Ushimen
JF-Expert Member
- Oct 24, 2012
- 42,579
- 105,441
MSIPOTEZE MUDA MLIOPEWA NA MUNGU, WA KUISHI NA MKEO AU MUMEO AMA MPENZI WAKO, KWA KUNYANYASANA NA KUGOMBANA. KUNA MUDA MCHACHE SANA WA KUPENDANA..!! TAFAKARI ANDIKO HILI:-
AYUBU 14 :1-2
Mwanadamu aliye zaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu, yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa, hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.
Mpende uliye naye na muonyeshe mapenzi ya kweli, kwani kuna siku ataondoka na utatafuta wa kumuonyesha mapenzi ya kweli hutampata.
Si kila mtu anafaa kuwa mke au kuwa mume ama kuwa mpenzi. Wewe uliye na mke/mume au mpenzi wako hivi sasa, huwezi kuelewe kwa haraka, ila mjane aliyepoteza mume au mgane aliyepoteza mke ama yeyote aliye poteza mpenzi anaelewa nyakati anazopitia. Anatamani amuamshe mwenzake amuonyeshe upendo, ila ndiyo haiwezekani tena.
Kuna Siri kubwa mbele za Mungu ya kuishi wawili, na ndio sehemu ya kumalizia maisha yako ukiwa duniani, maana ulisha zaliwa, ukakua ukatengana na wazazi. Sasa penye maisha ya mwisho kabla ya kuitwa na Mungu ni NDOA/mwenza.
Ndiyo maana andiko linasema:-
WAEFESO 5 :31-33
Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hiyo ni kubwa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe, wala mke asikose kumstahi mumewe.
Watu wengi wanachezea upendo wanaopewa leo na wake zao, au waume zao ama wapenzi wao, kwa kuwa wanadhani hautakoma, na siku ukikoma utajutaa.... Kuna siku utatamani kumwambia mume wako au mke ama mpenzi wako kuwa unampenda, lakini hatakuwepo..!!
MPAMBE MWENZIO KWA MAUA KWA SASA AKIWA HAI, AKIONA KWA MACHO YAKE KWAMBA MAUA YAKO NI UPENDO. USINGOJE KUPAMBA KABURI LAKE KWA MAUA, HAITASAIDIA TENA.
KWA NINI UTUMIE MUDA WAKO MWINGI KUTENGENEZA UGOMVI, CHUKI, NA MANYANYASO KWA MKEO AU MUMEO AMA MPENZI WAKO..?
TAFAKARI