Kuna haja ya uchaguzi Rwanda 2017?

jMali

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
8,401
4,965
Kwa kuwa miaka miwili kabla ya uchaguzi ujao 2017, 'Wanyarwanda walio wengi' wameamua kubadilisha katiba ili rais Kagame (na sio mtu mwingine yoyote yule), aweze kugombea urais mpaka 2034, kuna haja ya Rwanda kupoteza fedha kufanya uchaguzi wa rais 2017?

Si wangeufuta tu kupunguza matumizi magufuli style? Hao watakaompa ushindi mtu mwingine zaidi ya Kagame watatokea wapi ikiwa karibu wote wamekubali Kagame atawale mpaka 2034?
 
Hii kauli ya "wanyarwanda walio wengi" ni kiini macho, ni kuwapumbaza wasiofahamu historia na mambo ya Rwanda ili kuendelea kuwaaminisha Kagame ni chaguo la wengi. Kuwa na utashi wa kucheza na vyombo vya habari haitoshi, kwani jamii inayoathirika na utawala wa Kagame itaendelea kujipanga, hata kwa miaka 100 ijayo.
Nikuulize hiyo jamii inayoathirika ni ipi?
Unajua watu mnasema kila wakati hayo maneno wakati wanyarwanda halisi hawayaoni,cha kushangaza Burundi watu wanauwawa usiku kucha sijaona ukikemea hilo.
 
we jamaa ni liongo kweli, kati ya wewe uliopo kwenye key board na wale warwanda waliohojiwa na bbc na itv siku ile ya kura nani anaaminika
 
Hii kauli ya "wanyarwanda walio wengi" ni kiini macho, ni kuwapumbaza wasiofahamu historia na mambo ya Rwanda ili kuendelea kuwaaminisha Kagame ni chaguo la wengi. Kuwa na utashi wa kucheza na vyombo vya habari haitoshi, kwani jamii inayoathirika na utawala wa Kagame itaendelea kujipanga, hata kwa miaka 100 ijayo.

Eti genuine portrayal of Africa kumbe mzalendo kiazi tuu,kusikiliza viazi kama wewe Africa itabaki sehemu ya njaa na mauaji forever,acha Rwanda waende mbele and keep supporting viazi wenzako wa Bujumbura maana ndio akili yenu ilipoishia
 
Mkuu kwa kipindi chote tangu mapinduzi yafanyike, 1994. Serikali ya Paul Kagame imekuwa ikiwahukumu kwa kuwashutumu viongozi kutoka upande wa kabila la wahutu. Vitendo vinavyoendelea vimezorotesha uhusiano ya kijamii nchini Rwanda. Hili sio jambo geni kana kwamba hujawahi kusikia.!!

Mauaji yanatokea sehemu tofauti tofauti duniani, tunatakiwa kujiuliza mauaji ya Burundi yanasababishwa na nini.?? Baada ya kufeli mapinduzi ya kijeshi, wahaini wanatakiwa kuchukuliwa hatua gani.?? Je, Nkurunzinza alishindwa uchaguzi, na baada ya uchaguzi wapinzani walichukua hatua gani.?? Wote tunafahamu asili ya uongozi wa nchi zote mbili; Je kiongozi wa kijeshi aliyefeli mapinduzi alitoka tabaka gani na alipata ushirikiano kutoka taifa gani jirani.??

teh teh teh hiyo ITV ni ya wapi labda, mimi naifahamu ya Uingereza.!! Uongo wangu uko wapi.?? Unafahamu kuwa vituo vya televisheni na mitandao ya kijamii vyote ni vyanzo vya habari.!! Ni baadhi waliohojiwa na televisheni lakini maoni ya wengi yanapatikana kwenye mitandao ya kijamii. Au unahitaji mengine zaidi.??

1:Maendeleo unayo yasikia Rwanda yasingewezekana kama uhusiano wa kijamii ungekuwa mbaya,wananchi wa Rwanda hawana shida na wanaelewana, ndio maana husikii vurugu kama nchi nyingine:
Najuwa kwa hili utasema wanaogopa serikali, lakini kumbuka hata Burundi wanatumia jeshi, ingekuwa uoga hata Rwanda raia wasingeogopa:
2:Godefroid Niyombare ambaye alikuwa kiongozi wa mapinduzi yaliyo fail ni Mhutu na alikuwa mmoja wa ma General katika jeshi la CNDD/FDD la Nkurunziza; sasa sijui taifa unaloliongelea ni lipi;
 
Nikuulize hiyo jamii inayoathirika ni ipi?
Unajua watu mnasema kila wakati hayo maneno wakati wanyarwanda halisi hawayaoni,cha kushangaza Burundi watu wanauwawa usiku kucha sijaona ukikemea hilo.

