Kuna haja ya vyama kutumia helkopta Igunga?

CUF Ngangari

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
273
51
msajili ameweka kiwango cha pesa ya kampeni igunga kwa kila mgombea ni sh 40000000 na jimbo la igunga lina kata 20. usafiri wa helkopta kwa si chini ya 8000000 je? vyama kutumia helkopta hamuoni kuwa ni ubadhirifu wa pesa za ruzuku.
 
Tatizo lako unaleta hoja ambazo hazina mashiko.Kama chama chako cha ccm b kina uwezo wa baiskeli na maguta tumieni.Najua hapa unataka kukichafua chama cha upinzani Cdm.Hakuna lingine lililowapeleka igunga zaidi ya kugawa kura za Cdm ili mshirika wako Ccm ashinde kirahisi.Fahamu watanzania wamebadilika na mbinu hii mlitumie Tarime mkaangukia pua.Tafakari!
 
msajili ameweka kiwango cha pesa ya kampeni igunga kwa kila mgombea ni sh 40000000 na jimbo la igunga lina kata 20. usafiri wa helkopta kwa si chini ya 8000000 je? vyama kutumia helkopta hamuoni kuwa ni ubadhirifu wa pesa za ruzuku.

Kwa vyama vya upinzani ndio vinajijenga kuwafikia watu wote kwa kipindi kifupi kama vina uwezo vitumie helkopta. CCM wapo kila kaya, hivyo wao wanaweza wasitumie helkopta.
 
Chopa ya CCM haiwezi fanya kazi tena kwasababu RACHEL wamegoma na tayari wameondoka na pesa zao RA.
 
Kila chama kinambinu zake za kupiga kampeni,ukitumia gari sawa,pikipiki sawa,helkopta sawa.pigeni kampeni acha visingizio.
 
bujbuj hivi huwa unafikiria wapi? Coz post zako zote zavunja mbavu
 
msajili ameweka kiwango cha pesa ya kampeni igunga kwa kila mgombea ni sh 40000000 na jimbo la igunga lina kata 20. usafiri wa helkopta kwa si chini ya 8000000 je? vyama kutumia helkopta hamuoni kuwa ni ubadhirifu wa pesa za ruzuku.
Kwani tatizo lako nini huwezi kumpangia mtu atumie usafiri gani mnaweza kutumia hata treni kama Kafu mnataka, mwisho utakuja kuwapangia wale makande kila siku kupunguza gharama.
 
msajili ameweka kiwango cha pesa ya kampeni igunga kwa kila mgombea ni sh 40000000 na jimbo la igunga lina kata 20. usafiri wa helkopta kwa si chini ya 8000000 je? vyama kutumia helkopta hamuoni kuwa ni ubadhirifu wa pesa za ruzuku.
Mara hii mmeshaanza kuingiwa kiwewe hata dume lenyewe halijafika likifika je.
 
Raia wa igunga wanataka kiongozi muadilifu na mchapakazi, sio miroketi wala maandamano...
 
msajili ameweka kiwango cha pesa ya kampeni igunga kwa kila mgombea ni sh 40000000 na jimbo la igunga lina kata 20. usafiri wa helkopta kwa si chini ya 8000000 je? vyama kutumia helkopta hamuoni kuwa ni ubadhirifu wa pesa za ruzuku.

Vipi, chama hakina uwezo nini? Semeni tuwasaidie. Sidhani kama imekatazwa kwenye katiba
ya nchi kutumia chopa. Kama uwezo wenu ni wa baiskeli tumieni, kama ni wa bodaboda tumieni,
na hata kama mna uwezo wa kutumia Jet, tumieni ili mradi msivunje sheria za nchi.
 
Hata ungo CUF wanaruhusiwa kutumia maana mnyamwezi+mpemba hakikatizi kitu angani.
 
Back
Top Bottom