Kuna kipindi idadi ya watu duniani ilibaki takriba 1000 dunia nzima

Kuna kipindi idadi ya watu duniani ilibaki takriba 1000 dunia nzima

P h a r a o h

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
993
Reaction score
1,882
‎Utafiti kuhusu vinasaba vya binadamu unaonyesha kuwa kuna kipindi katika historia ambapo binadamu walikaribia kutoweka kabisa.

‎Takribani miaka 70,000 hadi 75,000 iliyopita, idadi ya watu duniani ilishuka kwa kasi sana na inakadiriwa idadi ya watu duniani ilibaki kati ya 1000 hadi 10,000.

‎Dunia iliingia katika wakati mgumu sana wa mabadiliko ya hali ya hewa baada ya mlipuko mkubwa wa volkano ya Toba iliyotokea maeneo ya Indonesia, mlipuko uliosababisha majivu yenye kemikali kutanda angani na kubadili hali ya hewa ya dunia kuwa baridi kali na kusababisha ukame uliovuruga maisha karibu kila sehemu ya dunia.

‎Katika kipindi hicho, makundi mengi ya binadamu wa zamani yalipotea kabisa. Waliofanikiwa kuishi walikuwa wachache sana, hasa katika baadhi ya maeneo ya Afrika ya Mashariki na Kusini ambako bado kulikuwa na maji, chakula, na hali ya hewa iliyovumilika. Maeneo haya yakawa kama kimbilio la mwisho la binadamu wakati sehemu nyingine ya dunia ikiwa haikaliki.

‎Kutoka kwa watu hawa wachache waliobaki ndipo binadamu wa leo walipoanza tena kuongezeka na kuenea duniani. Taratibu walijaza Afrika, kisha wakasambaa kwenda Mashariki ya Kati, Ulaya, Asia na sehemu nyingine za dunia.

‎Tukio hilo lilipunguza mgawanyiko wa vinasaba kwa binadamu ( Genetic Diversity ) hadi leo, ndiyo maana binadamu wanafanana sana vinasaba ukilinganisha na wanyama wengine.

‎Kupungua huku kwa tofauti za vinasaba kumeathiri namna tunavyorithisha baadhi ya magonjwa, jinsi miili yetu inavyopambana na vimelea, na jinsi sifa fulani za kimwili zilivyoenea haraka kadri watu walivyohamia mazingira mapya.

‎Hivyo katika istoria ya binadamu Kulikuwa na wakati ambapo spishi yetu ilikaribia kufutika kabisa duniani. Kwamba tulinusurika ni kwa sababu ya makundi machache yaliyoweza kustahimili mazingira magumu na kuanza upya maisha ya binadamu duniani.

 
Mhh andiko lako haliingii akilini kirahisi.
Kwamba anga ya east afrika haikuthurika, je wanyama walifanikiwaje kutokufa?

Mfano kama walibakia wanyama wa east afrika wenyewe nani aliwavusha maji kwenda haya mabara mengine?
 
Mhh andiko lako haliingii akilini kirahisi.
Kwamba anga ya east afrika haikuthurika, je wanyama walifanikiwaje kutokufa?

Mfano kama walibakia wanyama wa east afrika wenyewe nani aliwavusha maji kwenda haya mabara mengine?
hadi dunia nzima iliathirika hadi east africa ila kulikua na nafuu kidogo maeneo hayo
 
Screenshot_20260212-133952.png
 
Back
Top Bottom