Kuna haja ya kupunguza Masihara.

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,659
3,572
Kuna vitu vingi vya kushangaza lakini vipo pia vinavyoonekana ni vya kawaida lakini vinashangaza kutokana na matumizi yake.
Naomba nieleweke mapema kuwa sipingi suala la masihara ila ninachokiona kama kero ni kupitiliza kwa masihara kunakoonekana kuwa kawaida.
Nimekuwa Mwanachama wa Makundi mengi ya Mitandaoni ila nilichojifunza kinanipa ukakasi mwingi sana nikiangalia hali ilivyo na namna tunavyopaswa kuwa na kuwekeza ili kupiga hatua nzuri zaidi.
Leo kuna makundi mathalani ya Whats App licha ya kuwa na kusudi la kuanzishwa kwake yametawaliwa na masihara kwa kiasi kikubwa mno kuliko masuala yanayotawala uanzishwaji wa makundi hayo.
Masihara yamekuwa ni sehemu kubwa siyo tu kwenye makundi ya Whats App bali hata makundi mengine na imefikia hatua hata kujadiliana suala la muhimu kwa dakika kumi bila masihara kwa lengo la kutia umakini katika hoja limekuwa suala gumu mno kwa wengi.
Leo kuna watu wanahofia hata kutoa mawazo yao mazuri kwa kutumia njia ya mitandao kwa kuhisi tu wataibuka watu na masihara na kejeli na kwa sababu ni wengi huenda hata ujumbe muhimu usijadiliwe kwa kina.
Masihara ni sehemu ya kuliwaza akili lakini yanapotumika kiholela yanalemaza akili na kukuza husia za kupenda kujiliwaza au hata kujifurahisha badala ya kufikiri kwa kina.
Ninajiuliza kwa sauti ya chini sana ni lini vijana wetu watakuwa na mijadala kintu itakayozaa hoja za msingi zilizoshibishwa fikra bainifu na mawazo tofautitofauti kutokana na makundi yaliyopo mitandaoni?..je Mitandao ni kwa ajili ya kupata taarifa na kujifurahisha tu na marafiki pasi kuwa na uwanja wa fikra pevu?
Simaanishi kuwa wote ni wapenda masihara ila ninachotaka kukionesha hapa hali ambayo wengi imewachukua na kuwafanya waione kuwa kawaida katika maisha yao.
John Dewey anaamini kuwa "vionjo tofautitofauti ndiyo ladha ya maisha"..(varieties is the spice of life) hapa nataka kujitabainishha kuwa katika mijadala fikirifu inawezekana kuibuka kwa mawazo tofauti tofauti na wakati mwingine masihara ila masihara hayapaswi kuwa ndiyo hoja ya msingi labda mjadala uwe umelenga kujifurahisha akili kwa njia ya masihara.
Kila jambo linapaswa kuwa na kiasi hata mijadala fikirifu ninayoiunga mkono inapaswa kuzingatia kiasi ila pale masihara yanapozidi kiasi kuna uwezekano mkubwa wa Watu kushindwa kujadilina masuala nyeti na ya muhimu kujadiliwa kwa kina na kwa pamoja.
Leo kuna Watu licha ya kuwa ni Washiriki katika Makundi mengi Mitandaoni wameacha kabisa kujadiliana na wanachokifanya ni kuangalia Majadiliano yanayoendelea kwenye makundi hayo pasi na kuchangia mawazo yao kwa kuhofia masihara na kejeli au uvurugaji wa majadiliano hata majadiliano kuntu.
Mitandao ya Kijamii inaweza kutumika kwa shughuli nyingi mno mathalani shughuli za Kisiasa,Kiuchumi,Kijamii na Kiutamaduni na shughuli zote hizi zinategemea namna watu wanavyotumia mitandao hiyo kwa malengo.
Simu yako au Kompyuta mpakato yako inaweza ikawa ni sehemu kubwa sana ya wewe kujijenga katika nyanja zote au kujivuruga na kupoteza muda na pesa.
Ili kuhakikisha tunajifunza kuzingatia na kuheshimu raslimali muda tunapaswa kuangalia sana na muda tunaoutumia kwenye mijadala yetu.Je tunatumia muda mwingi kwenye masuala yapi na yana faida ipi kwetu katika nyanja zote? Na tunapaswa kufanya tathmini juu ya muda tunaotumia kwenye majadiliano yetu kwa kuangalia tunajadili nini? Kwa kiasi gani tutatia umakini katika kusudi na kufikia lengo la mijadala yetu?
Hatupaswi kujisifu kwa asilimia 70 ya Watanzania wanamiliki simu na wengi wao leo wanatumia Smartphone ila tujiulize wanatumia simu kuzalisha nini?je mijadala ya vijana leo kupitia mitandao ya Kijamii inazalisha nini kipya kitakachotufanya tupige hatua zaidi?.
Kuna haja ya kuitathmini mijadala yetu kwa kina sana katika kipindi hiki kuliko kipindi chochote kile kwa sababu ya Muono wa Taifa letu "National Vision 2025".
Tunapaswa kuangalia Taifa linataka kuzalisisha Watu wa namna ipi na kuwa Taifa la namna ipi na baada ya kujua hilo tunapaswa kuishi maisha ambayo Taifa linataka Watu wake wawe .Taifa limetamka kutaka kuwa la watu wasomi learned society" sasa tujiulize tunajifunza nini kwenye mijadala yetu inayoendelea ukiwepo na huu niliouanzisha na je mijadala yetu inatupeleka wapi?
NARUDIA TENA SIPINGI SUALA LA MASIHARA KWA KUONESHA KUWA NI BAYA SANA AU HALIFAI NA PIA SIMAANISHI KUWA NATAKA KUINGILIA UHURU WA WANAOPENDA MASIHARA AU KUFANYA MASIHARA KAMA BIASHARA ILA NINACHOMAANISHA NI KUWA NA KIASI NA KUTOFANYA MASIHARA KUWA HOJA YA MSINGI KATI MAKUNDI AMBAYO LENGO LAKE SIYO UTANI AU MASIHARA.
 
Wanaofanya kazi na wewe watakuwa wanakukoma aisee, nahisi we jamaa ni mnokomnoko sana. (Nawaza tu)

Sent using Jamii Forums mobile app
Mawazo tu Kaka ila watu wanaweza kumtafsiri Mtu kwa namna tofauti wanavyomuona nashukuru umekuwa muwazu kuonesha picha iliyokujia akililini kutokana na andiko langu.
 
Umeandika Mkeka mrefu.
Huwezi ku Summarize???

Back
Top Bottom