Kuna haja ya kuwazindika watoto wetu

Habari zenu wakuu

Alhamis hasubuhi nimewahi K/koo ofisini (uwakala)na nimefungua ofisi na kuanza kazi nimehudumia kama wateja watatu au wa nne nimekaa kwenye kiti naona panaanza kuwa kimya mara sisikii sauti ya kiumbe chochote wala magari yaani kimya na naanza kusikia mwili baridi sana ubaridi sio wa kawaida ilhali kulikuwa na jua kali sana siku hiyo.

Naona vizuri lakini nikigusa kitu sihisi kama nimegusa tofauti na vitu nilivyonavyo mfukoni na nguo nilizovaa ndio vinashikika.. sikujua hali gani inanikuta nilichukulia kawaida tu labda hali ya mda tu na itapita nitakuwa kawaida nilikuwa mtu kama ambaye anaota ivi ile mood ya ndoto naona rangi fulani hivi kama mwanga uliofifia.

Mara anakuja dada ambaye ananihudumiaga chai anasukuma mlango anaingia mpaka ndani mimi namuona vizuri lakini yeye anaonekana kama anioni mara naanza kusikia sauti tena kwa mbaali ananiita “” kaka “” mara ananiita jina langu “” tena anajisemea hapa hakuna mtu” namuitikia anasema hii sauti inatokea wapi!? Anaita tena kaka mara anaondoka na anajisemea wamefungua ofisi wameacha wazi kisha wameondoka .. na akaondoka” akili haikushituka kabsa” sikujua nini? Kinaendelea

Baada ya masaa kadhaa naona gari ya boss inajiegesha kwa nje kisha boss anashuka ndani ya gari na kuingia ofisini na kuwa kama mtu anatafuta mtu mule ndani na ananipita bila kunisemesha chochote na kujisemesha “dogo leo amekuaje? Amefungua ofisi alaf ameondoka “mara kwa mbali simu yangu inaita na kuiangalia ananipigia boss aliyekuwa namuona ndio nikagundua kuwa hanioni na pia yule dada wa chai hakuniona nikatoa sim mfukoni na kujaribu kupokea ikapokeleka na kumsikia boss anauliza upo wapi! Na namjibu nipo ofisini ananambia kuwa anisikii vizuri kumbuka namuona kabsa, akawapigia wafanya kazi wake wengine walikuwa mtaa pili kutoka pale na kuwaita pale ofisini kwangu mda si mda wakafika.. najaribu kuwaongelesha naona hawanijibu.. nkaanza kulia kwa kudhani kuwa nimeshakufa, lakini najisemea mtu akifa anakuwa hivi kweli.

Nikakumbuka kusoma dua mbili tatu, nikasoma sana mara kidogo nikakumbuka kwanini? Nisimpigie simu mama nimuelezee, kweli nachukua simu nampigia mama mara ya kwanza haikupokelewa, ikakata mara ya pili pia haikupokelewa na mara ya tatu na ya nne haijapokelewa nikazidi kulia nikajisemea sasa ndio nimeshakufa tena nikabaki kulia wale wafanya kazi na boss wanajadili leo nimekuaje!? Nimeacha ofisi na kuondoka nawasikia kila kitu ila wao hawanisikii na nikijaribu kuwagusa hawagusiki nikajaribu kumpigia boss namuona anapokea naongea anasema sikusikii naongeza sauti ananambia nakusikia lakini sikuelewi unaongea nini? Nakata simu nalia“ila najisemea mtu akifa awezi kushika simu na najiuliza mbona tofauti na simu vitu vingine nikishika havishikiki wala havisogei.. nalia tu bila ya kujua nini? Nifanye!

