Majighu2015
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 2,936
- 3,958
Nilipata wasaa wa kuangalia kipindi maalumu Maguli akiwa ziarani mkoani Mtwara. Kuna mambo alikua anaagiza yafanyike mpaka najisemea hivi mawaziri na team zao walikua wapi? Baadhi ni kama hivi
1. Magari ya Dangote yamekaa bandarini miezi miwili ila Rais alivyopiga simu bandarini wakayatoa. Hivi kweli kila kitu mpaka Rais aagize? Mbona watu hawataki kufanya kazi zao?
2. Rais kaagiza gas ipelekwe kwenye kiwanda cha Dangote Mtwara. Ni 10km kutoka gas ilipo lakini wizara husika imeshindwa kupeleka gas ili kiwanda kiweze kufanya kazi vizuri. Hili nalo wasaidizi wa Rais wameshindwa mpaka Rais atoe maamuzi?
3.Rais kaagiza Dangote apewe eneo huko yanapopatikana makaa ya mawe(sikumbuki ni mkoa gani) ili achimbe mwenyewe na kupeleka kwenye kiwanda chake. Kuna kampuni imepewa kazi ya kuchimba makaa ya mawe lakini hamna wanachofanya. Waziri na team yake wapo tu na wanakula kodi zetu.
Sasa kuna mambo mengi ya hovyohovyo hivi lakini viongozi wapo tu wanadunda bila wasiwasi. Tunashindwa kutumia resources zilizopo kujiendeleza sababu ya umimi na uchoyo wa viongozi wetu. Sina uhakika kama mawaziri na viongozi wengine wana TOR za kazi zao mana wangekua nazo wangefanya kazi badala ya kulialia. Honestly tuna safari ndefu sana mpaka tufike huko tunakohitaji.