Kuna halmashauri ni za hovyo mno!

Mfumo wa ugatuzi hauko sawa ndio maana kila kitu kinategemea Centra government..
Na Rais pia hapendi kupunguziwa madaraka yake kwasababu anapata chance za kupiga, kulipa fadhila, kuhonga vyeo na kulinda nafasi yake.

Mfano: Issa Michuzi ni MTU wa karibu na Kikwete na mpiga picha wa Ikulu wa muda mrefu.

Leo binti wa Michuzi, Zahra Michuzi ni DED huko Geita.

Unaweza ukiwa kama DC,RC au hata waziri ambaye ninyi nyote mamlaka zenu za uteuzi ni MOJA hata AVURUNDE vipi, wewe unaweza kumfanya nini huyo binti?

Hivi vyeo vya teuzi kutoka mamlaka moja, havitegemei nani amepewa cheo kikubwa, Bali ni nani ana ukaribu zaidi kwa MTEUZI.

Ndio maana Sabaya akiwa DC alikuwa na mamlaka makubwa kuliko hata RC na mawaziri.

Makonda akiwa RC lakini hata Waziri Mkuu alikuwa anamuogopa.
 
Mkimbiza mwenge hakushtuka?🤣🤣
 
Umebakiza kusema mwanaharakati huru musiba alikuwa anaogopwa hadi na IGP, wee jamaa bhanaa..
 
Kuna nyakati huwa nawaza, kwani kuna ulazima gani wa DED kuwa presidential appointee, kwani haiwezi kutumika njia nyingine kupata nafasi hiyo.
 
Unaificha ili iweje? Umeleta story utazani upo kukimbiza mwenge
 
hapa ndio kuna upigaji kwa kwel fedha za material sio sahihi kabisa wanakula baina ya supplier na viongoz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…