopitika muda wote kuliko kick za kisiasa za kuingilia Ada ya shule binafsi ili muonekane mnamjali mtanzania wa kawaida

Mkuu kusafiri na bus la umma au binafsi ni hiari ya mtu. Kama ilivyo hiari ku tune TBC au station binafsi. Uliwahi jiulize kwa nini huku kuna regulation?

Nikadhani hadi hapo kama ungali na wasiwasi na uelewa wangu utakuwa na matatizo zaidi.
 
mm nadhani unashindwa ku base ktk uhalisia mkuu, yapo mambo yakulia Lia ila siyo shule binafsiiii. Fikiria serikali imeweka shule zake bure na kila kitu unalipiwa tena unataka shule binafsi wakupangie Ada utakayo ww? Education is an investment.... Ww unahiari na siyo kulia lia
 
Education is an investment Boss
 
Mnachokimbia shule za serikali ni nini?
Kwanini usiiambie serikali iboreshe shule zake ili hawa wenye shule binafsi wapungze bei kwakukosa wanafunzi baada ya shule za serikali kufanya vizuri?
Yaani nyie mnataka mpaka shule za privaymte zianze kuzalisha vilaza kww kulazimisha waendeshe kwa mipango yenu wakati za kwenu zimewashinda?

Mkuu hayupo anayekimbia shule za serikali wala anaye aspire kusomeshwa au kusomesha private.

Soma uzi kuelewa usiwe mzembe wa kusoma ukajikuta warukia treni kwa mbele.

Mlaji anayo haki ya kulindwa bila kujali mtoa huduma ni nani. Huo ndiyo msingi wa huu uzi.
 
mm nadhani unashindwa ku base ktk uhalisia mkuu, yapo mambo yakulia Lia ila siyo shule binafsiiii. Fikiria serikali imeweka shule zake bure na kila kitu unalipiwa tena unataka shule binafsi wakupangie Ada utakayo ww? Education is an investment.... Ww unahiari na siyo kulia lia

Kuna haja ya kujaribu kukuitisha kujikita kwenye mada?

Mkuu uko mno nje ya mada kiasi kujaribu kukuitisha kuiona mada yaweza kuwa ni kupoteza muda.

Pole mkuu.
 
Shida iliyopo Watanzania ni watu wabinafsi kuliko mfano, wanaosomesha hizi Shule wanapenda zibakie kuwa hivyo aghali ili wao tu ndo waweze kusomeshea watoto hapo lkn 95% ya wazazi wanaopenda Shule binafsi ziwe kwa ajili ya wachache wao walisomeshwa na Serikali bure lkn leo hii hawataki wasio na uwezo wafaidike!
Ndio maana ikaitwa private na si gov or public schools. Private wanawazid gov schools kitu kimoja. Nacho ni miundo mbinu na mishahara ya walimu. Ili kuwa na miundo mbinu mizuri lazima gharama ziwepo, walimu nao walipwe mshahara wa mahana. Vyote hiv vinatoka kwenye ada za wanafunzi.
Lazima ada iwe juu.

Ww unataka washushe ada halaf vip wataweza maintain hiyo miundombinu?
Vip wataweza walipa walimu vizuri maana serikal haichangii msaada wowote wa fedha kwa hizi shule?
 
Mkuu msingi wa hoja watokea hapa:

Barua ya ada yawatibua wamiliki shule binafsi

Ulipata muda wa kusoma au umekurupuka tu?

Kwa nini ni taabu kutoa hiyo breakdown inayo uliziwa na serikali?

Kama ni siri si waseme tu?
 
Ndio maana ikaitwa private na si gov or public schools. Private wanawazid gov schools kitu kimoja. Nacho ni miundo mbinu na mishahara ya walimu. Ili kuwa na miundo mbinu mizuri lazima gharama ziwepo, walimu nao walipwe mshahara wa mahana. Vyote hiv vinatoka kwenye ada za wanafunzi.
Lazima ada iwe juu.

Ww unataka washushe ada halaf vip wataweza maintain hiyo miundombinu?
Vip wataweza walipa walimu vizuri maana serikal haichangii msaada wowote wa fedha kwa hizi shule?

Ndiyo hivyo, huo ndo ubinafsi wenyewe, kama Shule za misheni, Wazazi na Serikali wangesema hivyo wengi wenu mnaotetea ada kubwa kwenye hizi Shule labda msingesoma, wangeweza pia kusema unavyosema lkn hawakuwa Wabinafsi na hivyo kila mtoto alipata nafasi, leo hii mliosomeshwa bure mnataka hiyo privilege wawe nayo watoto wenu tu na siyo wa wengine!

Zaidi ya 90% ya Watanzania wa leo wamesoma bure!
 
Back
Top Bottom