Kuna nini katika soko la programming na TEHAMA Tanzania?

Kyatile

JF-Expert Member
Feb 5, 2017
1,576
1,395
Kila siku tunasikia wimbo kwamba TEHAMA tuko nyuma, tunahitaji wataalamu. Tunaona serikali ikihama kutoka kwenye paper files kuelekea kwenye mfumo wa mtandao; kuanzia malipo, maombi ya ajira, maombi ya vyuo, usajiri wa wanafunzi wa shule nk.

Lakini cha ajabu vijana wengi wanaomaliza wanakosa ajira na wamekata tamaa. Ni nini kinasababisha vijana waliosoma TEHAMA kukosa ajira? Tulitegemea mapinduzi katika ICT yachochee ajira kwa vijana katika sekta hiyo.

Je vijana wanaotegemea kusoma courses za TEHAMA kama CS, CE, SE, IS wafanye nn ili waweze kunufaika na fursa zilizo katika ICT?
 
Msimu wa neema embe ni nyingi hadi kukosa soko na hatimaye kuoza shambani. Taifa linazalisha wataalam wengi zaidi ya mahitaji- tatizo oversupply ya mundane coders????
 
Msimu wa neema embe ni nyingi hadi kukosa soko na hatimaye kuoza shambani. Taifa linazalisha wataalam wengi zaidi ya mahitaji- tatizo oversupply ya mundane coders????
Oversupply ya programmers hata marekani hawajafikia io state, ije iwe sisi
 
Msimu wa neema embe ni nyingi hadi kukosa soko na hatimaye kuoza shambani. Taifa linazalisha wataalam wengi zaidi ya mahitaji- tatizo oversupply ya mundane coders????
Sasa mbona system ambazo tunazitumia ni mbovu hao programmers wanafanya nn sasa? Mfano sote tumeshuhudia mfumo wa kuomba ajira serikalini imeshindwa kukidhi mahitaji wa waliokuwa wanaomba ajira, na mara nyingi umekuwa overloaded. Kama programmers wapo mbona serikali imekosa solution ndogo kiasi hicho?
 
Tatizo ni kuwa vijana wengi waliohitimu wamehitumu basic computer application tu ,na wengi hawana UJUZI wote zaidi ya kuwa na vyeti...tu ndio maana tu aona waganda na wake ya wameajiriwa sana , MAJUZI juzi tu hapa Nectar wameajiri vijana wengi sana wanaoshughulika na maswala ya Tehama wito wangu vijana km unapenda TEHAMA ,kubali kutokuwa mvivu katika kujifunza Kila siku computer language zinaongezeka .... Tubadilike na pia kwenye uchanguzi wa kozi tufanye tafiti sana kabla ya koptic
 
Back
Top Bottom