Kuna mgao wa umeme wa kimya kimya

Kuna mgao wa umeme wa kimya kimya

Sababu sio hizo tu, kuna zaidi ya hizo kama tulivyo ainisha, umetoa taarifa kuhusu kukatika kwa umeme eneo ulilopo? Umepewa namba ya taarifa?
Nami nauliza ni kwa nini mmekuja kuweka nguzo mtaani na kutuhamasisha tufanye wiring kisha mkatuhadaa kwamba transformer ya mtaa wa pili haina uwezo wa kutuhudumia kwa hiyo mtaleta nyingine, matokeo yake tunaishi kama vifaranga tukiamini nyonyo kesho na ilihali ni mwaka na miezi imepita tunashuhudia kunguru tu wakicheza kwenye nyaya? Mungu awatie nguvu tanesco kwa upendo wenu. AMINA
 
Sisi mda huu tunajiandaa kukatiwa kurudi mida ya saa tano au sita usiku
 
Huku 12 kamili washakata tunasubiria waturudishie kesho saa 4 asubuhi kama watapenda
 
Huku niliko ulikuwa unakatika saa 6 mchana hadi saa 10 jioni kwa siku tatu mfululizo. Leo naona hawajakata.
 
Maeneo mengi kukatika umeme hasa dar imekuwa sehemu ya maisha umeme kukatika saa sita hadi nane kwa siku bila taarifa zozote hii ni kila siku tena unaweza kukatika mara nyingi kwa siku unakuja unakata unarudi unakatika tena .

TANESCO wanataka kuturudisha miaka ya 2000-2015 ni vyema mh rais uchukue hatua kubwa maana hii sio vema kwa inchi ya viwanda na uchumi wa kati

USSR
Mwanza ni kila siku wanachukua mchana wanarudisha usiku.
 
Hakuna mgao wa umeme Mteja, umeme upo mwingi wa uhakika na wa kutosha na hadi sasa uwezo wa kuzalisha umeme katika gridi ya Taifa umefikia Megawati 1,565.72 na matumizi ya juu ambayo yamefikiwa (peak demand) ni megawati 1,177.20, utaona kabisa kutoka hapo umeme upo wa kutosha na ziada.

SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA KUKATIKA KWA UMEME

1. TANESCO itakata umeme BILA kuwataarifu wateja endapo kuna sababu zifuatazo:-
a) Kuna mali inaungua (Mf. nyumba, kiwanda au mtambo)
b) Kuna mtu kanaswa na umeme.
c) Dharura emergencies (imeelezwa hapo chini namba 4)

2. TANESCO itakata umeme baada ya kuwataarifu wateja - Planned Interruptions endapo:-

a) Kuna matengenezo Kinga yaliyopangwa kufanyika ili kuimarisha miundombinu Planned Preventive Maintanance (Mf. Kubadili nguzo zilizooza, kubadili waya chakavu, kubadili transfoma ili kuongeza uwezo wa umeme nk)
b) Matengenezo ya kila mara Routine Maintanance (Mf. Kukata miti inayogusa line za umeme, kukagua vikombe na vifaa vingine kwenye line)
c) Kumuunga mteja mkubwa kwenye line ya msongo mkubwa wa umeme 11kV au 33kV

3. SABABU zinazoweza kusababisha umeme kukatika kwa dharura Emergency cases nyingi ni Unplanned Interruptions

a) Za kiasilia Natural Calamities (Mf. Radi kupiga transfoma, mvua au upepo mkali kuangusha nguzo, kukata waya, miti au minazi au matawi ya miti kuangukia line, mafuriko, wanyama kama komba, nyani, nyoka, kunguru kunasa kwenye mifumo ya umeme nk.

b) Hujuma za kibinadamu Sarbotage
(Mf. Transfoma kuibiwa mafuta, kuibwa nyaya za umeme, nguzo kuchomwa moto na kuanguka, nguzo kubwa kuibiwa vyuma na kuanguka, magari kugonga nguzo za umeme na kuanguka, malori marefu kwenda juu kukata waya za umeme, wateja kukata miti ikaangukia kwenye line nk.

C) Uchomaji wa miundombinu ya umeme kama nguzo.

Hizi ni baadhi tu ya sababu za msingi zinazoweza kusababisha umeme Kukatika. Hivyo ieleweke kuwa sio kila KUKATIKA KWA UMEME -TANESCO wamekata ni suala pana linalohitaji kujua sababu. Wakati mwingine kwa maelezo hayo hapo juu, umeme unakatika hata TANESCO inabidi kufuatilia mifumo ili kujua sababu za kukatika.

Tunaomba umma uelewe sababu hizi na kuwa TANESCO tunaamini hakuna Mfanyakazi wa TANESCO anaweza kulihujumu Shirika kwa kukata umeme bila sababu au kukata umeme bila kufuata maagizo na utaratibu wa kukata line uliowekwa. Sio kila mfanyakazi au fundi anaweza kukata umeme. Upo utaratibu na wakati mwingine wa kimaandishi unaompa fundi ruhusa, kabla ya kukata umeme.

Tafadhali usiguse wala kukanyaga waya uliokatika au ulioanguka chini, toa taarifa Ofisi za TANESCO zilizo karibu.

Wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo: - Kitengo cha Miito ya Simu 0222194400 na 0768 985100

Tovuti:
www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii:

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook Tanesco Yetu

Huu uzi ni wa mwanzo wa Desemba, miezi mitatu iliyopita, mbona jana ulikuja na maelezo kuwa ni matengenezo ya madogo madogo. Hii kukatika kwa umeme ni zaidi ya miezi mitano sasa,na ww TANESCO unajua nini sababu, ila unaleta porojo za kisiasa.

Cc: athlete
 
Acha kulalamika umeme uko wa kumwaga mbona

Ova
 
Mtaelewa tu ! Mitano tena akikataa tumlazimishe ,nasema uongo ndugu zangu?
 
Huku Ukonga tumeishaanza kuzoea kadhia ya kukatika kwa umeme! Inakera pale tunapoelezea kukatika kwa umeme halafu mmoja anaejiita MTANESCO anajitokeza bila aibu kukanusha ukweli. Ukweli ni kwamba kuna shida ya umeme na TANESCO wana la kujibu. Hatutaki majibu mepesi kwa maswali magumu.
 
Imekuwa desturi sasa Arusha mnakata bila taarifa! Siku zote leo ndio mmetoa taarifa tena isiyo na mashiko
 
Yani kama leo siku nzima maeneo mengi ya Dar es Salaam hakuna umeme. Sijui hawa Tanesco wanafanya nini? Bila hata taarifa!
 
Halafu mtu anawekeza kwenye ndege wakati huduma za msingi za jamii zinasuasua kama hivi!!
 
Back
Top Bottom