Nikiri wazi mimi sio muumini wa tatoo, na sizipendi kabisa kuziona kwenye mwili wangu. Lakini cha kushangaza nimeamka asubuhi, nikawa nahisi kipele mgongoni ikabidi nijiangalie kwenye kioo, kweli kipele kilikuwepo ila kilichonishangaza nimeona kwenye bega la kulia kuna herufi "G". imechorwa vizuri kwa herufi kubwa. Na mimi sijawahi hata kufika kwa wachoraji wa hizi " TATOO" najiuliza imetoka wapi nakosa majibu. Labda wana jamvi kama kuna mtu, jambo kama hili lilishawahi kumtokea, au ana ufahamu kuhusu hili jambo naomba tueleweshane. Kama halina athari yeyote labda ya kiroho na kimwili.