Kuna nini Ikulu???!!!!

Irizar

JF-Expert Member
Oct 6, 2009
217
18
Leo, jana na juzi nasikiliza habari za mkanganyiko uliotokea huko Ikulu, kuhusu magari ya kubebea wagonjwa yaliyokuwa yakabidhiwe na Raisi wetu siku ya Jumatatu 18/01/2010. Badala ya kupewa wilaya iliyokuwa inatakiwa kupewa, akaja mtu wa wilaya nyingine kupokea hilo gari.
Mimi nashindwa kuelewa inakuwaje mkurugenzi katoka Ngorongoro mpaka Ikulu DSM, kuja kupokea gari na hakuna aliyeshituka mpaka raisi mwenyewe kaishitukia dili hiyo.
Sasa hawa wasaidizi wa raisi wetu wanafanya kazi gani??? hawahakiki mambo kabla ya JK kufika hiyo sehemu? tuliona pia miaka michache wakati Raisi JK alibeba cheki ya NMB ikiwa na maandishi tofauti kuliko ilivyotarajiwa, pikipiki alizotakiwa kugawa raisi akashitukia mwishoni hakuzigawa, akaenda kufunguwa hotel Arusha then the next day hotel ikavunjwa. Hivi ni kitu gani hiki.
Nilidhani watu walio wa karibu na raisi wangehakikisha haya makosa madogo madoga na ya aibu hayatokei.
Je kuna watu wanawajibishwa baada ya kufanya uzembe tunaousikia, au kwa vile ni ndugu, rafiki na washikaji wanaachiwa tu?.
Inasikitisha sana ofisi kubwa kama Ikulu inapofanya uzembe wa kijinga namna hii.

Naomba tuchangie ndugu wadau maana nchi inajengwa na watanzania wenyewe.
 
Back
Top Bottom