Wauaji unawajua naamini maana wanatokea hukohuko kagameni!
 
Sasa Godefroid Niyombare yupo wapi ? Na baada ya mapinduzi kushindwa alichukuliwa hatua gani ? Mimi nawashangaa baadhi ya wahutu kuwasaliti wenzao. Hivi unadhani kweli Niyombare ndio angekuwa rais iwapo mapinduzi yangefaulu ? Nyuma ya Niyombare kulikuwa na Buyoya, Sinduhije, Hussein na PAKA mwenyewe kama mfadhili. Mwaka 2003,kulikuwa na mapinduzi ya kijeshi, aliyekuwa kinara wa mapinduzi ni Fran?ais Ngeze (muhutu) lakini hali ilivyotulia tu, Buyoya akadandia kiti cha urais. Ya 2003 ndio yalitaka yatokee tena.
 
Haja ipo japo najuwa Kagame atashinda tena.si wanampenda? Teh teh teh mbona toka tupate uhuru ccm inashinda kila mwaka wa uchaguzi na haijawahi kusitishwa.
 
Mkuu uvumilivu kutoka serikali kuu, ndio kielelezo tosha cha kuonyesha Rwanda iko katika hali gani. Hofu ya kisiasa dhidi ya watuhumiwa wa uongozi wa Kagame haikupaswa kujadiliwa, kama kweli uongozi wa Kagame unahitajika kwa wanyarwanda walio wengi. Kwa nini kila siku wafungwa wa kisiasa wanazidi kuongezeka.??

Na mahusiano ya kijamii hayapimwi kwa kusikia maendeleo au kupitia miradi ya serikali inayofanywa hususan kwa nchi ndogo kama Rwanda inayotoa ugumu wa kutambua maeneo kimatabaka. Namaanisha ijapokuwa hatua ndogo za kimaendeleo zinazofanywa na Kagame, bado jamii ya wahutu ndio wahanga zaidi ukilinganisha na wale wanaompinga kutokana na sera zake.

Burundi inatumia jeshi kwa askari walioasi jeshi, bali Rwanda inatumia mahakama na jeshi kuwahukumu raia wasiokuwa na silaha. Mauji yasiyofahamika yameendelea katika mji wa Kigali na wanasiasa walioonekana kuleta upinzani kwa serikali ya mapinduzi, wamehukumiwa jela kwa muda usiojulikana.

Ndio ni mhutu lakini msaada huu wa mapinduzi uliupata kutoka kwa taifa gani jirani. Ni wazi kabisa Rwanda inahusika na kile kinachoendelea Bujumbura hivi sasa.

Huna hoja wewe umekalia ubishi wa kifala tuu,Rwanda don't need fake analyst kama wewe mnaotafuta umaarufu kwenye keyboards,keep defending viazi wenzako...and ulitaka kuchomekea Tutsi ndio walioongoza mapinduzi wenye data wamekuumbua sasa unakimbilia eti oooh ana support ya Kagame na kabila la Tutsi, whats next Mr very Honestly..?
 
Wauaji unawajua naamini maana wanatokea hukohuko kagameni!

Nyie what you commited 94 hamna mtu mwenye akili timamu atawasikiliza kwa lolote,kelele zenu mnapoteza muda tuu,pigeni kelele tuu ikifika time mtashughulikiwa accordingly
 
Hii kauli ya "wanyarwanda walio wengi" ni kiini macho, ni kuwapumbaza wasiofahamu historia na mambo ya Rwanda ili kuendelea kuwaaminisha Kagame ni chaguo la wengi. Kuwa na utashi wa kucheza na vyombo vya habari haitoshi, kwani jamii inayoathirika na utawala wa Kagame itaendelea kujipanga, hata kwa miaka 100 ijayo.

Mkuu
Mi sijui siasa za rwanda lakini toka 1990 walipo toka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe kagame ameweza kuwaletea maendeleo wananchi wake kiasi ambacho wananchi asilimia kubwa wanamuunga mkono pia ameweza kuwaunganisha na kuwa wamoja.

Corruption Tanzania uko juu kuliko rwanda, development rwanda iko huu kuliko Tanzania, umasikini watanzania ni masikini zaidi na wengi mno kuliko rwanda.

Tuwaachie wenyewe rwandan waamue.
 
Nikuulize hiyo jamii inayoathirika ni ipi?
Unajua watu mnasema kila wakati hayo maneno wakati wanyarwanda halisi hawayaoni,cha kushangaza Burundi watu wanauwawa usiku kucha sijaona ukikemea hilo.

Ya Burundi ndio yatahamia kwa Rwanda.
 
Mkuu
Mi sijui siasa za rwanda lakini toka 1990 walipo toka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe kagame ameweza kuwaletea maendeleo wananchi wake kiasi ambacho wananchi asilimia kubwa wanamuunga mkono pia ameweza kuwaunganisha na kuwa wamoja.

