Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,917
Sioni mantiki ya watumishi kuendelea kukatwa mishahara yao kuchangia vyama vya wafanyakazi kama TUGHE ,n.k maana sioni kama wanatimiza lengo kuu la kuanzishwa kwa vyama hivi.
Licha ya matatizo yanayowakabili wafanyakazi wa nchi hii,hata shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) nalo limekuwa kimya,bubu na butu na lisilo na msaada wowote kwa wafanyakazi.
Viongozi wapya wa shirikisho hili tangu wamachaguliwa hawajaonyesha tofauti yoyote na uongozi uliopita sasa sijui wana jipya gani la kuwafanya wastahili kulipwa kutoka kwenye michango ya wafanyakazi.
kuendelea kukatwa mshahara kuchangia Taasisi hizi za wafanyakazi zilizolala ni sawa na kutupa hela kusikojulikana/jalalani..