Nimesoma hiyo thread yako nikakumbuka quote ya Tuff Gong.
Life is one big road with lots of signs so when you riding through the ruts don't complicate your mind. Flee from hate, mischief and jealous. Wake up and live.
Kwangu mimi si tatizo hali uliyonayo. Tatizo ni kuendelea kuwa hivyo.
Kama upo mzima, unavuta pumzi basi hapo lipo tumaini. Na unaweza kubadili maisha yako.
Labda pengine kwa kubadili namna unavyojifikiria tu.
Mafanikio ni namna ile unajisikia fahari na furaha vile unavyoishi.
Si kila mtu anataka awe na gari kama lako.
Si kila mmoja anataka anunue nguo kama zako.
Au nyumba kama yako.
There is so much to offer. Even the most greedy person can't take it all.
Mimi nikiwa napitia magumu najiangalia kwenye kioo. Najilazimisha kutabasamu. Nakubali mambo ni magumu. Lakini najisemea lazima niendelee. Nijaribu tena.
Tumaini linaondoka pale unaaga dunia. Kama ungali mzima endelea kuwa dreamer.
Haijalishi watu watawazia nini.
Na ile siku ukiamua kuuona ukweli huu na kuanza kuishi maisha yako, unageuka unakuwa Simba. Sauti ya ushujaa inanguruma ndani yako. Wewe siyo kondoo tena.