Kuna nini cda dodoma ??????

kalukamise

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2011
Posts
683
Reaction score
191
Wana JF naomba msaada kwa yeyote mwenye jawabu kwa yafuatayo...
Wakazi wa majumba ya CDA Iringa road wanatakiwa kuhama ati kupisha matengenezo, swali watu hao wataishi wapi ??? kipindi cha matengenezo huu si ni uhamisho ndani ya nchi yao.
Pili kupandisha kodi toka 75,000 - 200,000 kwa mshahara gani ?? vinginevyo si wangezirudisha NHC wakazikodisha kwa wenye kipato cha chini na kati ??
Nasikia harufu ya ufisadi
 
kwani ulikuwa hujui ufisadi wa MAMLAKA YA UZOROTESHAJI MAKAO MAKUU?aka SIDIEI
 
kuna tafiti ilifanyika hapo dodoma kuhusu taasisi inayoongoza kwa kuchukua rushwa, CDA iliongoza kwa asilimia kubwa mara tatu ya polisi iliyoshika namba mbili, hao jamaa wa cda ni hatari kwa kuchukua rushwa kuanzia getini kwa mlinzi mpaka kwa mkurugenzi
 
kwani ulikuwa hujui ufisadi wa MAMLAKA YA UZOROTESHAJI MAKAO MAKUU?aka SIDIEI

umeona ee.. wapangaji wa Iringa road wamefungua kesi mahakamani kupinga kuhamishwa kiaina hivi.
 

Mkuu umeua hawa jamaa wanatisha aisee, ishu nyingine ni kwanini hawauzi viwanja, hivi toka 2009, mpaka leo ongezeko la watu wote dom wanategemea watu watajenga wapi?, si ndio maana slum haziishi nchi hii
 
Daaa hao CDA huwa ctaki hata kuwasikia! Ramani yangu ina mwaka wa 3 haijapitishwa sasa! &?*^@#+*&*^%

Mkuu kumbe na wewe na mhanga wa sidiei pole sana, kodi wanapandisha katika nyumba ambazo hazijakarabatiwa miaka nenda rudi, mbaya zaidi ni ongezeko la zaidi ya 100% ( maisha bora teh teh )
 
Sidiei, ni taasisi nyingine ambayo ni vigumu kueleza kwa mtu yoyote mwenye uwezo wa kufikiri na kupambanua mambo kuwa kwa nini ipo, na inafanya nini ambacho hakiwezi kufanywa na mamlaka za serikali za mitaa kama Manispaa. Wakazi wengi wa Dodoma watakubaliana na mimi mwingiliano wa kisheria, kimamlaka na kiutendaji uliopo kati ya CDA na Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma. Kwa kifupi, CDA ni moja ya kero kubwa kwa wakazi wa Dodoma na inaonekana ipo tu kwa sababu watu fulani kwenye system wanataka iendelee kuwepo hata kama haina maslahi kwa wananchi. Haya ndio matatizo ya serikali inayotokana na mfumo ambao mwanazuoni mmoja aliwahi kuuita: "Government buy the people, fool the people, and off the people". Msisitizo ni wangu.
 

mkakati uliopo ni kupandisha bei,ukarabati unakuja kama kigezo cha kuwawezesha kuwatoa wapangaji waliong'ang'ania kwenye hizi nyumba ambao si wa hali ya chini kama tunavyosema,watu wanajenga nyumba zao wanapangisha tena kwa bei kubwa afu wakipandishiwa hela ya pango wanaenda mahakamani wengi wao ni wafanyakazi,kuna wengine wamehamishwa kikazi kwenda mikoa ya mbali badala ya kuzirudisha cda nao wameanza kupangisha wakilipwa hadi 160,000/= kwa mwezi ili wao walipe 75,000/= kwa cda,afu nyumba hizi asilimia kubwa zimechakaa na kubaki kama magofu kwa kutofanyiwa ukarabati ata kidogo.
Ni bora cda wakaja na utaratibu mwingine ambao utasaidia pande zote mbili pamoja na mkataba wa mda maalumu wa mwisho wa mtu kuishi kwenye nyumba hizi kama miaka ata mitatu mtu anakuwa amejipanga kidogo kuweza kumdu gharama za mtaani ili wanao anza kazi au watu wa hali ya chini waweze kupewa kipaumbele kuishi kwenye nyumba hizi.
 
kuna mkurungezi sijui aliachishwa kazi au walimhamisha hadi mtoto wake wa mwaka mmoja alikuwa anamiliki viwanja zaidi ya 15!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…