Mara paaap” simu yangu inaita jina “MAMA” napokea huwa tuna desturi ya kusalimiana salamu ya kidini ilee napokea simu tu.. MAMA ananisalimia ile salaam” namuitikia ghafla namuuliza unanisikia “ ananijibu ndio nakusikia.. ananambia haunaga kawaida ya kupiga simu mara mbili kama haikupokelewa leo vipi?” Sikujibu mara nalia “ Mama ananiuliza vipi! Umepatwa na nini! Mara nae analia “ na kunibembeleza kuwa niseme tatzo nini? Badala ya kulia “” ndio naanza kumsimulia mkasa mzima mpaka nilipofikia hapo “” nayeye anaanza kulia kisha kuniambia “ kuwa anampigia BABU simu kisha atanipigia mda si mrefu na kuniambia nihakikishe simu yangu isizime charge.. ndipo navuta pumzi na kushukuru na kuendelea kusoma dua... nikiomba mama awahi kunipigia “” maongezi yanaendelea pale ofisini kati ya boss na wale wafanyakazi wengine kuhusu mimi nipo wapi? Na kuacha ofisi wazi kisha kuondoka..

Mara baada ya dakika chache simu yangu inaita baada ya kuangalia jina ni mama na kupokea mara anaanza kuniuliza maswali na kunipa maelekezo jinsi ya kufanya” kaniuliza mazingira niliyopo kuna watu wangapi? Jinsia gani? Wangapi na kuniambia kwamba nisikate simu nitoke nje na nitafute sehemu kwenye majani yeyote yale yaliyojiotea niyashike alaf nipate maelekezo tena kutoka kwake.. nikamjibu sawa.. kazi ilikuwa kufungua ule mlango yaani ni haushikiki nikijalibu kuu-vuta yaani mkono unaingia na unapita tu na nikajaribu kupita kwenye kioo kwa mfano wa mimi kivuli sipiti, ikabidi nisubiri mtu atoke nitoke nae, nilisubiri sana lakini wapi? Mara simu mama nasikia anaongea kuniuliza vipi? Nikamuelezea jinsi inavyokuwa akanambia sawa, mara akanambia kama kuna maji humo ndani yasogelee.. Kuna chupa ya maji pale najaribu kuishika hakuna haishikiki.

Mara nakumbuka kuwa kuna ndoo ya maji ya yanayotililika kutoka kwenye AC ipo wazi .. nikajibu simu nikamwambia nimepata maji” akanambia “nawa hayo maji mikono na uso nikafanya hivyo akanambia haya nenda kafungue mlango naenda najaribu kufungua mlango unakubali... naanza kutafuta sehemu iliyojiotea majani” niliangaika sana hatimae nikaipata na kumwambia naona majani hapa akaniuliza “mazingiara yakoje nikamwambia akanambia wewe likamatie hilo jani tu mpaka tutakapokupa maelekezo.. kweli ... nikakamata jani kwa mda mrefu nikapitiwa na usingizi na nikaanza na kuota ndoto ghafla nikashtuka.. na kuanza kuona na kusikia kawaida.

Nikavuka barabara na kwenda pembezoni kidogo kwenye mkusanyiko wa watu na kumsalimia mtu akaniitikia na kuniambia kuwa nina vumbi nijisafishe, nikajaribu mtu wa tatu na wanne wameniitikia na kusikilizana ndipo nikatafuta sehemu na kukaa na kumpigia mama na kuanza kumwambia kuwa sasa najihisi nipo vizuri na nikamwambia nataka nielekee ofisini” akanambia usiende ofisini “ tushampigia simu boss wako na kumjuza nini? Kinaendelea chukua bajaji na uanze safari ya kurudi nyumbani sisi tutalipa kama hauna pesa.. kweli naenda kuongea na jamaa wa bajaji kweli namuongelesha ananiitikia na kugundua tunasikilizana na kumueleza nataka niende wapi? Ananambia bei na kuanza safari hatimaye tukafika na wazee kumlipa mwenye bajaji.

Na kuniambia nikaoge na kunipa nguo za kuvaa tofauti na zile na wakachukua simu zangu zote.

Baada ya kupumzika nikawauliza nini? Kilichonikuta; dunia ina mambo mengi kwa hivyo watu tu walikuwa wanajaribu kukuzubaisha ila usijari kwa sasa upo poa.. na mambo mengine ya kiufundi nikafanyiwa.

Heshima kwa maji imeongezeka na majani pia imeanza kwa kasi sana naogopa hata kuyakanyaga majani bila sababu ya msingi..

Dunia sio mbaya ila walimwengu ndio wabaya.
DUUUUH
 
Back
Top Bottom