Corruption Tanzania uko juu kuliko rwanda, development rwanda iko huu kuliko Tanzania, umasikini watanzania ni masikini zaidi na wengi mno kuliko rwanda.

Tuwaachie wenyewe rwandan waamue.

Vita vikianza wanakimbilia kwetu,

Hivyo hatuwezi kuwaacha bila kusema neno.
 
Hii kauli ya "wanyarwanda walio wengi" ni kiini macho, ni kuwapumbaza wasiofahamu historia na mambo ya Rwanda ili kuendelea kuwaaminisha Kagame ni chaguo la wengi. Kuwa na utashi wa kucheza na vyombo vya habari haitoshi, kwani jamii inayoathirika na utawala wa Kagame itaendelea kujipanga, hata kwa miaka 100 ijayo.
jamii gani hiyo tena? ya nyinyi mlioamuwa kujifukuza nchini? bora mfie hukohuko, hawa ndi wenye umuhimu kwetu... enjoy it! https://www.youtube.com/watch?v=4m9bVoG9DsE
 
Kwa kuwa miaka miwili kabla ya uchaguzi ujao 2017, 'wanyarwanda walio wengi' wameamua kubadilisha katiba ili rais Kagame (na sio mtu mwingine yoyote yule), aweze kugombea urais mpaka 2034, kuna haja ya Rwanda kupoteza fedha kufanya uchaguzi wa rais 2017? Si wangeufuta tu kupunguza matumizi magufuli style? Hao watakaompa ushindi mtu mwingine zaidi ya Kagame watatokea wapi ikiwa karibu wote wamekubali Kagame atawale mpaka 2034? :bump2:
unafiki umekuzidi kiasi kwamba umeongea point bila ya wewe mwenye kutambua! sasa mbona hii account yako mpya inachemsha sana? cc: vyuma
 
Wewe ni mpuuzi.!! Kwani Burundi sio sehemu ya Afrika.?? Rwanda inaelekea mbele.!! huko mbele ni wapi ambapo hata Victoire Ingabire hafahamu hatma yake.?? Unakaa kutetea serikali ya Kagame kama hujui kabla ya uvamizi wa RPF, Rwanda ilikuwa katika hali gani. Unajitoa ufahamu kuhusu historia ya Rwanda, wakati tuliwapokea kama wakimbizi kipindi cha machafuko yaliyosababishwa na rais wako wa sasa, Paul Kagame.
yani hatma ya extremist INGABIRE VICTOIRE ndio itakupa mwelekeo wa future ya Rwanda? nilikuwa sijuwi kwamba ma extremist mnapendana hivyo! good luck...
 
Mimi ningekuwa Kageme nisingegombea, bali ningelipendekeza chama kimpate mtu mwingine agombee 2017
 
Nyie what you commited 94 hamna mtu mwenye akili timamu atawasikiliza kwa lolote,kelele zenu mnapoteza muda tuu,pigeni kelele tuu ikifika time mtashughulikiwa accordingly

Na nani ? Manyanyaso mnayowapa wahutu wa Rwanda yatakuja kuzaa haki muda ukifika. Burundi mlifanya hayahaya, wananchi wakichagua rais muhutu mnaua, sasa wahutu wa Burundi wamekataa ujinga wenu, ! Wa Rwanda, wapo tu wanawavutia kasi, mtajuta.
 
unafiki umekuzidi kiasi kwamba umeongea point bila ya wewe mwenye kutambua! sasa mbona hii account yako mpya inachemsha sana? cc: vyuma

Mkuu mchambawima1, kwa mara nyingine nakuuliza,jMali alikukosea nini ? Mbona unachuki kubwa sana juu yake ?Au unakasirishwa na ukweli anaousema? Binafsi jMali simfahamu zaidi ya kuona post zake na comment zake! Na katika hayo sioni tatizo kwake maana anayoyasema ni kweli tupu. Hebu tujuze tatizo ni nini ?
 
Mkuu
Mi sijui siasa za rwanda lakini toka 1990 walipo toka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe kagame ameweza kuwaletea maendeleo wananchi wake kiasi ambacho wananchi asilimia kubwa wanamuunga mkono pia ameweza kuwaunganisha na kuwa wamoja.

Corruption Tanzania uko juu kuliko rwanda, development rwanda iko huu kuliko Tanzania, umasikini watanzania ni masikini zaidi na wengi mno kuliko rwanda.

Tuwaachie wenyewe rwandan waamue.
Tanzania inahusishwaje na huu mjadala? Weka facts kudhibitisha madai yako kwamba watanzania ni masikini sana kuzidi wanyarwanda.
 
Back
Top Bottom