Naamini wewe ni mtu mzima huwezi tu ukaibuka na kulalama
kitu ambacho hakipo... bahati mbaya hujaeleza sifa hizo ni zipi
maana yaweza kua sifa za kumsifia kua ana msaada mkubwa hapo
nyumbani i.e kusaidia shughuli za hapa na pale au sifa za maumbile
i.e. ooh mdogo wako ana mvuto, dah sijui kifua kimefanyeje n.k
Kikubwa na kizuri ni kua umetambua hizo sifa na hivyo ni dhahiri
hawajafanya mchezo wowote mchafu (naona ndo hofu yako)
maana angekua amefanya au anafikiria asingedhubutu kumtaja taja
mbele yako...
Mimi nakushauri mwambie kua mbona sifa zimezidi??? Walau apate picha
kua hupendi na pia kua wawafuatilia...
Pole saana kwa tatizo lako. Kila la kheri.....
VIKWAZO:
Because you have not found anything suspicious, the easiest thing for you to do I think is to just be open and let your wife know that you do feel uncomfortable na hizo sifa kem kem anazomwagia dogo! She just may not be aware how unconfortable you are, so start by letting her know, ili aache au apunguze.
yawezekana kutoka na ubusy na shughuli zangu wakawa na uwezo wa kunifunika maana ratiba yangu in kama kanuni za wokovu
hiko fix. sana hovyo bado nina mashaka kuna kitu
Katika makosa ambayo unatakiwa kuyaepuka ni kufanya maamuzi kwa kutepemea hisia,utakuja kujilaumu sana,kagua tabia ya mke wako kama alikuwa na historia ya kutokuwa mwaminifu,ila fuatilia piam na uchunguze kinachosababisha anamsifia kisha utoe maamuzi!
Lakini hata hivyo ni bora umwambie, ukiona hata baada ya kumwambia anashindwa kujisitiri na kuvimilia, then at least utajua ana lake moyoni. Ila pole, lakini pia si vizuri, kuwazia mabaya peke yake. Inawezekana labda anasema hivyo ili na wewe uhamasike na kufuata vitu positive she sees from dogo. Kwa mfano, kama wewe ni mnene na mwenye kitambi, basi upunguze, kama wewe ni mkali, basi uwe mwenye upole and upendo kama dogo etc
jaribu kuvunja ratiba! uje home muda usiotarajiwa, uone hali ikoje. Ikiwezekana, njoo bila hata usafiri wako wa kawaida!
jamii leo nimeona nijisalimishe haba kwenu labda nitapata maarifa.
mke wangu ana msifia sana mdogo wangu wa kiume, yaani kuna wakati hata hakuna humuhi wa hizo sifa lakini yeye anamwaga tu sifa kwa bwana mdogo!!!!!!
nimefanya utafiti sijagundua kitu chochote mimi nampenda sana mdogo wangu nashindwa kumuondoa hapa nyumbani kwa kutumia hisia tu kwamba yawezekana kuna kitu kati yake na mama watoto au mama watoto anakitu kichwani?
mahusiano yetu yako sawa tu sijagundua kasoro, lakini sifa na maongezi muda wote kuhusu bwana mdogo sasa yanaanza kunipa ishara mbaya kichwani mwangu
naombeni maarifa sitaka kuchemka nawajari na kuwapenda wote, mmoja kama mke na mwengine kama ndugu