Kuna kitu nakiona kwenye ulimi wa Mh. Freeman Mbowe

marcus rojo

JF-Expert Member
Mar 19, 2017
1,496
5,317
KUNA KITU NAKIONA KWENYE ULIMI WA FREEMAN MBOWE. ''

Mishale ya saa iliyokuwa ikimuonyesha muda wa tabasamu..Ghafla imesimama kwenye dakika za huzuni..Siamini kama kifua chake kimebeba moyo wenye furaha kwasasa..Kama ipo basi ni furaha bandia, anayoitengeneza kwa nguvu kubwa mno..Ili igeuke tiba ya kuua bacteria wa simanzi waliomzonga nafsini.

Misukosuko inayofanya maandamano bila ruhusa wala kibali kila siku ihitwayo leo ktk maisha yake. Huenda kwa sasa inafanya ubongo wake uzalishe mamillion ya pipa za chuki na neno siasa chafu..

Ninasema haya sababu naamini. Ukweli unatabia ya kusimama hadharani bila kuvaa nguo ya ndani..Ili wenye macho ya haki wapate fursa ya kuutazama vema.

Walianza kumbomolea Club billcanas.. Wakampa tuhuma za kujihusisha na biashara ya unga. Wakaja kumuharibia shamba alilotumia mamillion kufanya uwekezaji..Muda wote huo, hasira yake ameizika kwa kutumia koleo ya hekima na sululu ya busara..Nimejaribu kuvaa viatu vyake kwa muda wa sekunde zisizozidi 45 tu..

Jibu nililopata nihili..Mitihani anayoipitia, ili mtu uweze kuifaulu inakulazimu uingie chumba cha mtihani ukiwa umejivika joho la Mtume au Yesu Kristo.. Sijajua yeye kavaa joho lipi kati ya hayo mawili?!

Namuongelea FREEMAN ELIKAERI MBOWE. Mbunge wa jimbo la hai na mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA.)

Huyu ni mwanasiasa aliyetunukiwa ulimi wa dhahabu..Huwa anatafakari kabla ya kusema na anasema akisha tafakari. Mtazame juzi akielezea kusikitishwa na mauji ya kibiti.. Au kayarudie maneno aliyoyaongea kwenye msiba wa marehemu mzee Samwel Sitta..

Mbowe kila anaposimama kuongea kwenye uma.. Ni ngumu kuimaliza hotuba bila kutoa mahubiri yanayoimiza umoja, mshikamano, utu nakuheshimiana. Bila kujali itikadi za dini wala vyama vya siasa..

Licha ya madhira yote anayoyapitia. Mbowe bado ameendelea kusisitiza umoja. Akiamini mlinzi bora wa amani ni haki na usawa kwa watu wote..Kwenye taifa ambalo watu wake mioyo yao imeivilia damu za chuki baina yao..Bunduki na mabomu havijawai kuwa mlinzi wa amani..

Taifa lilipofika kwa sasa linahitaji viongozi wenye ulimi kama wa mbowe. Ambao watakuwa wakihubiri umoja na amani kwa maneno namatendo.. Zile chuki za wazi wanazoonyeshana wabunge dodoma..Nikiashiria chakwamba tumevimbiwa amani. Tusipoamua kuwa wa moja..Zile chuki siku zikitoka kwenye mlango wa bunge. Tafsiri ya neno AMANI. Tutaishia kuisoma ndani ya kamusi..

Kwanini nimeamua kuitoa hii makala kwa Mbowe?!!. Sababu viongozi wengi wanahubiri wasichokitenda, na wanatenda wasichokiamini.

Napenda ku declare interest. Mimi sio mfuasi wa chama chochote cha siasa. Ila siku zote fikra zangu uungana nakuishi ktk kundi la watu walio kwenye mlengo wa siasa safi na uongozi bora. Wanaoishi kwa kuiabudu katiba nakuiheshimu misingi ya haki, usawa, na utii wa sheria bila shuruti..

Written by Green Osward
 
Unakwepa kodi....Unaharibu mazingira..unaihujumu NHC ...Unahusishwa na fedha nje ya nchi...Unahusishwa na ngada...

Yote haya yalihitaji busara moja tu...kujiuzulu uwenyekiti kwa maslahi mapana ya Chama.

Busara aliyonayo ni kucompromise chama chake kwa kukaribisha,kumlea na kumtetea fisadi mkuu.

Na hilo litautesa moyo wake na wafuasi wake milele hadi watakapomuondoa fisadi.

Busara zake hizi zilitoa mwanya kwa CCM na nchi kuanza upya...ni busara njema na abarikiwe.
 
Umeongea vizuri lakini hayo ni maneno anayotakiwa kuongea kila kiongozi.

Matatizo uliyoyasema kuhusu,Billicanas,Shamba na Biashara ya madawa ya kulevya ni mambo binafsi ya Mbowe hayana uhusiano na mambo ya siasa au uongozi wake.

Watanzania tusipende kuchanganya mambo binafsi na mambo ya uongozi.
 
Wabunge wa ccm kila kitu ndiyooooooooo, hawa ghasia utadhani ni Mwanamke mama ntilie wa bandari, yaani anatia aibu
Anaweza kuwa shemeji yako kwa mdogo wako au mama yako mdogo kwa baba yako...Mke wa pili!!:D:mad::(
 
Mbowe atakapoachia uenyekiti chama kitapasuka hakuna ninayemuamini ukimtoa mbowe waliobaki nawatazama kilipumba lipumba.
Kumbe bado hakijapasuka hata baada ya kubeba MAFISADI ya CCM?
Kina bahati!
 
Unakwepa kodi....Unaharibu mazingira..unaihujumu NHC ...Unahusishwa na fedha nje ya nchi...Unahusishwa na ngada...

Yote haya yalihitaji busara moja tu...kujiuzulu uwenyekiti kwa maslahi mapana ya Chama.

Busara aliyonayo ni kucompromise chama chake kwa kukaribisha,kumlea na kumtetea fisadi mkuu.

Na hilo litautesa moyo wake na wafuasi wake milele hadi watakapomuondoa fisadi.

Busara zake hizi zilitoa mwanya kwa CCM na nchi kuanza upya...ni busara njema na abarikiwe.
Una undugu na Musukuma?
 
Kaka FISADI mkuu mpelekeni mahakamani si mulianzisha wenyewe?
 
Unakwepa kodi....Unaharibu mazingira..unaihujumu NHC ...Unahusishwa na fedha nje ya nchi...Unahusishwa na ngada...

Yote haya yalihitaji busara moja tu...kujiuzulu uwenyekiti kwa maslahi mapana ya Chama.

Busara aliyonayo ni kucompromise chama chake kwa kukaribisha,kumlea na kumtetea fisadi mkuu.

Na hilo litautesa moyo wake na wafuasi wake milele hadi watakapomuondoa fisadi.

Busara zake hizi zilitoa mwanya kwa CCM na nchi kuanza upya...ni busara njema na abarikiwe.
Hujafikilia wanaodanganya watu kwa makenikia wanaogegeda hadi mayai yao hujafikilia hilo au nazo ni busara kwa ccm
 
Back
Top Bottom