DOKEZO Mbulu DC kuna kikundi kinatumia STAHIKI ZA WATUMISHI! Mamlaka chunguzeni

DOKEZO Mbulu DC kuna kikundi kinatumia STAHIKI ZA WATUMISHI! Mamlaka chunguzeni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kila mwezi halmashauri hupokea kiasi Cha pesa kutoka serikali kuu Kwa ajili ya uendeshaji wa Idara mbalimbali ikiwemo pesa malipo ya mda wa ziada Kwa watumishi, Kuna baadhi ya miezi watumishi hatulipwi pesa ya mda wa ziada.

Kuna miezi walisema pesa zimechukuliwa zinaenda kulipa mwenge, mwezi mwingine wakasema wamechukua wamepeleka kwenye mapokezi ya Raisi kipindi amekuja kwenye kampeni Mkoa wa Manyara.

Mwezi mwingine wakasema wamepeleka vijana Kwa ajili ya kuzima mwenge, na mwezi wa pili mwaka huu wanasema wamepeleka kwenye ziara ya waziri mkuu na kama ya kudumu ya Bunge wasipokuja wilayani kwetu.

Je Halmashauri Haina mapato na bajeti Kwa ajili ya hizo Shughuli? Kwanini wachukue sitahiki zetu?

Tutegemea hizo posho ili zitusaidie lakini baadhi ya watu tena wenye mishahara mkubwa wanajifaidisha Kwa kisingizio hela zimeenda kwenye Shughuli nyingine.

Tunaomba mamlaka za juu zichukue hatua kwa wahusika
 
Back
Top Bottom